Wasanii wamjia juu Fid Q kwa kufanikisha Steve Nyerere kuwa Msemaji wa Wanamuziki wote Tanzania

Wasanii wamjia juu Fid Q kwa kufanikisha Steve Nyerere kuwa Msemaji wa Wanamuziki wote Tanzania

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
1647556048742.png

Shirikisho la Muziki Nchini Tanzania ambalo Fid Q Ni katibu Mkuu, lilimtangaza Steve Nyerere kuwa Msemaji wa Wanamuziki Wote nchini.

Wasanii wamaupinga huu uteuzi na kudai wanataka Kusemewa na Mtu anaejua Changamoto zao na sio Steve ambae ni Mwanasiasa na Muigizaji.

Wasanii Wameonekana kutokua na imani na Steve kwa kigezo kuwa Haujui Muziki wa Tanzania na nafasi hiyo inamfaa mtu ambae yupo relevant na Muziki,

Wasanii waliopinga ni pamoja na Nay Wa Mitego, Diamond, Wakazi, Adam Mchomvu, Q Chief, Afande Sele, n.k

Imependekezwa Mchakato Urudiwe ili apatikane mtu sahihi wa kuwasemea wanamuziki
 
Binafsi naona msemaji ni bora angekuwa ashawahi kujihusisha na mziki, ingependeza awe Mike tee, Tid, P funk, Master J, lady jay dee, Enika, n.k.

Huyu Steve hapana kwakweli, njaa kali sana hadi ikafika kipindi kila msiba ukitokea anajipa cheo cha kukusanya rambi rambi, pia ni mtu ambae hupenda kutumia watu kama ngazi.
 
Ila Steve jamaa anajua kujipenyeza kutoka kwenye udalali wa wanawake, uuigizaji, uchawa kwa wanasiasa na baadhi ya matajiri mpaka uongozi.

Hako kajamaa kaoneni hivyo ila kana hela kwa sababu ya uchawa.

Nakumbuka 2017 nipo zangu Kawe, nikamuona anapita Prado kali.

Sasa nina mwanangu ni mbongo movie nika mwambia nimemuona Steve na Prado, jamaa akanipa Mkanda mzima.

Akanambia sio Prado ana gorofa analijenga lipo mwisho mwisho kuisha.

Zile chaguzi mbili zilizo mweka madarakani Kikwete, yeye ndiye alikuwa coordinator wa waigizaji wote, mzigo anapewa yy, then yy ndiye anaugawa.

Uchaguzi 2015 alipiga ila sio kivile kwani awamu ile Magu alikuwa hataki shobo, 2020 hajalamba kabisa.

Ila ndio mama kaingia mwamba anarudi tena na uchawa wake.

Steve alikuwa anauwezo wa kummiliki Welu Sengo, demu ana bonge la shepu hapo Steve alimpangishia, akamnunulia usafiri na bado mtoto wake akampeleka shule.

Kajamaa mademu anaotembea nao ni wale walio fungasha hatembei na vimodel.

Kajamaa kaoneni hivyo kanapiga hela kwa issues za uchawa kwawanasiasa na baadhi ya matajiri wanamuamini.

Kwa kifupi Fid Q kazingua jamaa hana quality za uongozi bali kujipendekeza.
 
Tatizo la Steve ni hajui kuongea mbele ya hadhara, mara nyingi hua anaongea kwa kuropoka na kuweka jokes kwenye kila kitu hadi inaboa.

Hapo wangemuweka msanii ambaye anajielewa + kujiamini + aliyekomaa kwenye muziki ambaye anaelewa vema safari ya muziki na changamoto zake.
 
Ni kweli wamekosea

Lakini hao walalamikaji naskia kwenye vikao wakiitwa hawaji, sasa wangekuwepo si wangekuwa na nguvu ya kuchagua mtu wanayemtaka?

Mfano ni huyo diamond hajawahi kwenda anajikuta star sasa analalamika nini?
 
Ni kweli wamekosea
Lakini hao walalamikaji naskia kwenye vikao wakiitwa hawaji sasa wangekuwepo si wangekuwa na nguvu ya kuchagua mtu wanayemtaka?

Mfano ni huyo diamond hajawahi kwenda anajikuta star sasa analalamika nini?
Hata kama hawaendi ndo achaguliwe mtu asie msanii kuwasemea wasanii mzebaba.

Ni kama masemaji wa wachezaji mpira ndo awe huyo steve nyerere, inakuja hiyo mzebaba??
 
Hii nchi hii
Hapo mwamba alichemka kwakweli.
Yaani mtu wa sanaa ya maigizo akawawakilishe watu wa sanaa ya muziki ambao hata hajui changamoto zake?
Huko kwenye muziki watu wameisha?
Afadhali urudiwe tu kwakweli.
 
Labda ni kiki kutangaza shirikisho lao, na kweli wamefanikiwa
 
Msemaji wa Wanamuziki ?

Ni ipi Job Description yake ?, Nadhani wangekuwa na Mtetezi wa Wanamuziki; Msemaji ni individual au management yake as anachosema huyu sio necessarily sauti moja na yule
 
Fid ni mshamba sana watu wengi wanamheshimu kwa zile flow zake ila ukipata nafasi ya kumsikia akiwa anaongea utagundua hana kitu kichwani zaidi ya kutafsili quotation maarufu duniani na kuziweka kwenye mashairi yake, kitendo cha kumteua steve kuwa msemaji wa wanamuziki kinaakisi mentality yake wala sio cha bahati mbaya au ni mkakati
 
Binafsi naona msemaji ni bora angekuwa ashawahi kujihusisha na mziki, ingependeza awe Mike tee, Tid, P funk, Master J, lady jay dee, Enika, n.k.

Huyu Steve hapana kwakweli, njaa kali sana hadi ikafika kipindi kila msiba ukitokea anajipa cheo cha kukusanya rambi rambi, pia ni mtu ambae hupenda kutumia watu kama ngazi.
Huyo wamemweka kwasababu kazi ya uchawa anaiweza atakuwa anawavutia michongo kutoka serikalini na chama tawala.
 
Fid ni mshamba sana watu wengi wanamheshimu kwa zile flow zake ila ukipata nafasi ya kumsikia akiwa anaongea utagundua hana kitu kichwani zaidi ya kutafsili quotation maarufu duniani na kuziweka kwenye mashairi yake, kitendo cha kumteua steve kuwa msemaji wa wanamuziki kinaakisi mentality yake wala sio cha bahati mbaya au ni mkakati
Uwa akiambiwa aeleze mistari yake uwa haeleweki.
Ila napenda flow zake iwe anacopy kwenye vitabu au la, ila ni kipaji cha kuipangilia si haba.
 
Back
Top Bottom