inaniwia vigumu sana kuamini kwamba pamoja na yote hayo bado watu hatukubali kuwa CHADEMA kuna tatizo kubwa tena la msingi. Tunaweza kufuta uanachama watu wengi lakini tatizo lililopo lisiposhughulikiwa nina hakikahatutafika mbali. Mh. Tundu Lissu nakuheshimu sana lakini naanza kupata wasiwasi sasa haiwezekani hautaki urais wa kifalme lakini unakumbatia Uenyekiti wa Kifalme, this is insanity.
Napitia waraka huu kila mara sioni tatizo aise ni vita vya kidemokrasia lakini pana tija ya kuijenga chadema kiuchumi zaidi! Kweli elimu ya mjinga ni majungu
huu mtiririko umejaa ushahidi laini na mwepesi sana kiasi hakuna kitu chochote kinachoshikika (tangible). Hauwezi hata kidogo kufananishwa na uzito wa ule ushahidi wa usaliti uliowezeshwa na akaunti za benki zilizo ujerumani..pole ndugu mwandishi lakini sijashawishika na lolote.
waraka umekamatwa kwenye laptop ya mwigamba na amekiri hili tatizo lliko wapi? Kitila na zitto waliitwa wakakubali na kuomba kujiuzulu nyazifa zao, tatizo liko wapi?
Njia ya mwongo haifiki mbali.Chadema sasa wajipange kuwaeleza watanzania na kuusambaza huu waraka pamoja na nyaraka zingine kwa watanzania ili wajionee kazi ovu iliyokuwainafanywa.
Eti Dr.Kitila Mkumbo amewahi kuwa usalama wa Taifa/ccm?
Siasa za ubabe, Chadema walikuwa wanaelekea mahali lakini kwa hili wamejivunja miguu. Mgogoro huu ulikuwa na fursa nzuri kwa chama kama wangeamua kuangalia tatizo liko wapi kuliko kufukiza watu wanaosikilizwa na wananchi