Wanaume wengi "smart" wenye hela, hawajiamini kwenye mahusiano

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Hello,

Nina washkaji zangu ambao kwa level za kibongo bongo kwenye swala la pesa unaweza sema wametoboa kiasi, wanaendesha magari mazuri, wana biashara kubwa kiasi, wana umri mdogo, siku moja tulikaa mahali, mwamba alitumiwa sms na mpenzi wake, mdada alituma sms ya kuomba kuzaa na mmoja wa washkaji zangu, huyo jamaa mbele yetu akacheka na kutuambia kwa sauti huku akituonesha sms, huyu mdada anachotaka ni matunzo.. kwa vile anahisi nina hela nyingi.

Kuna video moja Diamond alijirekodi juzi akiwa kwenye mavazi ya kimaskini, akawachana wadada wanaojifanya kumpenda, akawauliza wangemkuta kwenye hali ile wangempenda?? Diamond Akaongeza kuwa sura lake libaya lakini anaitwa handsome boy.

Harmonize amechorwa tattoo na mdada, lakini harmonize akasema sahivi hamwamini mdada yoyote.

Imefika mahali wanaume tumejidharau kiasi hicho? Kwamba unajiona wewe ni mbaya kiasi cha kwamba usipokuwa na hela hamna mdada hata mmoja atavutiwa na wewe Physically kama ulivyo? Ukiwa na hela Kila mdada akikuonesha Love interest unahisi ni mdangaji/ golddigger/ amekuja kwako kukuchuna hela/ akufilisi akupige kitu kizito hlf asepe, vipi kama unapoteza wife material bila kujua?
 
Uongo mtupu.
 
Kuna mmoja aliniambia kama utani anataka kuzaa na mimi tu, apate mtoto mwenye akili kama zangu, hahitaji matunzo wala nini.

Nikafikiri utani, nikamjibu kiutani kwamba aandike mkataba wa kisheria kabisa ili mbele tusigeukane.

Nikajua hawezi kuandika mkataba.

Siku chache baadaye akarudi na mkataba mrefu, akanitumia na kuniambia mkataba wangu huu, ila wewe una ruhusa ya kuubadilisha unavyotaka!
 
Vipi ulimpatia anachotaka au
 
Ni pisi kali? Sema ukweli hapa usiongopeee
 
Ni pisi kali ? Sema ukweli hapa usiongopeee
Ni zaidi ya pisi kali mkuu imekaa kati kwa kati mguu mguu, mpaja mpaja, aki smile kama jua limechomoza. Upstairs yko vizuri unaweza kuongea naye mkaelewana. Uafrika fulani anao, umagharibi fulani anao. Ana kike Wafaransa wanakiita "savoir faire".

Ila it wasn't to be tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…