Wanaume wa Dar! Mitaa mitatu Mnatekwa na Panya Road?

Watu wanakuja kuja tu kuanzisha uzi. Watu kumi wako na mapanga hata john cena hafui dafu.

Keyboard warriors wa mchongo
Tena wakija hivyo ni mabhangi kichwani ndo yanawaongoza yaani kukupasua sehemu haoni shida , hapo we usiye na chochote utakaa tu ushindane nao ili mwisho wa siku usifiwe ni mwanaume wa Dar umepambana. Lol.
 
Utoto wa Hali ya Juu,afu hao watoto Wana mapanga tuu
 
Hawa watoto wanatakiwa warudishwe kuzimu walipotoka, wanaume wa dar vipi
 
Urojo rojo
 
Acha hayo mambo mkuu kuna rafiki yangu familia yake yote ilibakwa aisee alafu yy hakuwepo Home. mkewe na watoto wake watatu wakike wote walibakwa hawa vijana niwakuua kabisa
 
Comments sasa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nyie mnaoita vigarasa wa Dar 'wanaume wa Dar' mnafanya makosa.....wale si wanaume wa ukweli. We umeona wapi mtu/mwanaume anakbali kuongozwa na Steve Nyerere?
 
Kabla hamjawalaumu inatakiwa mjue hao panya road wakija huwa wanakuja vipi?
Wanazuka ghafla kama magaidi wanafanya ambush mida ya saa kumi na mbili hadi saa mbili wakijua mida hio wanaume wapo makazini.wanakuwa watoto kuanzia miaka 14 hadi 30 jumla huwa ni kundi kuanzia watu 20 hadi 50 wakiwa na silaha baridi mfano wembe,bisibisi,panga,visu.Wakishambulia watu wanaokutana nao mtaani wakiwapora na kuwajeruhi, ukiona kikundi cha watoto mida hio unaweza dhambi wametoka mpirani huwa wanafujo na makelele.Wanashambulia police wakija wanatawanyika.Ni watoto wa mtaani wanaojilea wenyewe baada ya wazazi wao kufeli malezi.
Jamii ikiwa na umoja inaweza wadhibiti ikiwemo hata kuwarejesha kuzimu walipotoka ikiamua.
Kazi ya police ni kuja kuchukua maiti wakafukie na siyo kupambana na panya.Mitaa yenye umoja,mitaa iliyopangika kwa mstari huwa haisumbuliwi na panya wala vibaka maana awapendi kufukuzwa mda mrefu kwenye mitaa iliyonyooka.Thus wanapenda uswahili sababu ni rahisi kuescape maana KILA nyumba ni uchochoro.
 
Mkuu Kuna vitu vigumu kuvipata vya mabilioni huko

Kitu Cha laki Saba unasema kigumu kupata.

Tatizo mmezoea kila unachotaka kununua unadai risiti ,itakuwa ngumu kufanikisha
 
Dar kuna uzembe sana. Mitaa watu hawana ushirikiano kila mtu kwake. Watoto wadogo wanafanya mlale saa moja? Wanaume wa nyumba tano tu na mapanga mnawageuza bucha hao madogo na hairudii tena.
 
Wakuu wote na mtoa mada ni kwamba mfumo wa maisha kwa watu wa Dar es Salaam ndio unawafanya kudeal na hawa watu kuwa tabu.
UMOJA unakosekana kwa sababu Dar kila mtu yuko busy sana tofauti na mkoa.

Kwa mkoani watu kuwa tayari kuacha shughuli zao na kudeal hao viumbe ni rahisi sana kutokana na umoja.

Umoja, umoja, umoja, umoja.

Kijijini kwetu Mufindi miaka ya 2012 majambazi matatu yenye bunduki yaliuawa na wananchi wenye mundu na mafyekeo tu na wala hakuna mwananchi aliyedhurika tena usiku wa manane.
Tukio lilikuwa kijijini mkonge. Kwa wenyeji wa kule kama mzee N'yadikwa wanakijua.

Baada ya kuvamia kwa mzee fulani mfanyabiashara na baada ya uzembe wao wa kufyatua risasi watu walisikia basi simu zilipigwa kila mahali. Barabara za mdabulo, sawala mtwango zilifungwa kabisa ili wasiweze toka na pikipiki lao.
Huwezi amini mzee fulani alijificha pembeni ya road wakiwa ndio wanakimbia alirusha mundu yake hadi ikajipachika kwenye tairi la nyuma wakaanguka. Kilichotokea ni historia hadi leo.

Watu waliopigiwa simu toka sawala wanafika kutoa msaada na silaha za jadi ambazo mimi sijawahi hata kuziona toka nizaliwe wako kwenye mafuso wamekuja kutoa msaada.

Nb: mfumo wa Dar es Salaam watu kutojuana na kila mtu kuwa na hamsini zake na kutojuana ndio unawacost.

Umoja, umoja, umoja. [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…