Wanawake ambao hatujajaliwa kuzaa licha ya kuwa na wanaume tukutane tufarijiane

Wanawake ambao hatujajaliwa kuzaa licha ya kuwa na wanaume tukutane tufarijiane

Pole sana Ndege Tausi nakuombea sana upate hitaji lako.Dada yangu pia anatatizo km lako anahangaika mpk Mimi nakosa amani. ALLAH awape faraja ktk mioyo yenu Insh-Allah
 
Kuna mwanake nilianzisha nae mahusiano baada ya muda akaniambia ni mjamzito binafsi nikaona ananichungulia.,...baadae niakapewa habari kua alishatumia kila mbinu lakini hakupata mtoto mpk Kwa waganga alienda lakini wapi....nachojiuliza iweje kua na Mimi Tu basi apate mimba....binafsi nimegoma kulubali kua hyo mimba ni yangu may be mpk mtoto atakapozaliwa kwani inatia ukakasi.
Mungu awape watoto wale wenye uhitaji nao Insha Allah.


Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa inatokea labda damu zenu zeendana.
Me nliwahi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja.nilidumu naye ndani ya mda mrefu mno.ila sikuwahi kupata mimba.mpaka nikawa najiuliza kulikoni.
Maana nakumbuka mwanaaume alikuwa anahitaji sex.mkiwa faragha tu.
Japo nlikuwa kwenye dangerous day.sikupata mimba.
Niliachana nae nikawa nawanaume mwingine haikupita hata miezi 3 nikapata ujauzito...
Na hapo nlikuwa makini kweli nisipate mimba ila nilipata.
Kwa hiyo Damu zikiendana tu mambo nakuwa fresh
 
Poleni sana wanawake wenzangu na MUNGU awajaalie mpate watoto
Najuaa mnavyojisikia...poleni sana
 
Kutoa mimba ni tatizo sana ipo siku mwanaume atakuchoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu usiende kwa kukariri maisha...sio kila asiezaa alitoa mimba na sio kila mwanamke anayelalamika hapati watoto ni yeye ndio mwenye shida ..ukweli ni kwamba wanaume wengi wenu sikuizi mbegu zenu hazina nguvu yakumpa mtu mimba na mbaya zaidi mnajidanganya kwasababu utakuta nje umebambikiwa watoto au mtoto asiye wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dada pole sana, umepambana sana toka enzi na enzi.

Vipi mumeo alikubali uasili japo mtoto mmoja?

Screenshot_20200210-110426.jpeg
Screenshot_20200210-110408.jpeg
Screenshot_20200210-110343.jpeg



Unforgetable
 
Mkuu usiende kwa kukariri maisha...sio kila asiezaa alitoa mimba na sio kila mwanamke anayelalamika hapati watoto ni yeye ndio mwenye shida ..ukweli ni kwamba wanaume wengi wenu sikuizi mbegu zenu hazina nguvu yakumpa mtu mimba na mbaya zaidi mnajidanganya kwasababu utakuta nje umebambikiwa watoto au mtoto asiye wako

Sent using Jamii Forums mobile app
sawa sawa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni swala la kujipa moyo tu. Ni kawaida kuhisi kama ungekuwa na kitu fulani maisha yangekamilika wakati si kweli. Hao wenye watoto nao wana mitihani yao. Wakati mwingine na mara nyingi watu wasio na vitu fulani huwa wanajinyanyapaa wenyewe na kutafsiri kuwa kila kitu kuwa wanasemwa wao. Mnaweza kuwa mmekaa akina mama watano, mmoja hana mtoto. Ikatokea mada ya watoto kila mmoja akaanza kuchangia kuhusu mtoto wake. Mnakuja kukumbuka kuna mwenzenu hana mtoto akiwa anaondoka bila kuaga au amekuwa mwekundu.

Wakati mnasubiri miujiza yenu chukueni watoto wachanga na wadogo wasio na wazazi huko vituoni muwalee. Wengine huku kukosa watoto kumewapa hali ya kuona thamani kubwa ya mtoto na kujikuta wanapenda kuona watoto wakifurahi, hivyo wamejitoa kuhudumia watoto kwa njia mbalimbali. Tafuta kusudi kwenye kila gumu unalopitia badala ya kulalamika na kulia miaka nenda miaka rudi.
 
Ni mhanga kwa zaidi ya miaka 20. Nimezunguka hospitali mbalimbali na kufanyiwa vipimo mbalimbali ila haijawahi kubainika chanzo cha tatizo. Nimeombewa sana makanisani na kunywa dawa za mitishamba nyingi tu ila bado sijafanikiwa.
Nimejaribu hata kupandikiziwa mbegu zaidi ya mara moja bado ikashindikana.

Kuna watu hapa wanaropoka tu bila kujua uchungu wala uzito wa kulibeba tatizo hili.
Wengine wanakimbilia kuhukumu kuwa ni madhara ya kutoa mimba pasipo kujua kuwa sio wote wenye matatizo haya tulitoa mimba.
Pole sana, MUNGU yupo hutoa kwa wakati wake tumwamini tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom