Wanaume wenye watoto tupeni uzoefu wenu. Mara ya kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua, hiyo siku ilikuwaje?

Wanaume wenye watoto tupeni uzoefu wenu. Mara ya kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua, hiyo siku ilikuwaje?

Picha limeanza saa tisa usiku,,baby mama uchungu umempata na kumbuka baby mama wangu hujifungua kwa operesheni

So mwelekeo ni muhimbili na ndio mtoto wangu wa kwanza,nipo makazi africana mbezi,,mungu mkubwa nje kuna nissan march kadogo kadogo hivi ndio nikakapiga start hao muhimbili,,yaan baby mama anaugulia maumivu mwamba namtaja Allah kwa sana na kumtukuza atufikishe salama

Dah ilikuwa experience ya kipekee sana
Ulijitahidi mkuu. Nishawai kuona scenario kama hii mume anashindwa kudrive
 
Uzazi wa pili Kipindi kile corona imepamba moto 2020 ingawa ilikua vyepesi sana lakini kidogo akili iliyumba.

Uzazi wa kwanza ndio sita sahau!
Kwanza kabisa hospitali ya jirani walisema uzazi wa kwanza lazima mwananyamala ama sinza.
Nikaomba sinza tukaelekezwa maana tulikuwa wa geni dar, hatuna mwenyeji hata mmoja.
tukaenda, kipimo tukaambiwa kurudi tarehe fulani, siku hio tulivyorudi nikaambia anabaki nirudi nikaandae chakula na vinginevyo, bahati nzuri tulipewa abc za kujifungua so vifaa alikuwa navyo.
Siku ya kwaza ikakata, siku ya pilli nayo ikakata!
Nikashauriwa na daktari kwamba njia imekataa kufunguka inatakiwa dawa fulani kama kumbukumbu ziko vizuri ni dinoproston, bei 50,000 kidonge kimoja! Nilizunguka mji wa dar es laam karibu kila famasia hio dawa hamna, siku inayofuata nikarudi pale namwambia ness nimekosa akanijibu ongea na watu vizuri dawa ipo hapa hapa lete hela nikuchulie!
Nusu saa nyingi dawa ikapatikana!
Akapewa dawa hata haikusaidia, siku ya nne ikaisha , siku ya tano asubuhi na fika pale mtu wa kwanza naulizia mapokezi pale nikaambiwa bado, mwanamke alishuka gorofani maana sehemu ya kujifungulia pale sinza ipo juu, ile tunakutana alikua ana lia! Nilijikaza kiume ingawa machozi yalikua yananilenga mno! Tulivyo achana nisiseme uongo nilitoka nje nikalia kwa kweli! Akaja mama mmoja simjui ila alisha nisoma, akanipeleka kwenye mgahawa akanunua chai akanipa, akaniambia wewe ni mwanaume kuwa mwanaume!

Nikarudi nyumbani kuandaa chakula jioni nikaenda tena hali ni ile ile.

Mungu ni mwema asubuhi siku ya sita saa 12 asubuhi nafika pale nikajitambulisha nikaambiwa panda juu, kufika naonyeshwa mtoto mama bado hakaa sawa katika operation dakika kumi zilizopita, nilishukuru aisee mtoto wa kiume uzito kg 4.2.
You are a good man
 
Ni kipindi ambacho inabidi uandae walau laki 1 iwe rushwa ya manesi na madaktari kumsimamia na kumhudumia vizuri mkeo.

Kama huna gari hakikisha una namba ya dereva taxi wa uhakika anaepatikana usiku.
Punguza ukali wa maneno sema motisha[emoji16]
 
Ya kwangu mimi ilikuwa experience ya kujifunza mambo mengi, ambayo mwanaume ambae hajaoa au kubahatika kupata mtoto hawezi kuyajua.

Kwanza, mimba zote za mke wangu ni zile ziitwazo risky pregnancy.YMimba ya mtoto wa pili ikibidi washone ile cervix ili kuzuia mimba isitoke. Nikapigwa marufuku kufanya chochote kinachohusisha sehemu zake za siri. Hii ilikuwa torture ya hali ya juu.. Ilihitaji nidhamu ya hali ya juu kutulia nyumbani.
Halafu tukaambiwa na daktari wake kwamba mtoto anaweza kuzaliwa mapema (premature birth) kutokana matatizo ya wife. Kichwani, binafsi huwa nahisi wife, kabla yangu, alikuwa chinjachinja sana, yaani aliabort mimba nyingi mdio maana kizazi kikatepeta) ingawa Sina uhakika na hilo.

Siku ya kwenda kujifungua ndio ikaleta mauzauza ya hali ya juu. Tulikaa hospital zaidi ya masaa 48. Njia ya kutokea ikagoma kufunguka au ikaanza kufunguka kidogokidogo. Kwa hiyo, kila baada ya masaa kadha daktari anakuja, anaingiza mkono au vidole ili kuona kama kuna maendeleo yoyote.

Kasheshe ilikuja jioni yake baada yaa shift mpya kuanza. Daktari kaingia kwenye chumba alipo mke wangu na kundi la wanafunzi.
Hiyo hospital ipo (attached na Medical School. Doctor akatufahamisha kwamba mimba kama hii ya mke wangu haziji mara kwa mara, hivyo basi akaomba ruhusa ili wale ma Medical interns wajifunze mambo ya risky pregnancy kupitia mke wangu. Nikamuuliza bibie kama yupo ok, akasema hamna tabu.

Mhhhh! Yaani, kila moja wao anavaa glove anazamisha mkono. Moja baada ya mwingine. It was the most eye opening experience kwa kweli. 15 hours later tukafanyikiwq kupata mtoto wa kike. Maisha ni safari ndefu sana. Pia, kushi kwingi huona mengi.
Mkuu ninyi ni watu wema sana. Hongereni
 
Kuna mijadala kama hiyo mitaani hasa hawa shombe shombe lkn huenda hakuna ukweli wowote

Na hata hao ambao wanafanya michezo hiyo nasikia wanahospital zao maalum ambazo wanafichiana aibu zao huko

Anyways lililokubwa zaidi wengine nyonga zao hazifunguki hivyo kushindwa kuzaa kwa kawaida,mfano mama watoto wangu mimba ya kwanza ilikuwa operation,,ya pili walimchelewesha kidogo kuona kama atazaa kwa njia ya kawaida lkn ikashindikana so wakaamua kumpiga kisu,kwahiyo watoto wote watatu ni kwa operationi,,ishu ni kimaumbile zaidi na si habar za mtaani
Ni mfupi kidogo?
 
Wanaume ambao mnawatoto embu tupeni uzoefu wenu kwa mara kwanza unampelekea Mwanamke wako hospitali kujifungua,hiyo siku ilikuwaje na kipi utoweza kusahau kabisa
Bochi iyo 2022 baada ya kusubiri kama nusu saa operation ikiendelea huko Thearte...Anakuja Nesi Mzee Kimamingo Njoo naenda namuona kwa mara ya kwanza Binti yangu akirusha rusha mikono na miguu Raha ilioje.
 
Dah mleta mada unanikumbusha mbali sana, nakumbuka iyo siku ilikuwa mida ya sa tano usiku nafika hospitali pale kimara eh bhana we daktar ananiambia ngoma ngumu tukapewa transfa mpk mwananyamala iyo ngoma sa saba kasoro tumefika pale asubui kukakucha lakini ngoma ngumu bado kipenzi changu au mama watoto wangu hali yake ilikuwa mbaya kwa sababu mfuko wa uzaz ulikuwa umepasuka tangu ile siku tumeanzia pale kimara aisee mwananyamala pale tulikaa siku mbili hivi basi ikabidi wife apewe transfa kwenda muhimbili tumefika kule maumivu yaliyochanganyika na jasho la damu yalikuwa yanamwandama mke wangu usiku kucha uchungu ulimshika sana basi alfajili ilibidi apigwe kisu basi mungu akatujalia tukapata babe girl wetu ila nina mengi ya kuongea ipo siku nitashusha uzi kuelezea mazito yaliyotukuta.
 
Nilijikuta naambatana nae labour bila ya kujua, Nesi akaniwahi nikafukuzwa! sikurudi nyumbani nilisalia maeneo hayohayo ya hospital hadi mapambazuko! nikapata Dume langu la kwanza! Nashukuru sasa nna madume 5 na jike1! Alhamdulillah.
 
Mm sipendi kuona mshono wa mwanamke na hospital nying huwa zinalazimisha kujifungua Kwa operation so Ili kuepukana na kujifungua Kwa operation niliandaa wekundu wengi mfuko wa shati

Nachokumbuka ni kwamba yule mdudu alihudumiwa kama mfalme
 
Kuna mtu aliniambia uzazi wa mtoto wa kike ni wa mateso kuanzia mimba mpaka kuzaa naanza kumuelewa sasa baada ya kusoma hii mada changamoto nyingi unakuta mwishoni inamaliziwa na mtoto wa kike, nasikia hata uchungu wake unauma sana
 
Siku ambayo sitakaa niisahau ni Ile alirudi klinik akasema hajahudumiwa mimba yake mpaka aende na mwenzie,wakati huo ina miezi mitatu.
Kidume nikatupia vest raba na jinsi nkamwambia utanikuta nje.
Msala ni pale nlivyofika clinik eti naambiwa lazima nipimwe ngoma maana mtoto hatakiwa apate vvu.Kumbuka mm ni wale walioapa kutopima ngoma mpaka mwisho Dunia ila sasa yamenikuta.
Unaambiwa nilivuja jasho kinoma wakati yule nesi anapima.Yaani anagusa gusa specimens halafu anatikisa kichwa Kwa masikitiko ilimradi tu mbwembwe.
Siku Ile nilipungua kilo sana siwezi sahau.
Hahahaha,eti nesi alikuwa anatikisa kichwa,hiyo mbaya sana unaweza ukazimia
 
Back
Top Bottom