Wanawake mtatuua na hizi michezo za siri

Wanawake mtatuua na hizi michezo za siri

shuka chini

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2024
Posts
842
Reaction score
1,928
Habari za muda huu wadau .

Moja kwa moja kwenye mada ipo hivi mimi ni baba wa familia mwenye mke na mtoto mmoja .

Nimekuwa nikiacha matumizi hapa nyumbani sasa ajabu kila siku ninaacha matumizi hapa nyumbani nakuta mboga za ajabuajabu.

Nikaanza uchunguzi wangu taratibu katika fukunyuafukunyua nakutana na daftari limeandikwa majina matatu, lake na wamama wawili . Wanacheza mchezo na nimegundua mahali anapoficha hela .

Sasa wadau nizichukue au nisubirie ziwe nyingi kidogo. Yeye mke wangu anajua sijui kama kuna mchezo wanacheza na hapa nataka nimpige marufuku.
 
Mimi binafsi, Mwanaume na mwanamke ni viumbe viwili tofauti kabisa...Wana mambo Fulani ya ovyo sometime mpaka unaweza kuwa huyu anafikiri kama Mimi kweli?
So mkuu kwa muktadha huu wewe unajitoa pande zote?

Umeandika as if wewe ni kiumbe tofauti kimekaa mahali kikiwachora wanaume na wanawake wanaoishi dunia hii.
 
Mkuu hio ni pesa ya misosi iliyopita... Mwambie ukweli kua unaijua kinachoendelea halafu weka mipaka... Mpe na outcome kama atarudia utafanya kitu gani... Kwanza kwanini naficha, mwambie akirudia utamuacha akacheze vocoba kwao
 
Sasa wadau nizichukue au nisubirie ziwe nyingi kidogo. Yeye mke wangu anajua sijui kama kuna mchezo wanacheza na hapa nataka nimpige marufuku.
Sema nimejikuta nacheka hapa kwenye hii paragraph... Maana option iliyopo ni moja tu, kwamba ni kuzichukua ila unataka ushauriwe uzichukue sasa hivi au usubiri subiri ziwe nyingi kidogo😂😂
 
Uwe unachukua kidogo kidogo, ila asijue kama unajua maana sio kwamba ataacha bali atabadili mbinu. Si rahisi mwanamke kuingia katika mfumo unaokubalika kwa mwanaume, ni vigumu mno.
Ila kwa kuwa anakufanyia umafia kwenye bajeti, na wewe uwe unachomoa pale anapohifadhi kidogo kidogo.
 
IMG_1327.jpeg
 
Back
Top Bottom