Wanawake ndoa ni utii, acheni kujaza ujinga wadogo zenu

Wanawake ndoa ni utii, acheni kujaza ujinga wadogo zenu

Msemo halisi ni kuwa pepo yako iko chini ya unyayo wa mama yako....
Pepo Iko chini ya nyayo ya mama Yako ,ukiolewa mumeo Ndo Pepo yako,mwanaume Ndo Pepo yake Iko chini ya mama yake ht akioa
Kuna kisa Cha yule mwanamke aliyebashiriwa Pepo Kwa kumtii mumewe,alimzuia asitoke ndani mpk arudi safari,akauguliwa na baba yake ,akaambiwa hakwenda maana mmewe hakuwepo,mpk amekufa baba hakwenda Kwa kua Hana ruhusa ya mmewe,Baadae akarudi akasafiri tena akapewa tena wosia ule ule ,akauguliwa na mama ake mpk akafa hakwenda Kwa kua hana ruhusa ya mmewe....
Yule mwanamke alibashiriwa Pepo Kwa utiii wa kumtii mume...
Nadhani km sijakosea ntasahihishwa na wajuzi zaidi
 
Umemaliza kila kitu dada, shida ni kwamba wanawake tunataka kubeba majukumu ya wanaume, hasa hili jukumu la KUPENDA, mwanamke wake mi UTII, Kupenda sio Kazi yetu....kabla sijalijua hili niliteseka sana...
Mwanamke ukijifanya unampenda mwanaume utataka umcontrol, umpe pesa...which ni makosa makubwa sana (it is like you womanize him) we mtii mumeo, hakikisha unamtunza kuanzia jicho lake (ujiweke vizuri wewe na nyumba yako), pua yake (unukie vizuri), tumbo lake(mpikie chakula kizuri), mwili wake (mavazi yake yawe masafi) na masikio yake (asisikie maneno ya kero kutoka kwako)...
Hapo mwanaume asipokupenda huyo mgonjwa.
Tatizo Sisi tunajifanya haki Sawa, tunataka na Sisi tupende mwisho tunaishia kugombania password za simu...
NB. Hakuna usawa Kati ya mwanamke na mwanaume na hautokuja kutokea.... ukiona unatoka nyumbani huombi ruhusa Bali unatoa taarifa na ukirudi mume hata hakukosi Kosi na kibao, ujue hapo huna ndoa, tafuta shughuli nyingine ya kufanya
 
Heshima hailazimishwi, muhimu ni mawasiliano na upendo, ukiona baba anatoka analala nje siku mbili bila maelezo ya kutosha au mwanamke haagi kwa sababu jana mme hukuaga, hakuna ndoa hapo mnapoteza muda tuu na tafuta pa kutokea kabla hamjauana
Ongeza sautiiiiiii
 
Siwezi kufa kisa mwanaume, aisee na ugali ulivyomtamu huu [emoji16][emoji16]. Kwani si ndo mana Kuna neno "kuachana" my dear?. Na kama ulisoma vizuri, nimesema kwamba "ukiona manyanyaso na mateso yamezidi ni haki yako kujisogeza pembeni na kulea watoto wako,ni marufuku kuvumilia manyanyaso na mateso. Ni sawa kuachia ngazi lakini si sawa kutenda Yale ambayo yeye anatenda ukifikiri kwamba unamkomoa mwanaume kumbe unajiharibia mwenyewe sifa yako mtaani. Kwa sababu mwanaume ni malaya na ww unageuka malaya, utakufa kwa magonjwa. Ilhali una uwezo wa kusogea pembeni ukafanya mambo yako. Kamwe usivumilie ukatili katika ndoa, imekushinda, basi sogea pembeni.
Hapo sawaaa umeelewekaa.
 
Haisaidii kitu, iwe kwa mwanaume au mwanamke. Mimi leo mwanamke akinisaliti na mimi nikalipiza kwanjia yeyote ile hata kwakusaliti, kisasi hakitanibadilishia taswira iliyojijenga kuwa mwanamke amenifanyia dharau mno. Yaani hata nilale na wanawake wa dunia nzima hiyo trauma haitanitoka kamwe maana ni point of failure ambayo kila nikiikumbuka sitaweza ibadilisha. Hivyo hata kumuangalia au kumsogelea sitaweza tena maana atakuwa alama ya udhaifu wangu. Kilichobora kwangu ni kukaa naye mbali sana ambapo sitamsikia wala kumuona, hivyo nitajitenga naye. Labda kwanyie wenzetu ni tofauti ila kisasi huangamiza roho, ni kama tone moja la mvua kwenye jangwa kubwa. Itakuuwa baadaye kwa guilt.
Kwahyo ni Kuachanaa tyuuh.
 
Back
Top Bottom