YAANI...Kuna wakati najikuta naamini sana kuwa huyu mama anategemea zaidi Watu/ washauri waamue badala yake kisha wanamuambia tu amua hivi/fanya hivi naye hana jinsi
Kwasababu nikiangalia mfano msimamo wake juu ya tozo wanazolipishwa watanzania kupitia miamala...yeye binafsi hakuliafiki kwasababu alisema litazamwe upya, Mara paaap ni kama limelazimishwa na Mwigulu Nchemba na kupitishwa then mama akakaa kimya kumaanisha amelikubali
Hata Suala la kukamatwa kwa Mbowe ni kama vile mama anakuja kushirikishwa mambo baada ya kufanyika...
LAKINI pia kuna mambo mengine naamini anafanya kwa utashi wake, kwa mfano uteuzi wa hawa watoto / vibinti vya CCM kuteuliwa katika nafasi za Ukuu wa wilaya au Ukurugenzi, hapa naamini hajashauriwa ni ameamua yeye kama yeye kupitisha majina hayo.
Kifupi, yeye kama Rais kuna lawama nyingi anapaswa kuzipokea kutokana na nafasi aliyo nayo.