Wanawake kwa hizi akili, Mna haki ya kupigwa matukio

Kwani tunawasomesha wanawake wabadilike kuwa wanaume? Tunawaelimisha kwa vile ni haki yao kama ilivyo kwa wavulana.

Mawazo ya kipuuzi kuamini maisha ni kuajiriwa. Wenzetu wanajisifia kuwa waajiri siyo kuajiriwa
Sijui umewaza kwa kutumia nini, ila elimu inambadilisha mtu yeyote yule.

Hata sisi wanaume elimu inatubadilisha sana tu, baada ya kupata elimu Kuna mila na desturi tunaziona zimepitwa na wakati, tunaanza kuishi maisha mapya ya kisasa, lakini pia uwezekano wa kutucontrol unakuwa ni mdogo kwasababu ya elimu tuliyonayo

The same na kwa mwanamke, nayeye akipata elimu kuna vitu anaviona ni kama vimepitwa na wakati, nayeye anakuwa na exposure ya maisha ya kisasa na anajihisi hataki kuwa controlled. Ujinga ni kufikiri au kuamini ni sisi wanaume pekeake tunayo haki ya kuchange tukipata pesa au elimu🤣🤣 ila wanawake hawapaswi kubadilika.

Aisee kama tunawaza hivyo, ni matumizi mabaya ya akili.
 
Afanyiwe vyote Ila afundwe juu ya nafasi yake kama mke ikiwa familia zitataka aolewe. La sivyo wanawake nao waoe wanaume wawaweke ndani
Mkuu elimu na pesa imetubadilisha sana sisi wanaume, mila na desturi nyingi sana tumezikataa baada ya kupata elimu na pesa. Wanaume tukipata tu elimu tunataka kuishi kisasa.

Sasa tunataka tujisahaulisha kwamba hata mwanamke akipata elimu na pesa atabadilika pia. Nayeye atafikiri na kuishi kisasa. Yani sisi tunajidanganya eti mwanamke anapaswa kubaki yule yule haijalishi ana elimu au pesa🤣🤣 sisi tukiipata hiyo package tunabaki walewale?

Tunapoteza tu muda, mwanamke huyu wa sasa tunaempa elimu hawezi tena kuwa kama mwanamke wa zamani. Mimi baada ya kupata mtoto wa kike kuna vitu nimejifunza na sitamani mtoto wangu akavipitie kwenye maisha yake.
 
Rudisha mipira miwili makao makuu yakawe allocated Kwa wenye uhitaji then wewe hamia huko ili ukakamiwe🤣
Sijui kama una mtoto wa kike, ila niamini mimi ukipata mtoto wa kike hutamuandaa hivyo unavyotaka wanawake wawe. Huwezi kumpata mwanamke wa zamani kwa hawa watoto wa kisasa.

Mimi nina kabinti kangu hapa, kwakweli sitamani kakaishi haya maisha ya changamoto nazoziona kwenye ndoa za watu wengi.
 
Hatimaye Rose kanisemea upuuzi nisioufagilia wa kufua viboksa na kuacha kutafuta pesa..!!

Wanaume sijui mtamuendesha mwanamke gani karne hii 😹

Kila siku mnakula za uso 😹
Hajasema msifue boxer Bali mmafanye zaidi ya hapo sijui kwanini kiswahili kinakuwa kigumu kiasi hichi kiasi ambacho kashindwa kueleweka na wengi
 
Sasa mkuu huyo mama kakosea wapi? au ni vile tu chagua kupinga badala ya kusikiliza kwa umakini ujumbe wake uko hivi Wanawake wasiishie pekee kufua boxer wafanye zaidi ya hapo kwasababu wamepewa opportunity ya kupata Elimu, Ajira na kutafuta hela ili hata pale mume akiwa na changamoto wawe na uwezo wakutatua kifedha hapo umeshindwa vipi kuelewa
 
Tunapoelekea wanawake walio tayari na majukumu ya kumtunza mume watakuwa wachache sana.
Ila sio ujumbe alioumaanisha huyo pastor wa kike namnukuu Wanawake wasiishie pekee kufua boxer wafanye zaidi ya hapo kwa kuchangia uchumi wa familia kwasababu yeye kasomeshwa mpaka akapata degree nne sio tu awe mama wanyumbani pekee na kumtegea mumewe ni lazima aachangie uchumi wa familia Sasa mkuu sijui kiswahili limekuwa kigumu kiasi gani mpaka mmeshindwa kumuelewa
 
Hiyo takataka haiwezi kupata mme! Bure kabisa!
Ni vile mmemuelewa vibaya ujumbe uko hivi Wanawake wasiishie pekee kufua boxer wafanye zaidi ya hapo kuchangia fedha kwenye familia kwasababu wamepewa opportunity ya kupata Elimu, Ajira na utafutaji wa hela haya niambie hapo ubaya uko wapi?
 
Anapotosha mkuu. Ni asilimia ngapi ya wanaume wanawazuia wake zao wasijiendeleze au wasiwe na kazi zao? Ni wachache sana. Wanaume wengi wanaunga mkono wazo la mwanamke kujishughulisha. Na wanawake wengi wapo mtaani wanafanya usafi, wanahudumu, wanatuuzia vyakula na kadhalika. Na wengi wana ndoa zao. Sasa anamdanganya nani?
 
Ujengewe mnara we Kaka!!!! Asiyeelewa hapa basi tena!!!!!
 
Ujumbe wake upo clear na well understood ni vile wabongo tunashida kukurupuka bila kusikiliza kwa umakini
 
Yeye katoa ushauri kwa wale wanaoprefer kuwa mama wa nyumbani na Kuna wengine wakishaolewa wanaambiwa na Wanaume zao waache kazi wabaki nyumbani
 
Wapi katika hayo maelezo aliyoandika au kwenye clip huyo Dada kasema kuwa atakuwa na dharau na kiburi kwa mume wake? Hayo umeongeza wewe na hiyo ndiyo insecurity yenyewe kutoka kwa wanaume!!!!
 
Mwenza hivi unadhani mimi naelewa hicho kinachowapanikisha? Hivi watanzania ni wajinga kiasi hiki? Mbona maelezo ya huyo mama yamenyooka tu vizuri?
Nashangaa wanaume wengine wanapanic!!! Halafu hao hao wanasomesha watoto wao wa kike!!!! Wanawasomesha wakawe mama wa nyumbani????!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…