Wanawake ambao hatujajaliwa kuzaa licha ya kuwa na wanaume tukutane tufarijiane

Wanawake ambao hatujajaliwa kuzaa licha ya kuwa na wanaume tukutane tufarijiane

Mpenzi wangu ana hormonal imbalance ya viwango vya juu. Ana magonjwa chungu nzima na matatizo ya afya hayaishi. Nina wasiwasi nae kama atapata mtoto sijui kwa nini kuna roho inaniambia hivyo. Siwezi sema alitoa mimba au kutumia birth control kwa sababu matatizo yake ya muda mrefu kabla hatujaanza intercourse miezi minne iliyopita (her first time).
 
Kwahiyo mkuu na wewe ulishawahi kuchoropoa mimba
Mimi nishatumia njia zote za uzazi za mahospitali na nimeanza tokea na miaka 18 hukooo na Nina watoto zaidi ya 2 , natumia vijiti nawekaga vya miaka mitatu mitatu nikitoa tu haipiti mwezi mimba .na hapo sijakuhesabia mimba nilizopunch za ujana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mhanga kwa zaidi ya miaka 20. Nimezunguka hospitali mbalimbali na kufanyiwa vipimo mbalimbali ila haijawahi kubainika chanzo cha tatizo. Nimeombewa sana makanisani na kunywa dawa za mitishamba nyingi tu ila bado sijafanikiwa.
Nimejaribu hata kupandikiziwa mbegu zaidi ya mara moja bado ikashindikana.

Kuna watu hapa wanaropoka tu bila kujua uchungu wala uzito wa kulibeba tatizo hili.
Wengine wanakimbilia kuhukumu kuwa ni madhara ya kutoa mimba pasipo kujua kuwa sio wote wenye matatizo haya tulitoa mimba.
Pole Sana shida ya Jf Kuna vijana ambao bado wanahitaji muda wa kukua zaidi wajue changamoto za kidunia wakikua wataacha wasamehe bure tu.
 
Infertility is real.

Ila, kama kweli mungu yupo iweje, sasa aruhusu watu wengine, tena ambao si wawajibikaji, waweze kuzaa watoto wengi huku watu wengine, tena wenye kupenda sana watoto, wakihangaika kupata hata mtoto mmoja?

Kuna watu wanazaa watoto halafu wanawatupa majalalani mithili ya takataka.

Wengine wanazaa halafu hawawahudumii watoto wao. Wanawatelekeza.

Halafu unakuta mwingine anahangaika miaka nenda rudi akitafuta kupata mimba ili azae lakini wapi!

Kama mungu yupo kweli, kwa nini afanye hivyo?
 
Miaka 7 sasa, ila sijakata tamaa naamini iko siku Mungu atanipa, na pia nashukuru Mungu kwa mume nilienae manake bila upendo wake kwangu na kunitia moyo na kujitahidi kwa kila hali kunifanya nisijisikie kama kuna kitu kimepungua kwenye ndoa yetu, sijui ingekuaje manake sometimes huwa nasahau kama sina mtoto, pia mawifi na wakwe zangu aisee hawa watu Mungu aendelee kuwabariki ni wapekee sana, its like Mungu alijua ntapitia nini nikiolewa akaona anipeleke sehemu ambayo sitajutia
 
Nyani Ngabu,
Yupo kweli, na usiangalie nani anafanyai nini na nani afanyiwi, Mungu ni mwema kwa wema na wabaya ndo mana mvua hunyesha kwa kila mtu haichagui kwa mwema ndo inyeshe alafu kwa mwenye dhambi pawe pakame, hata jua ni la wote, ni kwa Neema tu
 
Pole sana dada
Watoto ni baraka kutoa kwa Mungu yeye ndio anajua wakati gani unastahili. Wapo wengi hata kwenye vitabu vyetu vya imani tunaona wanawake waliokosa watoto wakapata kwa wakati ambao hawakutegemea
Ni mhanga kwa zaidi ya miaka 20. Nimezunguka hospitali mbalimbali na kufanyiwa vipimo mbalimbali ila haijawahi kubainika chanzo cha tatizo. Nimeombewa sana makanisani na kunywa dawa za mitishamba nyingi tu ila bado sijafanikiwa.
Nimejaribu hata kupandikiziwa mbegu zaidi ya mara moja bado ikashindikana.

Kuna watu hapa wanaropoka tu bila kujua uchungu wala uzito wa kulibeba tatizo hili.
Wengine wanakimbilia kuhukumu kuwa ni madhara ya kutoa mimba pasipo kujua kuwa sio wote wenye matatizo haya tulitoa mimba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rafiki yangu alipata mtoto baada ya kudumu kwenye ndoa bila mtoto kwa miaka 14. Mume wake alikuwa upande wake na alimjali na kumtia moyo sana walikuwa ni wenye furaha kama vile hakuna walichopungukiwa Kinachotakiwa ni mume kuwa upande wako ili kuweza kupata faraja na kukuondolea stress.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mhanga kwa zaidi ya miaka 20. Nimezunguka hospitali mbalimbali na kufanyiwa vipimo mbalimbali ila haijawahi kubainika chanzo cha tatizo. Nimeombewa sana makanisani na kunywa dawa za mitishamba nyingi tu ila bado sijafanikiwa.
Nimejaribu hata kupandikiziwa mbegu zaidi ya mara moja bado ikashindikana.

Kuna watu hapa wanaropoka tu bila kujua uchungu wala uzito wa kulibeba tatizo hili.
Wengine wanakimbilia kuhukumu kuwa ni madhara ya kutoa mimba pasipo kujua kuwa sio wote wenye matatizo haya tulitoa mimba.
Pole mpenzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yupo kweli, na usiangalie nani anafanyai nini na nani afanyiwi, Mungu ni mwema kwa wema na wabaya ndo mana mvua hunyesha kwa kila mtu haichagui kwa mwema ndo inyeshe alafu kwa mwenye dhambi pawe pakame, hata jua ni la wote, ni kwa Neema tu

Gianna Bryant, mtoto wa Kobe Bryant, kafa na babake kwenye ajali ya helikopta.

Huyo binti kafanya nini mpaka maisha yake yakatishwe kikatili namna ile?

Wewe kama una uwezo wa kuzuia mwanao asife kwa ajali kama ile, utamwacha afe au utaizuia hiyo ajali?

Hakuna mungu.
 
Back
Top Bottom