Wanaume wengi hufa kabla ya wakati wao kwa sababu ya laana kutoka kwa wazazi

Zipo sababu pia za kimazingira na kazi za hatari. Kwa mfano madereva na makondakta na hata wasafiri wengi wa kibiashara ni wanaume. So ajali nyingi za magari tegemea wanaume wengi kufa zaidi.
 
Zipo sababu pia za kimazingira na kazi za hatari. Kwa mfano madereva na makondakta na hata wasafiri wengi wa kibiashara ni wanaume. So ajali nyingi za magari tegemea wanaume wengi kufa zaidi.
Ni Kweli ulichosema ndugu, sababu zipo nyingi,

Leo tunajadili LAANA ya wazazi kama sababu mojawapo muhimu ya vifo vya kabla ya muda Kwa wanaume wengi.
 
Kwani hii amri alipewa mwanaume pekee?
Walipewa watoto wote wa kike na kiume.

Leo tunawajadili wanaume zaidi maana wanawake Kwa kuwatunza na kujali wazazi wao waliowazaa hawajambo!!

Karibu.🙏
 
Namwongelea Mwanaume anayehangaisha KICHWA usiku na mchana kutafuta riziki ya familia na hapumziki, nini kinachomwondoa mapema?

Namwongelea Mwanaume anayevuja JASHO, anamhudumia mkewe na hawara na machangudoa na anamudu wote kuwapa mahitaji yao, kwanini anawahi kuchomoka duniani mapema?

Haya ndio majibu yako.
Kila Jambo kwa kiasi!
Mafanikio yanasema pia, 'mwanaume atamuacha Baba na Mama yake na kuambatana na mkewe'.

Ilitakuwa wazazi wawe wamejipanga tangu ujana wao na wasiwe tegenezi kwa watoto. Kuna hulka ya mtu kuzaa ili hapo baada apate wa kumtunza, ibadilike.
Mwanao atafariki, lawama mtamtupia mkewe', wakati wazazi mlibweteka na yeye kuelemewa.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Wazazi walijinyima kujenga nknk Ili usome shule, waliuza mashamba Ili upate matibabu hospitali sababu hawakuwa na bima!!

Stuka, mke unaemtunza Kwa Kila kitu, Huwa anakata kiasi na kuwatumia wazazi wake.

Uzuri malipo ni hapa hapa, watoto utakaowazaa na kuwatunza watakulipia.

Tusubiri.
 
Sababu kubwa ya wanaume wengi kufa mapema ni kwa sababu ya kutumika kupita kiasi, mwanaume anatakiwa ahangaike kuilisha familia iridhike, bado miongoni mwao, yupo mmoja nae akisha kula akashiba anatakiwa arishishww tena kwa namna yake ya kipekee, haya yote yanachangia kuidhoofisha afya ya mwanaume, inakuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa na hatimaye kifo kumuondoa mapema duniani.

Mbaya zaidi, utakuta mwanaume huyo huyo, bado ana wanawake wengine mitaani, wakati yeye akidhani ni starehe, kumbe kimsingi anajichimbia zaidi kaburi litakalowahi kumuondoa haraka duniani, kwani hizo nyumba ndogo nazo huitaji matunzo na kuridhishwa kibaiolojia na mwanaume yule yule mwenye mke na watoto nyumbani.

Hapa hakuna suala la laana ya wazazi, laan pekee kama ipo inayomwangamiza mwanaume ni lile andiko linalosema tunaangamia kwa kukosa maarifa, na hili linakwenda sambamba na adhabu tuliyopewa baada ya Adam kutenda ile dhambi bustani ya Eden, tutakula kwa jasho, ambayo hii ndio laana yenyewe, wala sio laana ya wazazi.
 
Umenena vyema ndugu,

Leo tunajadili mchango wa LAANA ya wazazi kama chanzo mojawapo Cha wanaume kufa before time, yaani wazazi wanateseka na kumhuzunikia mtoto Kwa kutowajali jambo linalopeleka LAANA then kifo.

Unaliongeleaje hili?
 
Logic,, kuishi miaka mingi siyo ishu, ishu ni kwamba kuishi huko Kuna heri na baraka!?
 
Bado hujaeleka au unataka kuleta taflani ili unitoe nje ya swali/reply yangu.

Sijasema wala kuandika popote kuacha wazazi wako na kuambatana na mkeo ni go and never come back, hiyo ni yako.


Narudia, soma hapo uelewe alafu njoo tufanye mjadala, usipanic kama ulivyonijibu hapo kijana 😄!.
 
HOJA tayari IPO mezani,nimesoma na kuandika maandiko uloquote,

Mchango wako tafadhali🙏

Pia mm Si kijana kama unavyodhani!!
 
Umeandika kitu Cha maana Sana.kuwasaidia wazazi ni jambo jema Sana.
Lakin Mimi Nina mtazamo tofauti na wewe. Tumerithi mfumo wa maisha ambao ni mbaya Sana. Kwamba kujengea wazazi na kuwasaidia ni jambo la lazima. Lakin tujiulize wazazi wetu walitumia vipi ujana wao katika maisha. Na walipitia ujana kama wewe Leo unavyoupitia. Ujana wako umeufanyia Nini?

Watu wengi hutumia ujana wao vibaya Sana bila kuwekeza chochote wakisubiri watoto waje wawasaidie huku wakati mwingine hawawapi sapoti yoyote ile. Ila lawama zinakuwa nyingi sana Kwa watoto wao.

Je watu wengi hutumiaje ujana wao. Kama watu tutatumia ujana wetu vizur hizi lawama kamwe mzazi hawezi malaumu Mtoto. Lakn kama ulitumia ujana wako vibaya utawalaumu watoto tu
 
Wazazi wengi Kwa Upendo walionao, hujinyima mambo Yao Kwa ajili ya watoto wao.

Hupasi kuuliza ujana wa wa wazazi waliutumiaje!!

Huo ni utovu wa nidhamu,

Timiza WAJIBU wako kama mtoto.
 
Na hili la kufa mapema Kwa wanaumme. Linaweza likawa kweli.

Ila sababu kubwa ni mfumo wa maisha unaopelekea tabia hatarishi za utafutaji Hela
hasa Kwa nchi zetu maskin. Tabia hatarishi kama vile.
Utumiaji wa madawa ya kulevya.
Pombe.
Umalaya
Uhalifu
Utafutaji wa pesa. Ajali nyingi huuwa Wanaumme. Kama vile uvuvi.uwindaji. migodi. Kilimo na zingine zingi zinachangia vifo Kwa wingi..
 
Katika siku umeandika pemba,basi ni katika hili andiko-mbona Wanaume wanaoishi katika Nchi za vipato vya juu umri wao wa kufa ni sawa na Wanawake.
Kinacho waua wanaume wengi katika Nchi za viator vya chini ni msongo wa mawazo pamoja na ulaji mbovu plus huduma mbovu za afya.

Urefu wa maisha ya mtu kuishi duniani hauthibitiki kiimani,bali ni sayansi.siku Ingine usilete mambo yako ya imani za kufirika na kuandikia kama fact.
 
Kutwa kutusimanga ...ingali wamezaliwa na mwanamke huyohuyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…