Wanaume wa Dar! Mitaa mitatu Mnatekwa na Panya Road?

Wanaume wa Dar! Mitaa mitatu Mnatekwa na Panya Road?

Watu wanakuja kuja tu kuanzisha uzi. Watu kumi wako na mapanga hata john cena hafui dafu.

Keyboard warriors wa mchongo
Tena wakija hivyo ni mabhangi kichwani ndo yanawaongoza yaani kukupasua sehemu haoni shida , hapo we usiye na chochote utakaa tu ushindane nao ili mwisho wa siku usifiwe ni mwanaume wa Dar umepambana. Lol.
 
Mitaa mitatu yote kutekwa kwa wakati mmoja huko chanika,bila hata Panya mmoja kukamatwa au kujeruhiwa.

Hili jambo nashindwa kulielewa kabisa!

Nafikiria ingekuwa vipi kama hao Panya road wangejaribu huo ujinga huku mikoani.

Sijui kama wangekuwa hai mpaka saa hii!

Wanaume wa Dar es salaam jifunzeni ukakamavu maana ni jukumu la kila Baba kuilinda familia yake.
Utoto wa Hali ya Juu,afu hao watoto Wana mapanga tuu
 
Hawa watoto wanatakiwa warudishwe kuzimu walipotoka, wanaume wa dar vipi
 
Rorya sehemu kubwa ya watu wanaendesha maisha yao kwa kutumia nguvu

Dsm sehemu kubwa ya watu wanaendesha maisha yao kwa kutumia akili

kuliko kwenda kupambana na panya road na kuhatarisha maisha yako Bora umuache abebe hizo TV sijui simu kwa kuwa hajaiba wala kujeruhi akili yako una uhakika wa kuvipata tena

hivi upambane kuokoa simu ya laki 6 kwa gharama ya bisibisi ya kwenye jicho?

Huko rorya mna haki ya kupambana kwa sababu mapambano hata ya kupata ugali wa siku asilimia 96% ni manguvu na 4% ni akili …sie huku ni kinyume chake
(mtaniwia radhi watani zangu wa kijita na kijaluo)

wenzenu hulu hata mambo ya ugomvi ugomvi wa kupigana yalishaisha…mtu akikuzingua hata kama una mmudu unamtaftia elf 50 unapeleka Polisi post unawapa hilo jukumu hii ikimaanisha hata kumpiga adui yako unaagiza na kuamuru Chombo cha dola
Urojo rojo
 
Kwanza bei ya bastola sio kubwa sana maana mpaka ukiwa na laki saba au nane unapata.

Tatizo ni msahariti ya namna ya kuipata. Maana unaanzia ngazi ya mtaaa mpaka mkoa na mamlaka husika ili kuipata kuimiliki kihalali. Hii inakiwa kikwazo kwa wananchi kujilinda maana vibaka wanadhalilisha watu na kuibia mali..

Fukiria mtu anabakwa mbele ya mke wake au mke wake na watoto wanabakwa na kuibiwa mali na vijana wa miaka 12 mpaka 18 kisa tu ni wavuta bangi na walioshindikana ki malezi.

Wanaume wa Dar wasaidiwe.
Acha hayo mambo mkuu kuna rafiki yangu familia yake yote ilibakwa aisee alafu yy hakuwepo Home. mkewe na watoto wake watatu wakike wote walibakwa hawa vijana niwakuua kabisa
 
Comments sasa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mitaa mitatu yote kutekwa kwa wakati mmoja huko chanika,bila hata Panya mmoja kukamatwa au kujeruhiwa.

Hili jambo nashindwa kulielewa kabisa!

Nafikiria ingekuwa vipi kama hao Panya road wangejaribu huo ujinga huku mikoani.

Sijui kama wangekuwa hai mpaka saa hii!

Wanaume wa Dar es salaam jifunzeni ukakamavu maana ni jukumu la kila Baba kuilinda familia yake.
Nyie mnaoita vigarasa wa Dar 'wanaume wa Dar' mnafanya makosa.....wale si wanaume wa ukweli. We umeona wapi mtu/mwanaume anakbali kuongozwa na Steve Nyerere?
 
Kabla hamjawalaumu inatakiwa mjue hao panya road wakija huwa wanakuja vipi?
Wanazuka ghafla kama magaidi wanafanya ambush mida ya saa kumi na mbili hadi saa mbili wakijua mida hio wanaume wapo makazini.wanakuwa watoto kuanzia miaka 14 hadi 30 jumla huwa ni kundi kuanzia watu 20 hadi 50 wakiwa na silaha baridi mfano wembe,bisibisi,panga,visu.Wakishambulia watu wanaokutana nao mtaani wakiwapora na kuwajeruhi, ukiona kikundi cha watoto mida hio unaweza dhambi wametoka mpirani huwa wanafujo na makelele.Wanashambulia police wakija wanatawanyika.Ni watoto wa mtaani wanaojilea wenyewe baada ya wazazi wao kufeli malezi.
Jamii ikiwa na umoja inaweza wadhibiti ikiwemo hata kuwarejesha kuzimu walipotoka ikiamua.
Kazi ya police ni kuja kuchukua maiti wakafukie na siyo kupambana na panya.Mitaa yenye umoja,mitaa iliyopangika kwa mstari huwa haisumbuliwi na panya wala vibaka maana awapendi kufukuzwa mda mrefu kwenye mitaa iliyonyooka.Thus wanapenda uswahili sababu ni rahisi kuescape maana KILA nyumba ni uchochoro.
 
Kwanza bei ya bastola sio kubwa sana maana mpaka ukiwa na laki saba au nane unapata.

Tatizo ni msahariti ya namna ya kuipata. Maana unaanzia ngazi ya mtaaa mpaka mkoa na mamlaka husika ili kuipata kuimiliki kihalali. Hii inakiwa kikwazo kwa wananchi kujilinda maana vibaka wanadhalilisha watu na kuibia mali..

Fukiria mtu anabakwa mbele ya mke wake au mke wake na watoto wanabakwa na kuibiwa mali na vijana wa miaka 12 mpaka 18 kisa tu ni wavuta bangi na walioshindikana ki malezi.

Wanaume wa Dar wasaidiwe.
Mkuu Kuna vitu vigumu kuvipata vya mabilioni huko

Kitu Cha laki Saba unasema kigumu kupata.

Tatizo mmezoea kila unachotaka kununua unadai risiti ,itakuwa ngumu kufanikisha
 
Dar kuna uzembe sana. Mitaa watu hawana ushirikiano kila mtu kwake. Watoto wadogo wanafanya mlale saa moja? Wanaume wa nyumba tano tu na mapanga mnawageuza bucha hao madogo na hairudii tena.
 
Wakuu wote na mtoa mada ni kwamba mfumo wa maisha kwa watu wa Dar es Salaam ndio unawafanya kudeal na hawa watu kuwa tabu.
UMOJA unakosekana kwa sababu Dar kila mtu yuko busy sana tofauti na mkoa.

Kwa mkoani watu kuwa tayari kuacha shughuli zao na kudeal hao viumbe ni rahisi sana kutokana na umoja.

Umoja, umoja, umoja, umoja.

Kijijini kwetu Mufindi miaka ya 2012 majambazi matatu yenye bunduki yaliuawa na wananchi wenye mundu na mafyekeo tu na wala hakuna mwananchi aliyedhurika tena usiku wa manane.
Tukio lilikuwa kijijini mkonge. Kwa wenyeji wa kule kama mzee N'yadikwa wanakijua.

Baada ya kuvamia kwa mzee fulani mfanyabiashara na baada ya uzembe wao wa kufyatua risasi watu walisikia basi simu zilipigwa kila mahali. Barabara za mdabulo, sawala mtwango zilifungwa kabisa ili wasiweze toka na pikipiki lao.
Huwezi amini mzee fulani alijificha pembeni ya road wakiwa ndio wanakimbia alirusha mundu yake hadi ikajipachika kwenye tairi la nyuma wakaanguka. Kilichotokea ni historia hadi leo.

Watu waliopigiwa simu toka sawala wanafika kutoa msaada na silaha za jadi ambazo mimi sijawahi hata kuziona toka nizaliwe wako kwenye mafuso wamekuja kutoa msaada.

Nb: mfumo wa Dar es Salaam watu kutojuana na kila mtu kuwa na hamsini zake na kutojuana ndio unawacost.

Umoja, umoja, umoja. [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom