Tuna mshukuru kwa maoni yake , maana yameweza kutujukisha mwanamke ni wa namna gani , wa thamani kiasi gani na aje anapaswa kuthaminiwa.
Hoja yake ina mantiki sana ila kama msomi mwenye shahada 4 uwasilishaji wake haukua mzuri, ni uwasilishaji ambao kwa yoyote anaesikia mara ya kwanza atakerwa.
Nadhani ama naamini kule kusoma kwake hakukosa kujua ama kusoma namna gani ya kuwasilisha jambo katika jamii kisha ivutike kukusikiliza na kukuunga mkono hoja yako.
Hata mimi ambae sija soma kuna nyakati kadhaa nilipata jukwaa la kuwasilisha hoja na maelezo na waliokuwa wananisikiliza walikuwa wasomi wengi ambao sifikii hata asilimia ndogo ya upeo wao ila walivutika kunisikiliza na kuchukua pointi kurekodi kwenye note book zao.
Why ni kwa sababu ya unyenyekevu katika kuwasilisha, ni kujua wanao kusikliza ni aina ya watu wengi wenye kaliba tofauti, wanaojua kuliko wewe nk.
Ndio maana pake juu kuna mtu kasema mwanaume mmoja mlevi anaweza kuwa bora kiakili kuliko wanawake watatu wenye shahada.
Issue ni mwanamke yupo kwenye vita dhidi ya mwanaume, ndio maana hata comment za wanawake zimeonyesha kufurahishwa na jinsi mwanaume anavyo pata mashambulizi na atakavyo shindwa na mwanamke .
Siku zote wasicho fahamu wanawake ama wanafahamu ila ubinafsi wao umewaziba kujua ni kwamba mwanaume hana vita na mwanamke, ndio maana mwanaume yupo tayari kumsaidia mwanamke dhidi ya mwanaume mwenzake.
Popote pale alipofika mwanamke nyuma yake kuna nguvu kubwa ya kiume.
Hakuna hata mmoja kati ya mwanaume ambe kwa dhati kabisa angependa kumtweza mwanamke, ingawa katika uchache visa hivyo haviwezi kosekana na kati ya hivyo vichache sababu inaweza kuwa mwanamke ndie msababishaji.
Mwanaume hamuitaji mwanamke kumpikia wala kumfulia nguo za ndani.
Mwanaume bila mwanamke anaweza maisha,tukitoa uzazi.
Kimaumbile dunia haitaendelea kusimama kama mwanaume hata kuwepo hata mwanamke asome kiasi gani.
Ujanja wa mwanamke msomi ni ofisini tu, dunia haisimami kupitia kazi za ofisi.
Huku site hatuwaoni wanawake , kwa sababu maumbil na mfumo wa ulimwengu hauna wepesi wa mwanamke kusimama mahali pa mwanaume.
Hakuna hata mmoja asie mhitaji mwenzake zi mwanaume na si mwanamke, ila mwanamke ni mbinafsi ma mwenye kutamani siku zote mwanaume asiwepo kwenye maisha yake na ndio maana huwaza sana kifo cha mwanaume wake kuliko mwanaume anavyo muwaza mwanamke.
Mimi ni mwanaume mwenye binti wawili , mwenye mke na ambae nitahakikisha watoto wa kike watasoma vile inavyo takiwa ila ikitanguliwa na kumkuza katiki malezi ya kumfanya daima awe mwanamke anae wajibika kama mwanamke .
Natamani ningemuuliza yule dada mchungaji kwamba alikosa neno la kuanzia kwenye hoja yake akapata la kufua boksa?