Muju4
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 5,489
- 7,446
Nawasalimu wanajukwaa,
Kwanza nianze kwa kuwapongeza kwa minyukano ya hoja humu jukwaani kwa ustaarabu wa hali ya juu, hii inaonesha jukwaa bado lina watu makini sana.
Nikirudi kwenye mada yangu,ni ukweli usiopingika kuwa wapinzani hamkujipanga vyema kwa ajili ya uchaguzi yanayotokea ACT ni mfano halisi ambapo Kiongozi mkuu, mwenyekiti na mgombea uraisi wamepishana misimamo, vile vile kwa Lissu amekuwa mtu mwenye kukurupuka na mara zote kuongelea watu,kutukana viongozi, kutuhumu kila taasisi na hivyo kushindwa kueleza atawafanyia nini Watanzania.
Magufuli atabebwa na rekodi ya kazi nzuri alizozifanya wananchi wanamkubali na wanampenda sana na watamchagua kwa kishindo hapo kesho.
Hebu tuwaze nani ataacha kufurahia yafuatayo:-
1. Umeme vijijini
2. Barabara za lami zilizounganisha maeneo mengi ya nchi kwasasa unaweza kutoka Mtwara hadi Kagera kwa Taxi.
3. Amerudisha nidhamu ya hali ya juu kwa watumishi wa Umma.
4. Vituo vya afya kila kata
5. Mikopo elimu ya juu pamoja na makazi ya wanafunzi hebu tukumbuke shida walikuwa wakizipata vijana wetu UDSM.
6. Ameongeza makusanyo ya kodi na sasa miradi mingi inaendeshwa kwa fedha za ndani.
7. Amekuwa mfano katika ubanaji wa matumizi kwa kupunguza safari za nje ambazo amewakilishwa na wajumbe aliowateua hivyo kupunguza gharama kama angeondoka na ujumbe wake mzima.
8. Kama kuna jambo lilikuwa linatuchafua ni la madawa ya kulevya maana haikuwa ajabu kusikia Watanzania wakikamatwa na madawa ya kulevya kila sehemu Duniani ila kwa sasa hilo ni historia.
9.Ujenzi wa miundo mbinu ya kisasa standard gauge ambayo itaenda kuboresha usafiri wa reli.
10. Elimu bure.
11. Mapambano ya Covid 19 hapa wabunge wa upinzani walikimbia bungeni na hata kuwafukuza wale ambao hawakukubaliana na nao wakanda mbali wakitaka wananchi wafungiwe yaani"lockdown" lakini Magufuli alisimama imara na kusisitiza hakuna lockdown.
12. Amekuwa msikivu na kusikiliza shida za wananchi na kuzitatua hapo hapo kila alipokuwa akipita njiani kuelekea katika ziara za kikazi.
13. Ameweza kusimamia kuletwa sheria za madini ambazo zitawabana watu ambao wamekuwa wakitunyonya kwa kutupa gawio ambalo halikuwa sawa na kile wanachokichukua.
14. Ufufuaji wa shirika letu la ndege.
Zipo kazi nyingine nyingi sana ambazo ndio zitambeba Rais Magufuli.
Msione vyaelea mjue vimeundwa.
Kesho tunakwenda kumpa kura nyingi za Upendo na wivu mkubwa Magufuli, na haki kusema anastahili miaka 5 Tenaaa.
JPM anatosha
CCM kwa maendeleo ya Tanzania