Wanawake ndoa ni utii, acheni kujaza ujinga wadogo zenu

Wanawake ndoa ni utii, acheni kujaza ujinga wadogo zenu

Hayo usemayo yako Afghanistan na Saudi Arabia - Siyo hapa Tanzania
Sheria na kanuni zetu zinampa mwanamke haki ya elimu na ya kumiliki mali na ya uongozi
Ukitaka mwanamke akutii na akunyenyekee basi nenda kwa Taliban siyo hapa Bongo ambayo ni sekula. BADILIKENI !!!
 
Umemaliza kila kitu dada, shida ni kwamba wanawake tunataka kubeba majukumu ya wanaume, hasa hili jukumu la KUPENDA, mwanamke wake mi UTII, Kupenda sio Kazi yetu....kabla sijalijua hili niliteseka sana...
Mwanamke ukijifanya unampenda mwanaume utataka umcontrol, umpe pesa...which ni makosa makubwa sana (it is like you womanize him) we mtii mumeo, hakikisha unamtunza kuanzia jicho lake (ujiweke vizuri wewe na nyumba yako), pua yake (unukie vizuri), tumbo lake(mpikie chakula kizuri), mwili wake (mavazi yake yawe masafi) na masikio yake (asisikie maneno ya kero kutoka kwako)...
Hapo mwanaume asipokupenda huyo mgonjwa.
Tatizo Sisi tunajifanya haki Sawa, tunataka na Sisi tupende mwisho tunaishia kugombania password za simu...
NB. Hakuna usawa Kati ya mwanamke na mwanaume na hautokuja kutokea.... ukiona unatoka nyumbani huombi ruhusa Bali unatoa taarifa na ukirudi mume hata hakukosi Kosi na kibao, ujue hapo huna ndoa, tafuta shughuli nyingine ya kufanya
Natarajia kuolewa hivi karibuni naomba uwe kungwi wangu😂😂😂
 
Mamy K baada ya yote mazuri uliyosema kuhusu mke mwema, naongezea mke pia awe mtundu kitandani mume atafurahi zaidi.

Mtuonyeshe mahaba kunoga msituonee aibu hakuna mume atakayekuona malaya bali atainjoi.

Fungukeni nini tuwafanyie mfurahie shoo
Nilikua napekua hii comment hatimae [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hua nawaza nyumba kama chombo kinachopaswa kuendeshwa, hivi chombo kinawezaje kwenda na kufika destination yake kikiwa na madereva wawili na wote wanataka waendeshe kwa wakati mmoja? Ni ngumu sana chombo kitaenda mlama tu
 
Back
Top Bottom