Wanaume wenye watoto tupeni uzoefu wenu. Mara ya kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua, hiyo siku ilikuwaje?

Ulijitahidi mkuu. Nishawai kuona scenario kama hii mume anashindwa kudrive
 
You are a good man
 
Ni kipindi ambacho inabidi uandae walau laki 1 iwe rushwa ya manesi na madaktari kumsimamia na kumhudumia vizuri mkeo.

Kama huna gari hakikisha una namba ya dereva taxi wa uhakika anaepatikana usiku.
Punguza ukali wa maneno sema motisha[emoji16]
 
Mkuu ninyi ni watu wema sana. Hongereni
 
Ni mfupi kidogo?
 
Wanaume ambao mnawatoto embu tupeni uzoefu wenu kwa mara kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua,hiyo siku ilikuwaje na kipi utoweza kusahau kabisa
Bochi iyo 2022 baada ya kusubiri kama nusu saa operation ikiendelea huko Thearte...Anakuja Nesi Mzee Kimamingo Njoo naenda namuona kwa mara ya kwanza Binti yangu akirusha rusha mikono na miguu Raha ilioje.
 
Dah mleta mada unanikumbusha mbali sana, nakumbuka iyo siku ilikuwa mida ya sa tano usiku nafika hospitali pale kimara eh bhana we daktar ananiambia ngoma ngumu tukapewa transfa mpk mwananyamala iyo ngoma sa saba kasoro tumefika pale asubui kukakucha lakini ngoma ngumu bado kipenzi changu au mama watoto wangu hali yake ilikuwa mbaya kwa sababu mfuko wa uzaz ulikuwa umepasuka tangu ile siku tumeanzia pale kimara aisee mwananyamala pale tulikaa siku mbili hivi basi ikabidi wife apewe transfa kwenda muhimbili tumefika kule maumivu yaliyochanganyika na jasho la damu yalikuwa yanamwandama mke wangu usiku kucha uchungu ulimshika sana basi alfajili ilibidi apigwe kisu basi mungu akatujalia tukapata babe girl wetu ila nina mengi ya kuongea ipo siku nitashusha uzi kuelezea mazito yaliyotukuta.
 
Nilijikuta naambatana nae labour bila ya kujua, Nesi akaniwahi nikafukuzwa! sikurudi nyumbani nilisalia maeneo hayohayo ya hospital hadi mapambazuko! nikapata Dume langu la kwanza! Nashukuru sasa nna madume 5 na jike1! Alhamdulillah.
 
Mm sipendi kuona mshono wa mwanamke na hospital nying huwa zinalazimisha kujifungua Kwa operation so Ili kuepukana na kujifungua Kwa operation niliandaa wekundu wengi mfuko wa shati

Nachokumbuka ni kwamba yule mdudu alihudumiwa kama mfalme
 
Kuna mtu aliniambia uzazi wa mtoto wa kike ni wa mateso kuanzia mimba mpaka kuzaa naanza kumuelewa sasa baada ya kusoma hii mada changamoto nyingi unakuta mwishoni inamaliziwa na mtoto wa kike, nasikia hata uchungu wake unauma sana
 
Hahahaha,eti nesi alikuwa anatikisa kichwa,hiyo mbaya sana unaweza ukazimia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…