Wanaume wanaoijua hii Baiolojia ya wanawake ni wachache sana

Ndio maana umepata likes nyingi kuliko mtoa mada. Ongeza na hili, wanawake wa zamani hawakuwa na hizi tabia za kiburi, jeuri maneno nk, hasakuwa wanapata hedhi?
 
Kumbe mtoa mada ni mwanamke. Hakuna kitu humu, pumba tu
 
Wanawake wengine wanatakiwa wake kujifunza hapa ili wajue jinsi ya kuzidhibiti hisia zao pindi wawapo kwenye siku zao.
 
Duh. Ongera sana. Ni ukweli umeongea. Percent ya watu wengi wapo na matatizo ya akili. Yaani kuwa na kimahusiano yahitaji uvumili na kuchukuliana. Shida maisha yapo speed sana hivyo watu hawana muda wa kuchukuliana. Mtu anaweza kukujibu madudu lkn ulikaa na kufikiria utaona huyu si akili yake. Uvumilivu umeisha kwenye Karne hii. Hii ni wote waume Kwa wanawake. Mwanamke wa Sasa akiona mwanaume Hana pesa uvumilivu hamna. Pia Mwanaume naye akiona mwanamke Hana utii uvumilivu hamna.
 
It's a lie. Mimi Ni mwanamke nimezaa watoto wanne. Hiyo kusema mimba inabadilisha mood ya mwanamke sio kweli Basi Tu vile watu wanasikia kwa waliopita na wao wanajifanyisha. Kwenye hedhi nakubali kwa asilimia ndogo kwa wale ambao wakiwa kwenye Siku zao wanapata maumivu makali. Hii ya mimba eti simpendi mtu Fulani Ni uongo kijifanyisha au chuki binafsi tu isiyokuwa na connection na mtoto aliyetumboni.
 
Mimi ni nacho jua ni hivi mwanamke anapo kua kwenye siku zake anakua muoga zaidi na mwenye aibu na utii kwa mumewe au mpenzi wake kuliko kawaida yani utapendwa sana mpaka uhisi dunia ni yako japo wanakua na hasira kwa mbali ukimkwanza ila wanauka wa nyenyekevu sana, sasa ukiona wako anapokua kwenye siku zake anakua na kiburi, hasira kupita kiasi, gubu, ananuna, mjeuri mpaka basi jua hakupendi wala hakutaki anatumia kigezo cha siku zake kukuonyesha jinsi alivyo..

Kinacho weza kumfanya mwanamke awe hajitambui kisaikolojia na kimaamuzi ni mimba tuu na hapa hua tunajua mkituectia tunajua pia

Sasa msiseme hamjaambiwa
 
Clepatina nimekuelewa sana. Wakati nasoma uzi huu kanijia kichwani mzazi mwenzangu ambaye tumeachana. Ukweli ni kuwa hadi leo huwa sielewi aliligwa au ndio haya mapito. Nachojua changamoto zilianzia wakati wa ujauzito na alipojifungua mambo yakawa mengi
 
Umeandika Vzuri Wanaume Tumeumbiwa tuishi Na Nyinyi Kwa Akili Hapo Kwenye Akili Ndo Yapo Yote Uliyoandika Wewe
 
Mbona mahausi geli wakiwa na mimba hawanaga hizo mbwembwe ulizosema ni kujiendekeza na kudeka kusiko kuwa na maana!!!
 
Yote uliyoandika ni sahihi na nimejionea haya. Kuna dada mmoja tukiwa chuo akiwa katika siku zake alikuwa na mihasira na ana majibu ya hovyo hataki ushirikiano kabisa anapenda kujitenga wakati mko group discussion moja ya seminars. Lakini siku zake zikiisha anakuwa mtu poa sana. Baadaye yeye mwenyewe alikuja kutuomba na kutuambia hali anayopitia anapokuwa hedhi hivyo tumuelewe

Na hiyo ya pili mambo kutriger after delivery hiyo ndio usiseme nina experience nayo balaa. Ni kweli wanaume kuna wakati tunaoa vichaa haijalishi ana uwezo wa akili darasani wa kiwango gani. Anaweza kuwa anapasua na kupata divisions na GPA za juu ila ndio ana umoko fulani, kiasi kwamba kakitokea kakitu ka kum boost kichaa chake anageuka kuwa sio yule uliyemfahamu wakati unamuoa. Na hapa ndio panahitaji hekima ya mwanaume maana yeye kuna wakati anakuwa hajitambui na unaweza hisi anajifanyisha.
 
Tuweke akilini kuwa binadamu hatufanani. Sasa turudi kwenye uongo uliuona, vipi kuhusu mwanamke kutapika sana wakati amebeba mimba huwa mnajifanyisha? Kuna uhusiano gani kati ya kubeba mimba na kichefuchefu? Au mnakuwa mlisikia kwa waliopita basi mnafuata mkumbo na nyinyi mnaanza kutapika?[emoji848]
 
aise umepita mule mule nilipftaka kupita
 
Hii Ni dawa
 
Hizo hormones zenu kwa kweli zitakuja kutuua,mi demu angu akijaga home akiwa kwenye period,huwa anaoga zake anaweka nywele zake safiiiiii,anavaa nguo safiiii yaaani kila kitu kisafi..ila sasa ananuna siku nzimaaa unaambiwa,mpaka naanza kumbembeleza akati sijamkosea,sema namjulia huwa najua ni mood tu..
 
Mwandishi ameileta mada sijajua ni kwa mtazamo wake ama ni research kafanya. Kuna vilivyo katika uhalisia, lakini kwa dunia ya sasa naomba nami nitoe maoni haya.
Hii mambo ya hormone and stuff imetupelekea mpaka kuwa na uchafu katika dunia ya leo.

Yes mwanamke ana challenges yanapotokea mabadiliko mwilini katika mizunguko, BUT, hiki si kigezo cha mtu kuwa rude, kiburi, jeuri, gubu and stuff like that. Hivi kweli Mungu kachukua muda wake mzuri kuumba mwanadamu kwa ustadi tena kwa mfano wake. Ni yeye ndie alieziweka hizo hormone mwilini mind.

Hizi tabia mbaya tunazojipa nazo moyo kwamba ni sawa kwa sababu tuna hormone its a lie. Kila mwanadamu ana hormone. Tunatakiwa kutiisha miili yetu. Miili yetu inatakiwa iwe dhabihu hai, takatifu mbele za Mungu. Miili yetu ilishakufa pamoja na Kristo na tukafufuka pamoja nae. Ni HATARI kuruhusu mwili ukutawale.

Kuna circumstances najua zipo lakin sio ndo tuendekeze wapendwa. Kuna dada yangu mmoja alishanipiga stop kabisa kuhusu mambo ya drama za mimba ama period. Akaniambia siamini na hakuna mambo kama drama, kisirani ama kumchukia mtu. Mungu ni upendo, yeye ndie aliyeweka uhai kwa mtoto tumboni mwa mwanamke. Iweje leo mwanamke unamfanyia drama mtoto wa mwanamke mwenzako tena kwa maneno ya ghadhabu, kiburi, hasira, matusi yote in the name of pregnancy?..I do beg to differ. Lakini mwanamke huyo huyo akizaa mtoto wa kiume nae akaja akaoa, na mka mwana wake akawa hivyo atasema ananitesea mwanangu, anajifanyisha! Kuna vitu tunaviona ni sawa sana katika uso wa dunia ya leo lakin ni upotevu na ubatili.

Kuna cases za chakula ambazo hata mimi nazielewa kwamba mtu anashindwa kula chakula fulani hiyo sawa. Lakini sio ndo saa tisa kumtafutisha mume wako ubuyu ulioko kwenye gunzi lake. Atapata wapi labda? Mungu atusaidie na atupe hekima ya kuishi katika haya maisha.
 
Hili swali name nilitaka kuuliza ngoja nione alikujibuje boss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…