Wanaume wanaokataa ndoa wana matatizo yafuatayo...

Wanaume wanaokataa ndoa wana matatizo yafuatayo...

Mkuu unaona za kijinga kwa sababu umezeeka , kampeni ya kataa ndoa kuna watu apa wapo ndoani wanaona ni nzuri ya nn kufuga ng'ombe wakati unapata maziwa ? Kma ninaweza kuzaa na mke wa mtu kuna haja gan yakuoa ?
Na kwanini uzae na mke wa mtu..?
Huoni wewe ni sehemu ya kuharibu ndoa ya mwenzako?..
 
Na kwanini uzae na mke wa mtu..?
Huoni wewe ni sehemu ya kuharibu ndoa ya mwenzako?..
Mkuu maamuzi ya kushika mimba niya mwanamke , alafu kusema kuna mwanamke wa mtu itakuja kukuweka jela badae
 
Mkuu unaona za kijinga kwa sababu umezeeka , kampeni ya kataa ndoa kuna watu apa wapo ndoani wanaona ni nzuri ya nn kufuga ng'ombe wakati unapata maziwa ? Kma ninaweza kuzaa na mke wa mtu kuna haja gan yakuoa ?
Hakuna mahali mimi nilipo endesha kampeni ya #kataa ndoa.

Jambo la msingi tunalo paswa kufahamu ni kuwa ndoa sio jambo la lazima bali ni jambo la hiari mtu kutekeleza au laah.

Ndio maana kuna watu walio amua kuishi maisha ya kiseja iwe ni kwa sababu za kidini au sababu zao binafsi mmoja wapo mimi, jamii yetu ya kiafrika ina hitaji kubadili fikra na mitazamo yao juu ya hili kundi la watu ikiwemo huyu mleta mada maana kwa asilimia kubwa alio andika kuhusu hili kundi la watu hayana maana.

Ndoa haipaswi kuwa kasumba kwa watu kutekeleza bali inapaswa kuwa hitaji la hiari tu.

Jamii inapaswa kubadili mitazamo yao hasi ya awali na kuzalisha fikra mpya kuhusu swala la ndoa na mahusiano ya kimapenzi maana haya ni maswala ya hiari binafsi ya mtu na wala sio matakwa ya lazima kutekeleza.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Nyakati hizi ukitaka kuishi na mwanamke kwenye ndoa ni lazima ujifanye zoba, ujitie upofu, ujitie kiziwi ndio unaweza kuishi na mwanamke wa nyakati hizi.....lakini ukiishi kama mume ndani ya nyumba hauwezi kudumu naye........

Ndoa ni jambo la msingi kwenye maisha lakini changamoto na varangati yanayotendeka kwenye ndoa yanawaacha vijana dilemma kuamua.......

Nimeshuhudia vijana wengi waliokuwa wamestawi kimaisha lakini wamekuja kuporomoshwa na wake zao..... wengine tumewazika kwa kushindwa kuhimili machungu......

Wapo wanaoishi kwenye ndoa ilimradi lakini kimsingi nafsi zao zimeshakufa na wanatembea kama wafu.........

Zamani nilikuwa nahamasisha vijana wengi Suala la kuoa lakini Siku hizi kijana akinifuata kuniomba ushauri namkwepa sana.....maana kwa namna moja au nyingine nimewaingiza vijana wengi kwenye matatizo nikiwahamasisha waoe.....

Hakuna kijana rijali asiyependa kuoa....,isipokuwa yanayoshuhudiwa mitaani kuhusu wanandoa yanatisha na kutia kinyaa kabisa.......

Hakuna kijana rijali asiyependa kuoa....,isipokuwa yanayoshuhudiwa mitaani kuhusu wanandoa yanatisha na kutia kinyaa kabisa.....

Na hi ndio sababu mkuu
Wanadhani hatutaki kuowa
Kuowa ni jambo jema
Kuowa ni baraka kwa mungu na familia
Kwa imani yangu kelphin nnaamini hivi
“Mtu anapoowa hata njia za kipato hufunguka zaidi kadri na anavyotafuta”

Lakini shida ni!
Wanawake wamekua wakichukulia vitu rahisi
Utandawazi unavyozidi kuendelea kwenye technology ndivyo vilevile kwenye mahusiano ya mapenzi
Hakuna uvulilivu
Heshima na ustahimilivu
Kila kitu cha ajabu kimekua CHAKAWAIDA
Wake za watu wanapigwa pumbu peupe kabisa.
Na hawastuki na wala hakuna tabu
Then unanitaka niowe ili?

Lucky dube alisema”ukitaka kumbadilisha mtu usimnunulie nguo wala viatu wala chochote, bali mbadilishe mtazamo wake”

Mtazamo haukui from no where
Mtazamo unwjiunda kutokana na unachokiona

Sasa kwa haya tuyaonayo je hizo ndoa tuzipapalikie ili?
Kama nlivyowahi kusema hapo nyuma ya kua
Hakuna mwanaume kamili anaekimbia majukumu

Lakini utakua na uhakika gani kama majukumu ni yako!??
 
Umekazania kuuana.Hawajaambiwa wakioana wapigane au kuuana.Huo ni ujinga wao.Ndoa ni taasisi ya kufurahia maisha.
Wewe umesema matatizo hayapaswi kukimbiwa, rudia ulicho andika awali.

Na kupiga nusu kuua ni miongoni mwa matatizo mengi yanayo jitokeza mara kwa mara ndani ya ndoa nyingi, kwa nini una likwepa hili tatizo ?
 
Hakuna mwanaume ambaye amewahi kumuua mkewe au mpenzi wake kwasababu ya MALI,wengi ni usaliti,watu wengi hawataki kuoa kwasababu kuoa inakua ni nadharia tu,ila huyo unayemuoa anakua mgawaji wa nyapu nje,kama kawa,kuna haja gani ya kumuoa?
Wazee zamani walikua wanaoa,sababu moja wapo ni ukosekanaji wa wadada wanaogawa nyapu hovyohovyo,tofauti nasasa.
Unadhani sisi tunawakomalia waoe mkuu? Walaaa. Tunapingana na sababu zao eti wanahofia wanawake wanaolewa kwa tamaa. Eti wakiachana watagawana mali. Sasa wewe kama baba wa binti niambie hiki
Kitu, je, unamlea mtoto wako aje kuwa tegemezi kwa mwanaume?

Basi the sad part of this ni kwamba baadhi ya wanaume humu jf wana dhana kwamba tunaolewa kwa sababu ya mali zao ambazo wazazi wetu walitusomesha tukazitafute at the same time hawataki wanawake wafanya kazi wanasema ni feminists. Kuna mkanganyiko humu Mkuu usione tunapopoana. Mambo ni mengi😅

Endelea kupekua thread utakutana na hii kauli, “ huyu ataolewa na nani hivi alivyo mjeuri” yaani they think we are desperate for marriage. Of which it’s not true.

Nyinyi kama wazazi/walezi na wakubwa pia waelekezeni vijana kwamba kuna wanawake watafutaji tena sana ndo maana kizazi cha marioo kimeongezeka miaka hii mwanaume anakunja nne mwanamke anatafuta kwa jasho. Ni hayo tu
 
Hakuna mwanaume ambaye amewahi kumuua mkewe au mpenzi wake kwasababu ya MALI,wengi ni usaliti,watu wengi hawataki kuoa kwasababu kuoa inakua ni nadharia tu,ila huyo unayemuoa anakua mgawaji wa nyapu nje,kama kawa,kuna haja gani ya kumuoa?
Wazee zamani walikua wanaoa,sababu moja wapo ni ukosekanaji wa wadada wanaogawa nyapu hovyohovyo,tofauti nasasa.
Eti HAKUNA. Rudia kusoma kwa sauti. Kama vitu hujui uwe unanyamaza. Wanaume wangapi wameua wake zao kwa sababu ya mali?

Unavyosema wazee wa zamani, kakae nao saizi uskie hadithi zao. Wengi walibambikiziwa watoto. Na kusema eti ukioa mtu atakua anagawa nyapu nje. Msiwe mnaleta mifano ya wanawake mliokuzwa nao mnapigia hesabu ndo wanawake wote.
 
Mkuu maamuzi ya kushika mimba niya mwanamke , alafu kusema kuna mwanamke wa mtu itakuja kukuweka jela badae
Kama maamuzi ni ya "kwake"..si pekee..na ndio maana Sheria zinakubana uhudumie..(child support)
 
Hakuna mahali mimi nilipo endesha kampeni ya #kataa ndoa.

Jambo la msingi tunalo paswa kufahamu ni kuwa ndoa sio jambo la lazima bali ni jambo la hiari mtu kutekeleza au laah.

Ndio maana kuna watu walio amua kuishi maisha ya kiseja iwe ni kwa sababu za kidini au sababu zao binafsi mmoja wapo mimi, jamii yetu ya kiafrika ina hitaji kubadili fikra na mitazamo yao juu ya hili kundi la watu ikiwemo huyu mleta mada maana kwa asilimia kubwa alio andika kuhusu hili kundi la watu hayana maana.

Ndoa haipaswi kuwa kasumba kwa watu kutekeleza bali inapaswa kuwa hitaji la hiari tu.

Jamii inapaswa kubadili mitazamo yao hasi ya awali na kuzalisha fikra mpya kuhusu swala la ndoa na mahusiano ya kimapenzi maana haya ni maswala ya hiari binafsi ya mtu na wala sio matakwa ya lazima kutekeleza.
Ni kweli mkuu
 
Asili ya nafsi ni yenye kupenda maovu na starehe, ndio mana wazee wa zaman hata kabla ya dini walikua strict sana na suala la zinaa.
Mnachofanya mnaokataa ndoa ni kuipamba zanaa ambayo ina athali nyingi sana kwa jamii
Wanaoongoza kwa zinaa ni Hao walioko ndoani. Tena Wana viapo kabisa.
 
Mkikataa kuoa msitembee na mabinti za,watu na kuwapa mimba na kuwaacha huku wana expect ndoa...nyie ndo wa kwanza kuwaponda singo maza humu
Na nyie mliooa na kuolewa tulieni ndoani sio kila siku manafumaniana na kuuana juzi tu hapa jamaa kachoma visu mkewe kisa kamfumania. Nyie ndio mnaongoza kusalitiana
 
Back
Top Bottom