WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Je huu waraka ndiyo uliotolewa na baraza la maaskofu Tanzania yaani TEC? Nini kinaweza kuthibitisha hilo maana miaka yote waraka kama huu ukitolewa unasomwa kwenye makanisa yote Tanzania ,sasa huu mbona haujasomwa kwenye makanisa??? Au kama kuna muumini ambaye ameusikia ukisomwa kutoka kwa paroko wake atuthibitishie
Maaskofu wenyewe wamejiorodhesha mwisho wa waraka huo. Ni kweli ni authentic kutoka kwa Maaskofu Katoliki. Ni mara ya kwanza kwa Baraza la Maaskofu lenyewe kutoa waraka wenye ujumbe wa aina hii, yaani wenye kauli kali katika hali ya siasa ya nchi yetu. huko nyuma hizo nyaraka zilitolewa na Tume ya Haki na Amani ya Baraza hilo, ambayo husimamiwa na Askofu mmoja tu. Lakini hii ni kauli ya Maaskofu yote chini ya Rais wao, ambaye ndiye msemaji rasmi wa Kanisa Katoliki hapa Tanzania.
 
Walikuwa wapi kuyasema haya tangia mwaka 2016 ??
Au kwasababu wananufaika na huu mfumo kwa namna moja au nyingine ??
Marx was right when he uttered this bold statement "Religion is an Opium of the People"
Hapa hakuna jipya ni yale yale tu ya Catherine De' Medici na Gregory XIII just disgusting!

NB: Uwe na kwaresma njema na usisahau kutubia hii dhambi...
Ni kweli wengi tulikuwa tunashangaa iweje viongozi wa Makanisa wamekuwa kimya? mawazo mengi yalitolewa, yakiwemo kama haya ya kwako. Lakini basi kauli ndio imetoka, na ni kali haijawahi kutokea. siyo bure Serikali nayo inavuta pumzi kujiuliza ijibu vipi. la msingi ni kwamba kuna Historia imeandikwa hapa. Baraza la Maaskofu halijawahi kutoa kauli kali namna hii, tena kwa ngazi hii. hayo ni mambo muhimu. Kanisa limeshapiga mstari. tunasubiri viongozi wengine wa dini waungane na wakatoliki. kwa hiyo kuanzia sasa Serikali itatakiwa kujipanga inajieleza vipi kwa wananchi.
 
Hawa maaskofu wameshindwa kuhubiri siku hizi
wanapoikosoa serikali ndio huwa tunasema wameshindwa kuhubiri. Lakini wanapoisifia, tunafurahi wala hatuhoji mbona wanachanganya dini na siasa? Wanasiasa kutwa wanakwenda makanisani na wanatoa hotuba huko na kuomba waombewe. huwa wanafuata nini? Lakini basi, Siasa ni mfumo mzima wa maisha, huwezi kutofautisha na dini. cha kujiuliza ni je, wamesema kweli?
 
Sipati picha wangekuwa ma sheikh ndo wametoa waraka kama huu..wangeandamwa na tuhuma na vitishoo... dah
 
Ni kweli wengi tulikuwa tunashangaa iweje viongozi wa Makanisa wamekuwa kimya? mawazo mengi yalitolewa, yakiwemo kama haya ya kwako. Lakini basi kauli ndio imetoka, na ni kali haijawahi kutokea. siyo bure Serikali nayo inavuta pumzi kujiuliza ijibu vipi. la msingi ni kwamba kuna Historia imeandikwa hapa. Baraza la Maaskofu halijawahi kutoa kauli kali namna hii, tena kwa ngazi hii. hayo ni mambo muhimu. Kanisa limeshapiga mstari. tunasubiri viongozi wengine wa dini waungane na wakatoliki. kwa hiyo kuanzia sasa Serikali itatakiwa kujipanga inajieleza vipi kwa wananchi.

Kinga ni bora kuliko tiba,
Katika mtazamo wako unadhani huu Waraka unaweza kubadilisha chochote ndani ya nchi katika kipindi hiki ??
Mambo mengi sana yameharibika hapa nchini na madhara yake hatutayaona leo wala kesho lakini ni makubwa sana.
Huu waraka hauwezi kubadilisha kitu chochote wala lolote. Jiulize kama nyaraka za Kanisa Katoliki zingekuwa zinabadilisha uongozi basi Uongozi wa Awamu ya nne wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ungekuwa ulishabadilishwa muda mrefu sana maana kila kukicha kulikuwa na matamko makali ya Baraza la Maaskofu.

Sasa wao wamesubiri miaka miwili (2) imepita ndiyo wametoa waraka,
Watu walivyokuwa wanapotea, demokrasia inaminywa, uhuru wa mahakama unadharauliwa na kuminywa upinzani wao walikuwa wapi ?? Umeongelea kuungwa mkono na madhehebu mengine lakini umesahau kwamba Madhehebu mengine yalianza kukemea haya maovu mapema sana. Mbona Kanisa Katoliki halikuunga mkono hizi juhudi za madhehebu mengine ?? Halafu usisahau kwamba wakati Madhehebu mengine na baadhi ya maaskofu wa Katoliki wenye uchungu na nchi wanakemea na huu Uovu Askofu Pengo alikuwa anamkingia kifua Raisi Magufuli na kusema huu siyo msimamo wa Kanisa, nauliza leo hii kimewakuta nini kuja na huu waraka ??

NB: Unakumbuka Tanzania tulibakia sana hatua chache kufanya mapinduzi makubwa sana kwenye Mchakato wa Katiba miaka michache iliyopita ?? Hivi tukumbushane Madhehebu mengine yote yalivyokubali kusimama na wananchi ni nani aliyevuruga ile nguvu ya Umoja ?? Hawa Maaskofu wakiitwa Wanafiki na kufananishwa na Mafarisayo watakuwa wanaonewa kweli ?? Tafakari sana na Ukumbuke kwamba nyaraka za namna hii zinaweza kuwadanganya Watanzania wachache wasiojua lakini werevu wameshang'amua kwamba huku ni kufukuza upepo tu na kujisafisha mbele ya Umma kwamba siku yakitokea ya kutokea muwe na sababu ya kusema kwamba "Mbona na sisi tulikemea". Hii dhambi mnayoifanya dhidi ya roho za Watanzania karibia milioni 46 itawatafuna sanaa na Mungu wa Mbinguni anaona. Kama siyo leo mtajutia kesho!
 
Mkuu kwa Kanisa Katoliki, mkubwa ni mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu kwa muda hubo sino Kardinali kama wengi wanavyodhani
Kwa kawaida mkuu akiwa kimya sana, na mdogo akawa ndio active zaidi, basi mdogo ndio huonekana mkuu. Na hata ukiangalia, utagundua kardinali ndio ambaye akiunguruma tu watu wanakaa sawa, sio Siri-kali tu, mpaka waumini wote.
 
Kuna watu ktk nyuzi kama hawatiagi mguu kabisa.
 
....Namsubiri yule mheshimiwa Alhadi mzee wa totoz ajitokeze tena kukemea viongozi wa dini kuingilia siasa.......
 
Sio rahisi kwani vinaitwa ''visakramenti'', kufungia ni kuingilia uhuru wa kuabudu!!!

Kwani mpaka sasa Uhuru wa kuabudu upo?Wale walioshiriki ibada huko Mufindi waliambiwa wasali haraka ili wakampokee Makamu wa Rais bado unaimba nyimbo za enzi ya JKN.
 
Kinga ni bora kuliko tiba,
Katika mtazamo wako unadhani huu Waraka unaweza kubadilisha chochote ndani ya nchi katika kipindi hiki ??
Mambo mengi sana yameharibika hapa nchini na madhara yake hatutayaona leo wala kesho lakini ni makubwa sana.
Huu waraka hauwezi kubadilisha kitu chochote wala lolote. Jiulize kama nyaraka za Kanisa Katoliki zingekuwa zinabadilisha uongozi basi Uongozi wa Awamu ya nne wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ungekuwa ulishabadilishwa muda mrefu sana maana kila kukicha kulikuwa na matamko makali ya Baraza la Maaskofu.

Sasa wao wamesubiri miaka miwili (2) imepita ndiyo wametoa waraka,
Watu walivyokuwa wanapotea, demokrasia inaminywa, uhuru wa mahakama unadharauliwa na kuminywa upinzani wao walikuwa wapi ?? Umeongelea kuungwa mkono na madhehebu mengine lakini umesahau kwamba Madhehebu mengine yalianza kukemea haya maovu mapema sana. Mbona Kanisa Katoliki halikuunga mkono hizi juhudi za madhehebu mengine ?? Halafu usisahau kwamba wakati Madhehebu mengine na baadhi ya maaskofu wa Katoliki wenye uchungu na nchi wanakemea na huu Uovu Askofu Pengo alikuwa anamkingia kifua Raisi Magufuli na kusema huu siyo msimamo wa Kanisa, nauliza leo hii kimewakuta nini kuja na huu waraka ??

NB: Unakumbuka Tanzania tulibakia sana hatua chache kufanya mapinduzi makubwa sana kwenye Mchakato wa Katiba miaka michache iliyopita ?? Hivi tukumbushane Madhehebu mengine yote yalivyokubali kusimama na wananchi ni nani aliyevuruga ile nguvu ya Umoja ?? Hawa Maaskofu wakiitwa Wanafiki na kufananishwa na! Mafarisayo watakuwa wanaonewa kweli ?? Tafakari sana na Ukumbuke kwamba nyaraka za namna hii zinaweza kuwadanganya Watanzania wachache wasiojua lakini werevu wameshang'amua kwamba huku ni kufukuza upepo tu na kujisafisha mbele ya Umma kwamba siku yakitokea ya kutokea muwe na sababu ya kusema kwamba "Mbona na sisi tulikemea". Hii dhambi mnayoifanya dhidi ya roho za Watanzania karibia milioni 46 itawatafuna sanaa na Mungu wa Mbinguni anaona. Kama siyo leo mtajutia kesho!
Mimi mwenyewe nimepinga sana kitendo cha Kanisa Katoliki kurudi nyuma katika kupigania haki za watanzania. Ila ninachofanya ni kuwa realistic. Kuhusu Katiba aliyevuruga ni Jakaya Kikwete baada ya kugeuka nyuma, sijui alionywa na akina Mkapa? Kanisa Katoliki lilifanya kazi kubwa sana, ingawa Kardinali Pengo alivunja nguvu jitihada hizo. lakini mvunjaji hasa ni Kikwete mwenyewe aliyeanzisha huo mchakato toka mwanzo.

Unasema madhehebu mengine yamekuwa yakikemea toka mapema? siyo sahihi! Ni juzi tu wakati wa Krismasi ndio Maaskofu walianza kukemea, nao ni KKKT na Katoliki. kabla ya hapo ilikuwa kimya kabisa. Lakini hata hivyo tofautisha kemea ya Askofu mmoja mmoja, na kauli ya Kanisa zima ambayo ni rasmi. hakuna dhehebu la kikristo wala waislamu ambao wametoa kwa kiwango hicho.

Unauliza Waraka unasaidia nini, kwa kweli hakuna chochote kinachoweza kumzuia JPM kufanya chochote anachotaka hivi sasa. isipokuwa, unapokuwa na Maaskofu wametoa tamko kama hilo, unaondoa ule uhuru wa serikali kuongea kwa kujinasibu. it is on the defensive. hiyo inapunguza kasi yake ya kutenda maovu. pia inagalvanise opposition both from outside and inside. pia taarifa kama hizi zinasaidia vyombo vya nje ambavyo vinaweza kufuta baadhi ya mikataba kutokana na kutoridhishwa na hiki au kile. Kumbuka pia kwamba Madikteta wote wanapenda kusikika vizuri. hivyo publicity kama hii inawakera sana, na watajitahidi kuiepuka. hiyo itatusaidia. pia angalau tutashuhudia kupungua kwa "ziara za Rais katika Makanisa na hotuba za kwenye mimbari" huku akiomba "kuombewa". haituongezei ubwabwa lakini angalau inatupunguzia kero.
 
Hao maaskofu wa kanisa katoliki Tanzania ni wasemaji maneno matupu bila matendo kama wenzao wa nchi ya DR Congo.

Waraka wa wajumbe TEC ni kelele za debe tupu hayana athari kwa serikali yao kama mnavyoona sasa kinachoendelea nchini.

Kanisa Katoliki Tanzania limetoa waraka kwa ajili ya kuwaandaa waamini wake kwa ajili ya kipindi cha Toba, kinachoanza rasmi Jumatano ijayo tarehe 14 Februari 2018 [ambayo ndiyo siku ya wapendanao, Valentine. tusherehekee kwa Toba eeeh tafadhalini!]. Kipindi hicho hujulikana pia kama KWARESIMA, ambacho kinahitimishwa na JUMA KUU na kisha sikukuu ya PASAKA.

Kama una haraka sana, soma ukurasa wa 11 na 12 (kurasa orijino) au ukurasa wa 14 na 15 kwa kurasa za PDF. Naambatanisha waraka huo.
Karibu! Ni nondo Kali!

=======

Maaskofu Katoliki watoa msimamo kuhusu masuala ya Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii

f1771774c03dc128b4ace4aa419e3351.jpg


031c2b5fb1cb36dcf26e0f2f70abaf9b.jpg

ceaa75236b2d1b4546253650ed852b54.jpg


----------------------

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa ujumbe wa Kwaresma wa mwaka 2018 ndani yake likitoa msimamo kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini.

Ujumbe huo ulioandikwa na maaskofu wote 35 wa TEC wakiongozwa na Rais wake, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa upo katika kitabu cha kurasa 20 ikiwa ni maandalizi ya ibada hiyo ya siku 40, kipindi ambacho ni cha mfungo wa sala kukumbuka siku 40 za Kristo kufunga na kwenda jangwani.

Hali ya kisiasa

Katika ujumbe huo, TEC imesema uamuzi wa Serikali kuzuia maandamano, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni kwenda kinyume cha Katiba ya nchi.

Baraza hilo pia limeonya hatua ya Serikali kuvibana vyombo vya habari ikiwa pamoja na kuvifungia kwa sababu mbalimbali.

“Kufungiwa huku kwa vyombo vya habari kumeenda sambamba na kuminya uhuru wa Mahakama na Bunge kwa njia ya kuminya haki wabunge na kutowapa nafasi ya mikutano ya hadhara kama haki yao ya msingi ya kikatiba.”

Alipopigiwa simu ili kutoa maoni ya upande wa Serikali kuhusu ujumbe huo, Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbasi alisema, “Sijaliona bado tamko husika kwa hiyo siwezi kujibu hoja ambayo sijaisoma kwa sasa.”

TEC imetoa ujumbe huo katika kipindi ambacho vyama vya siasa, hasa vya upinzani vikilalamika kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara baada ya Serikali kuipiga marufuku mpaka mwaka 2020, isipokuwa kwa wabunge walioshinda uchaguzi ambao wameruhusiwa kufanya mikutano kwenye majimbo yao.

Ugumu huo umetajwa na vyama hivyo kwamba unapunguza nguvu ya ushindani kwa vyama vya upinzani kukikabili chama tawala.

“Kikatiba, nchi yetu inafuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katiba na sheria mbalimbali zimeainisha utaratibu wa kazi na shughuli za vyama vya siasa. Ili kuhakikisha kwamba shughuli za vyama vya siasa zinakuwa endelevu, vyama vyenye kukidhi vigezo hupewa ruzuku kupitia bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge,” unaeleza ujumbe huo.

“Hata hivyo, shughuli za, siasa bado zinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola. Maana yake ni kwamba shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa, kama vile mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na hata mikutano ya ndani, ambayo ni haki ya kila raia, zimekoma mpaka uchaguzi mwingine. Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na sheria za nchi.”

Kuhusu vyombo vya habari, TEC imesema Serikali imepunguza wigo wa uhuru wa wananchi wa kupata habari na maoni ya kujieleza na kueleza kwamba kwa ujumla wake, mazingira hayo yatasababisha jamii kufarakana na hata kujenga chuki.

“Kumekuwapo pia hali ya vurugu katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi hizi zinaacha nyuma uchungu, hasira, tamaa ya kulipa kisasi na hata kususia chaguzi nyingine,” unasema ujumbe huo wa TEC na kuonya kuwa kama hali hiyo itaachwa, itakuja kusababisha mifarakano mikubwa itakayobomoa amani na umoja wa kitaifa.

Kiuchumi

Kuhusu uchumi, TEC imetoa mambo sita ya kujiuliza; “Tunazitumiaje mali na rasilimali nyingine tulizokabidhiwa na Mungu kama mawakili wake? Tunalipa kodi stahiki kwa ajili ya kugharamia huduma za jamii ambazo Serikali inapaswa kutoa kwa ajili ya wananchi?”

“Wale ambao tu waajiri, tunawajali wafanyakazi na wahudumu wetu kwa kuwalipa mishahara ya halali? Wale ambao tu wafanya biashara, tunalipa kodi zote kihalali?”

“Wale ambao tumepewa jukumu la kukusanya kodi, ushuru na ada nyingine kama tunafanya hivyo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu husika? Tunaepukaje na kishawishi cha rushwa, hongo, mulungula, magendo au aina yoyote ya ufisadi?”

Kijamii

Katika eneo la kijamii TEC imesema bado kuna kishawishi cha kupingana na azma ya kuboresha maisha ya kijamii.

“Hii inajidhihirisha kwa njia ya uhasama, ugomvi, ukatili kwa watoto na wanawake, ujambazi, na maovu mengine kama hayo miongoni mwa jamii yetu. Kama wamisionari tunaopaswa kuleta habari njema kwa ndugu zetu, kwa nini turuhusu roho ya namna hii ambayo kwa kweli ni roho ya Kaini inayouliza kwa jeuri kabisa,” unasema ujumbe huo.

Mambo matatu

Katika ujumbe wake, Baraza hilo limesema, “Kwa mwaka huu wa 2018 kipindi hiki ni cha kujitafakari mbele ya Mungu na kufanya toba hususan uhai wa amani yetu kwa njia ya matendo ya huruma, haki upendo na amani kwa jirani zetu.”

Limesema hiki ni kipindi chenye upekee wa aina yake kwake sababu ya mambo matatu;

“Ni katika mwaka huu ambapo Kanisa Katoliki Tanzania linaadhimisha na kusherehekea miaka 150 ya Ukatoliki Tanzania Bara, na kilele chake kitakuwa tarehe 2 Oktoba.

Mwaka huu pia utakuwa ni mwaka wa 50 tangu Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania watoe tamko rasmi kuhusu mwelekeo na hatima ya nchi yetu na Mwaka huu ni mwaka wa maandalizi ya utekelezaji wa haki ya msingi ya kidemokrasia ya raia wote ya kuchagua viongozi wa Serikali zetu za mitaa, vijiji na vitongoji hapo mwakani 2019.”

Kwa sababu hizo tatu, TEC imesema, “Ni vyema tafakari yetu ya Kwaresima ikalenga katika swali ambalo, kwa namna moja au nyingine, linahusu sababu hizo tatu. Kwa njia ya swali hilo mwanadamu hudiriki kumhoji na kumuuliza Mungu na Muumba wake kuhusu hali ya binadamu mwenzake. Swali hilo ni Je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” (Mw. 4:9).
 
Back
Top Bottom