Wanaume wengi pia hatujui namna ya kuwa viongozi kwenye ndoa zao. Utii kutoka kwa mwanamke hauji tu ati kwa kuwa umemuoa.
Kuna namna unapaswa kuishi kama mwanaume unayejielewa, kiongozi, baba na mlinzi wa familia. Mkeo mwenyewe ana-salute kwako anajua kweli yuko na mme jembe lazima akuheshimu tu.
Lakini mwanamke akikubishia jambo dogo tu, tayari unaamua ukitoka kazini unapitia bar unarudi akishalala ati unaogopa kelele za mkeo.
Hapo mkeo lazima akushangae na akuone una mapungufu hasa ya kiuongozi.
Mwanamke anaweza kukuhoji kuhusu jambo lolote lile maana naye ni mwanadamu na ni partner wako kwenye maisha.
Sasa wewe badala ya kuonesha uanaume wako wa kutoa hoja zenye majibu na kuweka msimamo na uonvozi juu ya hoja hiyo unaishia kukimbilia bar.
Ni shida kubwa wanaume tunayo.
Hatujielewi haswa na tumekuwa waoga mno wa maisha na debate za kwenye ndoa. Mwanamke mpaka anashindwa kuelewa aishije na wewe maana huonekani kujua lolote na wala humuongozi kujua na kuufuata uelekeo wenu.
Sasa mwanaume anachelews kurudi nyumbani ati kisa hapendi mkewe anavyokagua simu yake[emoji3][emoji3][emoji3]. Wakati ukichukulia positively ni kwamba inawezekana anakupenda huyo na anaogopa kuibiwa baaaas.
Kwahiyo kama una mambo yako jua jinsi ya kuyaficha kwenye simu asiyaone au yafute. Akikagua anakukuta swafi baadae anazoea tu.
Tushaambiwa tuishi nao kwa akili. Akili asipoziona kwako anakudharau.