Wanaume wengi siku hizi wakiombwa msaada wa kipesa na wadada, wanahisi wanatapeliwa

Hello wanajf

Wanaume wengi siku hizi nimegundua tumekua wagumu wa kuweka effort kwenye mahusiano, hasa yakiwa mapya, namaanisha effort ya attention, pesa na juhudi, wanaume zamani tulikua tuko tayari kumsuburia mdada njiani masaa 3 huku tukiumwa na mbu na kumfukuzia miezi 8 hata miaka,, ili tu tupate nafasi ya kuongea naye, yakobo alifanya kazi miaka 14 kwa labani ili apate nafasi na alipie mahari ya kumuoa Rachel , ila siku hizi naona wanaume wengi tunawekeza effort ambayo ni ndogo sana kwenye mahusiano.

Mdada akiomba msaada wa kipesa, let's say ni kweli amekwama kipesa kama binadamu mwingine yeyote ambavyo angeweza kukwama, kwa wanaume wengi hata akitoa hiyo pesa atawaza mmh hapa natapeliwa.

Najiuliza sasa inakuaje unampenda mdada alafu akikuomba msaada, uhisi kwamba anataka kukupiga, wakati kama mtu umempenda, inatakiwa usiwe tayari kumwona mtu umpendae anapata shida yoyote, unakua unaamua kujitoa uwezavyo ili uweze mtoa kwenye hio shida.

Tangu lini kuombwa msaada wa kipesa na mdada, mara nyingi inaonekana na baadhi ya wanaume kuwa huo ni utapeli na fimbo ya kutupiga, na baadhi wanawake wanaona ni fimbo ya kupigia wanaume, wakati sometimes huenda ni kweli mtu anahitaji msaada huo, dunia sijui imekuaje.

Ref: ya screenshots toka kwa baadhi wanajf wa humu
View attachment 3227102
View attachment 3227103

Nimekumbuka maneno ya the late Kevin Samuels alisema kwenye dating world, winter is coming
Achani tutoe hela kwa upendo wetu na siyo kwa mapenzi yetu. kutoa hela kwa mapenzi yetu ni utakatishaji pesa uliojificha kwenye ngono!!. Kwa mademu kuombaomba hela nawaungamkono KATAA NGONO /NDOA.
 
Hello wanajf

Wanaume wengi siku hizi nimegundua tumekua wagumu wa kuweka effort kwenye mahusiano, hasa yakiwa mapya, namaanisha effort ya attention, pesa na juhudi, wanaume zamani tulikua tuko tayari kumsuburia mdada njiani masaa 3 huku tukiumwa na mbu na kumfukuzia miezi 8 hata miaka,, ili tu tupate nafasi ya kuongea naye, yakobo alifanya kazi miaka 14 kwa labani ili apate nafasi na alipie mahari ya kumuoa Rachel , ila siku hizi naona wanaume wengi tunawekeza effort ambayo ni ndogo sana kwenye mahusiano.

Mdada akiomba msaada wa kipesa, let's say ni kweli amekwama kipesa kama binadamu mwingine yeyote ambavyo angeweza kukwama, kwa wanaume wengi hata akitoa hiyo pesa atawaza mmh hapa natapeliwa.

Najiuliza sasa inakuaje unampenda mdada alafu akikuomba msaada, uhisi kwamba anataka kukupiga, wakati kama mtu umempenda, inatakiwa usiwe tayari kumwona mtu umpendae anapata shida yoyote, unakua unaamua kujitoa uwezavyo ili uweze mtoa kwenye hio shida.

Tangu lini kuombwa msaada wa kipesa na mdada, mara nyingi inaonekana na baadhi ya wanaume kuwa huo ni utapeli na fimbo ya kutupiga, na baadhi wanawake wanaona ni fimbo ya kupigia wanaume, wakati sometimes huenda ni kweli mtu anahitaji msaada huo, dunia sijui imekuaje.

Ref: ya screenshots toka kwa baadhi wanajf wa humu
View attachment 3227102
View attachment 3227103

Nimekumbuka maneno ya the late Kevin Samuels alisema kwenye dating world, winter is coming
Kinachofanya Dunia inakuwa vile ambavyo hujui, ni mfululizo wa utapeli mwingi unaofanywa na wanawake. Fatilia nyuzi nyingi humu za kuchapiwa, utakuta ishu ni hizo, mwanamke alikuwa anahudumiwa vizuri na boy wake, jamaa anajituma kumtunza demu wake kwasababu anampenda, kumbe demu anamcheat.

Kuna wengine wamepigwa chini kabisa. Sasa matukio haya yameteketeza kabisa, Imani ya wanaume Kwa wanawake, utandawazi umewachukua sana Hawa viumbe, Najiuliza unaishi Dunia gani mkuu maana haya Mambo ni ya kawaida sana siku hizi. Jamaa anamhudumia demu wake yupo chuo, jamaa ana madeni kwasababu ya kukopa pesa kumsaidia demu wake halaf siku anampigia simu demu wake saa saba za usiku anapokea mshkaji. Ni Bora Kama asinge mpigia.

You have a lot to learn brother, usije ukawalaumu wanaume, kwasababu hata MUNGU alitetea maumivu ya ayubu kwasababu ya udhaifu wa asili wa kibinadamu.
 
Hehe ukija huku uswazi kwetu kuna wale hawaachagi kitu,,ukichovya tu kwenye kidude chake basi unaingia kwenye list ...siku akiamua anacheki ile list yake anakusanya sadaka kote, kuna wale wa kuombwa buku kuna wa 10, hawaachagi kitu na wanawapenda sana bodaboda akikusanya buku zao ndani ya siku kwenye ile list yake anatoka na ka hela ka maana......hamna mahusiano siku hizi ukijichanganya unageuzwa USAID
 
Vipi kama na yeye anakupima kama utampa
Atujaanza leo mwanzo nilikuwa nampa but kwasasa nilipata fulani ya pesa na nikamwambia na anafaham lakini bado ajali ananiambia anashida na 60k na awez subili nimalize madeni so niangalie namna ya kumsaidia kwa vyovyote
 
Huyo pure gold digger itkuwa anadaiwa vikoba
Aamke afanye kazi hela za kuomba omba hazitoshi
 
Sasa tupo kwenye 50/50.. kwanini mwingine awe na shida tuu, na mwingine awe anatatua shida za mwingine?

Kila mtu ashinde match zane.

Mwanamke akiomba, azima au.akitaka hela; hairudi... Kuliko kupoteza heri uamue umpe tu au usimpe kabisa.
Kwenye suala la hela wenzetu iyo 50/50 hawataki hata kuisikia. Elimu, ajira, uhuru, kurithi mali, uongozi n.k uko kote 50/50 na ukowaunga mkono watakuita gentleman.

Ila sasa ongelea 50/50 hapo kwenye kutoa hela au kulipa bill, wanaamisha goli
 
Wake zenu wakiwaomba hela mnakataa?? Zingatia (mke)
Mwanaume anaejielewa, atampa mkewe hela ya ziada, zawadi na ku-clear bills za basic needs ya familia yake k.v chakula, makazi, malazi, elimu, kulingana na uwezo wa kipesa alio nao na kuhakikisha anakua baba bora kwa watoto wake na mume bora kwa mkewe, biblia imeagiza tuwapende wake zetu, hivyo kuwapa wake zetu hela ni moja ya ishara ya kuwaonesha upendo

Ingawa kwa bahati mbaya sahivi wanawake wengi wanaingia kwenye ndoa kwa nia ya kupewa pesa na mume, ila kiuhalisia hawampendi huyo mume nakwede97
 
Kumbe wengine wanaingia kwenye ndoa Kwa kutaka kupewa hela doooh hii kali ya mwaka
 
Back
Top Bottom