Wanaume wa siku hizi ni waoga kueleza hisia zao

Unaweza ukadhani watu wameacha kutongoza kwa kasi kumbe we ndio umri umeenda wameacha kukufuata wanataka young age 😅
 
Umefanya utafiti? Au umeangalia wale wachache waliokuface wewe!? Watu tuna confidence asikuambie mtu.
Sema wakati mwingine ni aibu yakukataliwa Ndo inatuzuga wengi yaan umeenda kwa binti umeshusha verse alafu anakuambia sikupendi au Sina hisia na wewe dah! Hili jibu lisikie tu yaan.
Akikuambia hivo lazima ujikague yaan mwisho wa siku ndo inakuja Ile sijui nikimtongozea nin.
Ila ifike wakati wanaume tuzoee haya majibu.
 
Hiyo ni kweli huu ni ukweli mtupu,naomba serikali hii suala waliangalie ikibidi wapeleke bungeni wakajadili
 
Poleni aisee.
Lakini nlichojua mnaogopa kukataliwa.feeling yake ikoje baada ya Hilo jibu?
 
Mapenzi yamegeuzwa biashara huria sasa mnatongozana kitu gani badala ya kubargain tu?

Wanawake wanaojitambuwa na kuthamini utu wao kwa sasa ni wachache wengi wao ni majangili tu.

Mimi nawaheshimu sana wanawake wanaojiuza maana wako really wanauza utamu usimfate na sound anataka pesa.
 
Walikua wanawatongoza kiujasiri mkasema watafte hela,,wako bze kutafta hela ili mjiongeze wenyewe tena mnawasema,iv mnataka nn nyie viumbe hai😂
 
Usiangalie upande mmoja tu, wanawake wenyewe wa kutumia nguvu hizo siku hizi wachache sana. Kitoto cha elfu 2 kinakukazia macho wala hakiangalii pembeni kumaanisha kinajua pengine hata kukuzidi.

SIku hizi mambo ya kutumia nguvu kufukuzia yanapungua kwa kasi sana.
 
Nijuavyo mimi kutongoza ni sanaa.
Jifunze kutongoza mahali sahihi na muda sahihi.
Ukiyajua haya mawili hakuna ndoano itakosa samaki
 
Nijuavyo mimi kutongoza ni sanaa.
Jifunze kutongoza mahali sahihi na muda sahihi.
Ukiyajua haya mawili hakuna ndoano itakosa samaki
Mzee naona uko busy kutoa semina Kwa vijana[emoji1][emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…