Avriel
JF-Expert Member
- Jun 25, 2017
- 4,992
- 5,456
Mshukuru Mungu kwa hali unayoipitia..Ni mhanga kwa zaidi ya miaka 20. Nimezunguka hospitali mbalimbali na kufanyiwa vipimo mbalimbali ila haijawahi kubainika chanzo cha tatizo. Nimeombewa sana makanisani na kunywa dawa za mitishamba nyingi tu ila bado sijafanikiwa.
Nimejaribu hata kupandikiziwa mbegu zaidi ya mara moja bado ikashindikana.
Kuna watu hapa wanaropoka tu bila kujua uchungu wala uzito wa kulibeba tatizo hili.
Wengine wanakimbilia kuhukumu kuwa ni madhara ya kutoa mimba pasipo kujua kuwa sio wote wenye matatizo haya tulitoa mimba.
Ni maombi yangu kutoka ndani ya vilindi vya moyo wangu,Mungu akukumbuke na akupatie hitaji la moyo wako kwa utukufu Wa jina lake.
Sent using Jamii Forums mobile app