Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Kuna hii ‘narrative’ inayoendelea sasa hivi kuwa Rais Samia anashauriwa vibaya.
Kila jambo linaloonekana kwenda mrama, lawama wanapewa hao washauri wake!
Yeye hakosei [kwa maneno yake mwenyewe aliwahi kunena kuwa Rais hakosei]. Ikitokea kuonekana kafanya makosa, wapenzi wake wanakimbilia kuwalaumu washauri wake.
Sasa Ngabu anauliza: hao washauri wa Rais Samia ni akina nani hasa?
Majina yao ni nani na nani?
Sura zao zikoje? Jinsia zao ni zipi?
Wana vyeo gani serikalini? Nani aliwafanya wawe washauri wa Samia?
Nataka kuwajua hao washauri wa Samia wanaomshauri vibaya.
Kubwa zaidi, Rais mstaafu Nyerere aliwahi kusema kwenye moja ya hotuba zake, hii nadhani ilikuwa ni ya mwaka 1995 akiwahutubia wafanyakazi huko Mbeya kwenye sherehe ya Mei Mosi, kuwa, mtu mwenye akili, anayejua kwamba na wewe una akili, akikupa mawazo/ ushauri wa kipumbavu na wewe ukaukubali, basi mtu huyo atakudharau kabisa.
Video yake hii hapa. Anzia dakika ya 1:00 mpaka 2:00.
Huyu Rais wetu mpya hana uwezo wa kuchuja ushauri ulio mzuri na ushauri ulio wa kipumbavu?
Mimi napenda kuwa na Rais ambaye yuko ‘engaged’. Sipendi kuwa na Rais anayeshauriwa tu bila ya yeye kuweka input yake.
Je, Rais wetu huyu mpya, yeye ni Rais wa aina gani? Kila anachoshauriwa kufanya yeye anaenda nacho tu?