Wanawake kwa hizi akili, Mna haki ya kupigwa matukio

Kwani tunawasomesha wanawake wabadilike kuwa wanaume? Tunawaelimisha kwa vile ni haki yao kama ilivyo kwa wavulana.

Mawazo ya kipuuzi kuamini maisha ni kuajiriwa. Wenzetu wanajisifia kuwa waajiri siyo kuajiriwa
 
Wanauliza what do you bring to the table, yaani yale mambo unatakayomfanyia nyumbani hayahesabu. Tukisema haya tujamasishane tutafute hicho cha kuleta mezani wanalia 😁
Mtawala huwa anaangalia mgogoro tu sio kile kilichosababisha mgogoro, Typical sisiemu shenanigans 😂
 
For today i will reserve my comment..

I hate you sababu unajua ila unapotosha, you are being manipulative for some “known”reasons.

Not hating you per se 😅
 
Nimesomeshwa na mzazi wangu, sio mwanaume...nafasi yake ya uzazi kwangu ndio oliyomfanya anisomeshe na sio uanaume wake. Hata angekuwa mzazi wa kike peke yake angetimiza wajibu uleule. Wanawake hatumuoni mwanaume kama adui yetu hata siku moja ingekuwa hivyo wanawake wenye pesa zao wasingekuwa wanaolewa
 
Msingi mzima wa furaha ya ndoa ni mgawanyo wa majukumu ya mke na mume kulingana na mazingira yenu.

Anyway, labda sielewi ukisasa unavyofanya kazi. Embu niambie, kwanini mwanamke akifanya kazi haiwezekani kumtunza mume?
Sio haiwezekani, muda unakuwa mchache sisi ni binadamu tunachoka pia
 
Afanyiwe vyote Ila afundwe juu ya nafasi yake kama mke ikiwa familia zitataka aolewe. La sivyo wanawake nao waoe wanaume wawaweke ndani
 
Mila gani hizo zinazomfanya mwanaume kuwa muhanga?
 
Mila gani hizo zinazomfanya mwanaume kuwa muhanga?
Fikiria kijana anafundishwa na kushuhudia tangu utotoni kwamba kumpiga mwanamke anayekujibu vibaya ndo uanaume. Na anasifiwa mpaka na dada zake akifanya hivyo. Huyo akija kumpiga mkewe ukubwani huoni kwamba kwa sehemu kubwa hicho kitendo chake cha kikatili dhidi ya mkewe ni matokeo ya mila potofu alizolishwa na jamii maisha yake yoote ya utotoni na ujanani na si ubabe tu peke yake?

Hata tu huko kufuliwa boxer. Mwanaume anayetarajia umfulie boxer siyo anakufanyia ubabe au yupo kukuendesha. Ndivyo alivyokua programmed na mila na desturi. Mwanaume huyohuyo ukiishi naye America ya kaskazini anaweza kukufulia nguo yako ya ndani. Siyo kwasababu anakuogopa au sheria. Ni kwasababu mila za huko zitambadilisha mtazamo na matendo yake dhidi yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…