Wanawake mnawezaje kuishi na mwanaume anayefokafoka?

Astaghifilullah!
 
Itabidi ujifunze ndondi, ndoa za sasaiv zataka kujipanga kwa mbinu zote[emoji23] uwe mkimya, mwenye busara hekima, mchapakazi, mwanasaikolojia, mjasiriamali, mwana mieleka, mwenye kidomo,, kahaba kitandani, mlezi na mzazi,, kazi tuko nayo walahi
Kungwi, the legend.....hadi raha
 
Yani Kuna wanaume wasumbufu jamani,,, Sasa mtu si ajue kuwa stress za nje hazihusiani na ndani?
 
Pole sana, binadamu tunatofautia sana, mimi binafsi ni mkimya sana hata kwenye makosa ya dhahiri hasira zangu hunielekeza kwenye ukimya, matokeo yake naonekana boya!
Cha kufanya endelea kutafuta nafasi nzuri ya kumwambia vile unakwazika na hio tabia yake, hata kama itachukua miaka mingi kubadilika atabadilika tu, akili ya binadamu imeumbwa na hali ya kujifunza na kubadilika kulingana na wakati na mazingira, so ipo siku atabadilika.

Pia mtu wa namna hiyo ikiisha mjulia basi wewe timiza wajibu wako kadiri ya dhamiri yako hata kama ataongea vipi wewe puuza tu usitarajie kupata amani kutoka kwake ilimradi tu wajibu wako unautekeleza. Itakusaidia sana kupata amani nje ya binadamu mwenzako kwa binadamu mwenzako tarajia makwazo tu.
 
Kama hana kero nyinginezo mzoee jitahidi kupuuza tu,, Tena siku nyingine akifoka jililishe kwa machozi maana wa hivyo wajuzi wa kubembeleza hatari na akiona chozi anajua umeumia pengine atapunguza,,
Ushauri mzuri sana trust me, kila akifikiria akikufokea utalia atapunguza ila anavyofoka na anakuona umekausha anahisi una jeuri.. Its kinda inferiority complex
 
Ushauri mzuri sana trust me, kila akifikiria akikufokea utalia atapunguza ila anavyofoka na anakuona umekausha anahisi una jeuri.. Its kinda inferiority complex
Hata mie nimewaza hivyo kuwa akifoka ajifanye mnyonge, huenda ikasaidia, nae alijibu kuwa alikuwa akilia na haikusaidia chochote,,
Kwa ninavyojua wanaume aina hii wengi wao wanapenda kunyenyekewa sana zaidi ya kawaida,, kupigiwa magoti, ujinyenyekeze kama unasujudu, ndo wale wanaopenda kunawishwa miguu na hii wanawake wa Tanga wanaiweza na ndipo hapo wanamwagiwa sifa kemkem,,
siku akiwa ktk mood nzuri atumie hapo kumueleza anavyokwazika,
 
Kwani kufoka ameanza mwaka huu?? Kama alikuwa hivyo tangu uchumba wenu na ukakiri kumtumilia mpaka kifo kiwatenganishe jikaze, maana katika zile shida ulizosema Kwa midomo yako bila kulazimishwa na ntu kwamba utavumilia ni pamoja na hiyo
 
Aachane naye aende wapi? Kamzidi miaka Saba kiufupi anamuona kama Mtoto, hapo cha msingi awe mtii na mnyenyekevu hiyo hali itaisha, akiondoka hamna waoaji si unaona singo Maza shuruba wanazokutana nazo
 
Na kucha amkate mwambieni awe soft Sio softness inapatikana tu Wakat wamahanjamu chumbani hivi mnajua hata wanaume wanapenda kudekezwa sometimes, aweke kichwa chake kwenye mapaja ya mkewe huku sotori na vijisifa vya hapa na pale vinaendelea atafoka hapo kweli??? Hakuna mkate mgumu mbele ya chai
 
Ungetuambia ndoa Ina miaka mingapi, jekabla ya hapo alikuwa anakufokea ya laa, nakama sivyo Basi Kuna namna anakuchukulia poa, na kwa kiasi Sasa haoni thamani yako wewe, vumilia
Huyu sidhani kama ana ndoa maana inaonesha mabaharia wanapishana tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!!! Kila wakati case mpya
 
Yataka moyo Sana kumdekeza mtu anaekufokea ovyo,,
 
Gubu tu hilo analo,Rudi tena kwa kungwi wako bibie akufundishe kumpa yotee..Gubu lote litakwisha..
 
Nunua kiredio kile cha bluetooth, hakikisha akiwa around unawasha mziki sauti ya juu usimpe chance ya kukupigia makelele....unafanya kazi zako huku unaimba imba tu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huko kwenye kumpea hafoki, kwanza sijawahi kumnyima toka anioe....ye mwenyewe anakiri hilo.
Ila hebu fikiria labda namtengea chakula, bahati mbaya wakati naweka glass mezani nikosee hesabu glass ijigonge, jamani atafokaaa, Yani atanifokea Kama mtoto.
ana gubu huyo, mvumilie tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…