Washauri wa Rais Samia ni akina nani?

Washauri wa Rais Samia ni akina nani?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Kuna hii ‘narrative’ inayoendelea sasa hivi kuwa Rais Samia anashauriwa vibaya.

Kila jambo linaloonekana kwenda mrama, lawama wanapewa hao washauri wake!

Yeye hakosei [kwa maneno yake mwenyewe aliwahi kunena kuwa Rais hakosei]. Ikitokea kuonekana kafanya makosa, wapenzi wake wanakimbilia kuwalaumu washauri wake.

Sasa Ngabu anauliza: hao washauri wa Rais Samia ni akina nani hasa?

Majina yao ni nani na nani?

Sura zao zikoje? Jinsia zao ni zipi?

Wana vyeo gani serikalini? Nani aliwafanya wawe washauri wa Samia?

Nataka kuwajua hao washauri wa Samia wanaomshauri vibaya.

Kubwa zaidi, Rais mstaafu Nyerere aliwahi kusema kwenye moja ya hotuba zake, hii nadhani ilikuwa ni ya mwaka 1995 akiwahutubia wafanyakazi huko Mbeya kwenye sherehe ya Mei Mosi, kuwa, mtu mwenye akili, anayejua kwamba na wewe una akili, akikupa mawazo/ ushauri wa kipumbavu na wewe ukaukubali, basi mtu huyo atakudharau kabisa.

Video yake hii hapa. Anzia dakika ya 1:00 mpaka 2:00.




Huyu Rais wetu mpya hana uwezo wa kuchuja ushauri ulio mzuri na ushauri ulio wa kipumbavu?

Mimi napenda kuwa na Rais ambaye yuko ‘engaged’. Sipendi kuwa na Rais anayeshauriwa tu bila ya yeye kuweka input yake.

Je, Rais wetu huyu mpya, yeye ni Rais wa aina gani? Kila anachoshauriwa kufanya yeye anaenda nacho tu?
 
Akiletewa ushauri mezani anawaambia "Nendeni mtekeleze hayo mlosema".

Yeye binafsi hawezi kuchakata taarifa na kuzidadavua.

Kwahiyo washauri wake wana exploit sana huo udhaifu wa Bibi-maushungi.
.
IMG_20201018_091547.jpg
 
Na wewe si ndo ulisema siku Jakaya Kikwete atapoachia madaraka utaisherehekea kila mwaka siku hiyo?

Tafuta kioo. Kiangalie. Utachokiona ndo mnafiki.
Huyo alieweka mashehe wa uamsho miaka zaidi ya mitano jela kwanini nisifurahie akitoka madarakani?

Hujui kuwa yeye ni muasisi wa huu uovu wote unaoendelea leo hii?

Halafu acha kuhamisha mada kisa umeumbuka.
 
YAANI...Kuna wakati najikuta naamini sana kuwa huyu mama anategemea zaidi Watu/ washauri waamue badala yake kisha wanamuambia tu amua hivi/fanya hivi naye hana jinsi

Kwasababu nikiangalia mfano msimamo wake juu ya tozo wanazolipishwa watanzania kupitia miamala...yeye binafsi hakuliafiki kwasababu alisema litazamwe upya, Mara paaap ni kama limelazimishwa na Mwigulu Nchemba na kupitishwa then mama akakaa kimya kumaanisha amelikubali

Hata Suala la kukamatwa kwa Mbowe ni kama vile mama anakuja kushirikishwa mambo baada ya kufanyika...

LAKINI pia kuna mambo mengine naamini anafanya kwa utashi wake, kwa mfano uteuzi wa hawa watoto / vibinti vya CCM kuteuliwa katika nafasi za Ukuu wa wilaya au Ukurugenzi, hapa naamini hajashauriwa ni ameamua yeye kama yeye kupitisha majina hayo.

Kifupi, yeye kama Rais kuna lawama nyingi anapaswa kuzipokea kutokana na nafasi aliyo nayo.
 
Huyo alieweka mashehe wa uamsho miaka zaidi ya mitano jela kwanini nisifurahie akitoka madarakani?

Hujui kuwa yeye ni muasisi wa huu uovu wote unaoendelea leo hii?

Halafu acha kuhamisha mada kisa umeumbuka.
Nimeumbuka nini sasa? We jamaa unachekesha sana 🤣
 
Back
Top Bottom