Wapi nikatafute maisha kati ya Botswana, Mauritius,Namibia au Sychelles?

Wapi nikatafute maisha kati ya Botswana, Mauritius,Namibia au Sychelles?

Kuna siku nilipata nafasi ya kuhudhuria mkutano ulifanyika Masaki. Mgeni rasmi alikua ni balozi mstaafu wa Tanzania nchini Canada.
Aliongea issue nyingi ila alisema katika kipindi chake chote akiwa Canada hakuwahi kupewa tangazo la uhitaji wa nafasi za ufadhili wa masomo nchini Canada lakini cha ajabu kila mwaka watanzania karibia 200 walikua wakiingia Canada kwa ajili ya ufadhili wa kimasomo. Hitimisho, ni kuwa kutafta taarifa sahihi na kuzifanyia kazi kutakufikisha unapotaka kwenda.
Otherwise, utapiga domo sana JF unataka uende kule sijui wapi mwisho wa siku hutoki. Fanya maamuzi, tafta taarifa hata katika balozi za nchi husika unazotaka kwenda kisha chukua hatua.
Wengi wa unaowaomba ushauri humu hawako kwenye nafasi ya kukusaidia na wao wana matamanio tu ila hawana purpose. Nisamehe kama utahisi nimefanya personal attack.

Mwisho atasema wabongo wa hizo nchi hawatoi connection. Kwenda sehemu 99% ni dhamira na juhudi zako.
 
Nenda South, uko kwingine njaa tu omba omba.

mwanyaluke Kuna jamaa huwa anachukua nguo na viatu anapeleka Botswana hii imekaaje?
Nguo na viatu unaweza fanya , hata ukiwa kule kama unatoa china , Botswana ni watu flan sio wanjanja ila maisha Yao mazuri , ila kwangu nilichokiona ni ukiwa na fani hizi za mtaani inalipa, kazi ya fundi ninayomlipa kurekebisha pampu ya gari botswana ni mshahara huku wa mtu Tanzania , kwa nini ipo hivyo mafundi hamna , na ndio maana watanzania wengi wanaotoka haasa mbeya walikuwa wamekimbilia Malawi saizi unawakuta botswana , Zim,
 
Kwa uzoefu wangu niliofika kwa mda Cha kwanza hawa jamaa wapi makini sana kwa mgeni maswali ambayo watakuuliza cha kwanza unatakiwa uwe na show money isiopungua Dola 500 Cha pili unawenda wap au mwenyeji wako ni nani na huyo mwenyeji wako lazima wajue ana Kaa sehemu Gani na anajishuhulisha na nini na wakikugongea passport mda utaokuwepo kwao usije ukazidisha tarehe ya kukaa kwao ukizidisha Wana faini zao au jela na kingine hawa jamaa Wana ubinafsi sana kwa raia Mimi nilipoingia gaberon walipokagua passport yangu waliniuliza maswali mengi sana kabla hawajanigongea passport na kingine Cha muhimu sana epuka kumchukuwa mke wa mtu au x wa mtu wanawake ni wazuri sana na ukimwi ni mwingi sana na nchi nzuri sana ya kutafuta maisha hasa ukiwa unafanya biashara na biashara ambao itakayokuchomoa haraka ni biashara ya vinyago au kacha kama za huku kwetu na raia wengi hawapendi kufanya kazi ngumu maisha Yao asilimia kubwa ni ya bata
 
Fursa hasa ni zipi mgeni anaweza fanya zikakubarika na wenyeji?
Fursa ni nyingi inategemeana na wewe kwanza kama ni biashara ana na kacha hizi za kwetu wapelekee vinyago vya kuchonga kama vile wanavyochonga kule mwenge hata biashara za nafaka kama Mchele kama umeenda kuangalia ingia kwenye migodi ya almasi kule Kuna pesa nazani katika dunia wachimbaji wakubwa ni wao
 
Back
Top Bottom