Wataalam wetu wamefikia hatua gani kuhusu kinga ama tiba ya Corona?

Wataalam wetu wamefikia hatua gani kuhusu kinga ama tiba ya Corona?

Ndugu zangu hamjui mambo yanavyoenda.
Hizo complex machines (microscopes) za kumpembua huyo corona mnazo??

Nahisi umefikiri mambo yanaenda kama kuchambua mchele.
 
Tatizo mfumo mzima wa vyuo vikuu na taasisi za tafiti umetupwa na viongozi, hakuna hela ya maana inayowekwa kwa ajili ya utafiti. Mfano tu hapa Tanzania, Leo hii unakuta profesa anafuga nguruwe ama kuuza vitenge ili ajipatie kipato cha ziada unafikiri hata kuwaza kutafuta hiyo tiba anaanzia wapi, sana sana wanasubiria tu uteuzi wawe mawaziri na makatibu wakuu basi ama kukimbilia kwenye ubunge. Unaweza kukuta kwenye timu itakayogundua tiba ya ugonjwa huu kukawa na waafrika lakini waliokimbilia ughaibuni kutafuta maisha.
 
Elimu yetu ya African ni applications tuu na sio innovative
Tunajifunza walicho fanya wazungu na sio kuvumbua vitu vipya,

mfano, (Matindale Extra pharmacopoeia, Pharmaceutical codex, na vitabu viingi tunatumia vya wazungu unategemea dawa tutapata ? Labda ya babu wa loliondo
 
Mimi nadhani sio busara kuwalaumu, research zinahitaji pesa je ni kiasi gani serikali imetenga kwa ajili ya tafiti vyuoni?

Umeita pesa. Me naita investments.
1. Mfumo. Watawala wamewawezesha wataaluma kufanya anayoyataka mtoa mada? Vision ya watawala ina mlengo upi?
2. Ubora wa maabara na vitendea kazi vyake vyote. Maabara zetu zipo equipped?
3. Huyu mtaaluma unavyomtaka kumexpose na huyo corona, unampatia life insurance? Mfumo unasemaje?
4. Mengineyo.

Wataaluma tupo tayari muda wowote kuingia kufanya kazi.
 
Wao wanajua tu kufanya fractional distillation,litmus paper test,how to use bunsen burner,frog dissection etc lkn mambo mengine wao hayawahusu.

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Hata kama wanajua kufanya tafiti,je pesa wanayo?
 
Kama serikali haitoi pesa zipo taasisi na vyuo na makampuni ya nchi za nje hasa Ulaya na America ambayo yako tayari kutoa Funds kwa shughuli za researches, kinachotakiwa ni wewe kupeleka Proposal zako tu.

Maprofesa na wataalamu wetu ni wazuri katika kukariri Paper Works tu, lakini kwenye vitendo na uhalisia ni sufuri tofauti na Maprofesa wa Ulaya na nchi zingine.

Mkuu embu taja hayo mashirika yanayotoa funds kwa research 😊😊😊
 
Wanasayansi wetu wote wanataka kuwa wanasiasa..
Manake hata sayansi Africa hailipi
 
Mimi nina omba angalau waandishi mahiri watakaokuwa wamejikita ktk masuala ya utabibu tu , wamtafute Dr. Louis Shika kwenye interview aongelee masuala ya corona na public health. Maana vyeti vyake alivyotaja na miaka yake ya kufundisha nchini Russia atakuwa ana jambo la kushauri kuhusu siyo tiba, kinga tu bali hata uelekeo wa uvumbuzi.

CV ya Dr. Luis Shika :

Nov 2017
Dr Luis Shika ambae amefunguka na kueeleza elimu yake ya udaktari ambayo amesomea nchini Urusi na kuwa na Degree 4



Source : Muungwana TV
 
Elimu yetu ya African ni applications tuu na sio innovative
Tunajifunza walicho fanya wazungu na sio kuvumbua vitu vipya,

mfano, (Matindale Extra pharmacopoeia, Pharmaceutical codex, na vitabu viingi tunatumia vya wazungu unategemea dawa tutapata ? Labda ya babu wa loliondo
Utafanyaje innovation kama huna fund? utafanyaje innovation kama serikali haikusapoti? unawakumbuka wale walio tengeneza bnduki na ndege waliishia wapi?
 
Ndugu zangu hamjui mambo yanavyoenda.
Hizo complex machines (microscopes) za kumpembua huyo corona mnazo??

Nahisi umefikiri mambo yanaenda kama kuchambua mchele.
Mbona huwa wanaenda hizo nchi zenye machine bora! Huwa wanaenda kufanya nin?
 
I wish watu wangejua na kutuheshimu madaktari

Atleast wangejua hatusomi kugundua vitu sisi

Atleast wapatikane binadamu wachache wenye uelewa

Kwamba kuna muda wewe kuishi au kutokuishi kupo mikononi mwangu

I wish wangetuombea, rafiki yangu daktari kafariki italia nlihuzunika ninawaza na mimi je itakuaje na us ngoma imechangamka hivi

Asante!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Thread humu ilikua inatembea ni yupi lecture bora wako chuoni, wapo wengi walisifiwa mpaka ukawa unazan wanaeza gundua moyo. Kila mmoja anamsifia lecture wake kuwa alikua bora balaa wakati wa ufundishaji, sasa Leo najiuliza wapo wapi hao Madaktari malecture waliokua wanaonekana bora darasani. Wapo wapi wasigundue dawa ya kutibu Vimafua tu mpaka tunakufa. Wameshindwa nini kufanyia kwa vitendo Yale ambayo waliokua mpka wanatoa supp mtu akishindwa. Imagine unakumbuka ticha alikufelisha kisa umesaau meaning of virus na characteristics zake lkn ticha huyo huyo mpaka Leo nae anajifungia ndani anaogopa eti virus ni ajabu. Hebu mtag Profesa au lecture ambae alikua anajifanya anaijua topic ya Virus lkn Leo kajifungia ndani kisa mafua.

Sent using Jamii Forums mobile app
LOooh, mkuu'Shark' umetoa mada ya kichokozi kweli!

Unakumbuka hadi 'suppl' wakati huu?

Kuna sababu nyingi mkuu zinazowakwamisha hawa maticha wetu, nyingi ya hizo zikiwa nje ya uwezo wao kabisa, na nyingine zikihusiana na mazingira tu wanamofanyia kazi.

Kwa mfano nikupe huu wa siasa zetu zinazolipa kushinda jambo jingine lolote kwa hapa kwetu Tanzania.
Chukulia maprofesa wangapi, bila kuhesabu wenye fani zao zisizokuwa za sayansi, walivutwa kutoka kwenye fani hizo mhimu walizosomea na kujitumbukiza kwenye siasa!

Na wanapotumbukia huko, huku nyuma walipotoka hawapakumbuki tena kupapigania ili pawe na mazingira ya kuwezesha wenzao waliobaki huko.
Sio siasa tu. Profesa anaamua ajishughulishe na ufugaji wa ng'ombe, kuku wa mayai. Jana nzima kuku walikuwa wakifa "kifo cha nusu nusu" (hii niliipata kwa wataalam humu JF), unadhani profesa huyo anahabari tena na kutafiti chochote?

Yapo mengi sana ya kutolea "visingizio" kwa nini maticha wetu wapo wapo tu!

Lakini nirudi nyuma kidogo.
Tukiachia mazingira yao yasiyoruhusu kuonyesha uimara wa uwzo walionao katika nyanja zao, imani yangu kubwa ni kuwa wataalam tunao wengi kabisa wa kutosha hapa nchini, kama wakipewa CHANGAMOTO (kichocheo) na kupata uongozi mzuri wa kusimamia juhudi zao.

Ninayo imani kabisa, tulipofikia kama nchi, Tanzania sasa inao uwezo wa kufanya mambo mengi sana mhimu ya kupunguza changamoto tulizonazo kwa kuwategemea wataalam wetu sisi wenyewe.

India na Pakistan hawakwenda kutafutiza wataalam toka nje kwenda kuwajengea mabomu yao ya nuklia, hata kabla ya kutimiza miaka 30 baada ya uhuru wao.

Nchi zao ziliamua kwamba kwa usalama wao katika eneo lile, walihitaji kuwa na uwezo wa kuwa na silaha hiyo. Wataalam wao wakapewa changamoto (challenge) na wakatimiza.

Leo hii bado sisi tunalialia na changamoto nyiingi tu, tena nyingine ndogondogo kabisa, tukitafuta tuje tusaidiwe, huku wataalam wetu tuliowaandaa sisi wenyewe wakishindia kwenye vijiwe - mfano mzuri kwa hili ni wahitimu wa Sokoine University.

Kila mwaka wanahitimu wangapi, kwenye fani mbali mbali kama za ufugaji - hadi leo hii hata kiasi cha maziwa tunayozalisha sisi haifikii nusu ya yale yanayozalishwa na jirani zetu hapo kaskazini, na inatubidi tuuziwe maziwa!
Jiulize mwenyewe - hawa watu wamesoma, hata msaada wa kutuwezesha kufuga kuku wa kisasa kwa ufanisi, kweli hawana?

Naweza kuandika gazeti hapa na kutoka nje kabisa ya Coronavirus.

Ukimwangalia coronavirus alivyokaa (hata picha hatuwezi kumpiga, kwa sababu darubini hatuna, sasa tutamsoma vipi - lifikirie hilo pia) - nilishaweka challenge humu nikitamani niwe mwalimu mahala, niwaambie vijana wangu, wanavyomwona yule coronavirus,alivyo umbwa, wangeanzia wapi kumshambulia? Ile mikia yake haiwezi kudhurika?
Acha hiyo - kwa nini tusiangalie anapoingilia kumshambulia binaadam, puani au mdomoni, ndio njia kuu - hawa vijana wangu hawawezi wakapendekeza tuweke kinga puani? Mbona kila leo wataalam wa madawa wanaelekeza wagonjwa fulani fulani kuweka matone puani, mara kadhaa kwa siku, ili haya matone yawe na dawa za kumshambulia au kumzuia asikanyage na kujiimarisha kwenye cell ambazo ndizo anapoanzia kushambulia na kuingia na kusambaa sehemu mbalimbali?

Hawa vijana wangu, tena wenye akili zinazochacha kabisa, wakisubilia kuongozwa tu na mwalimu makini, hata wasiweze kubuni njia za kuondoa haraka zile 'aerosols' tunazoambiwa kuwa ndio njia kuu ya kusambazwa kwa coronavirus, mara tu mtu aliyeathirika anapopiga chafya, ili aerosol hizi zisivutwe ndani na watu waliopo karibu naye?

Sitaaandika chochote njia nyingi zinazowezekana kuzuia uharibifu mwilini akishaingia kwenye cell anazozishambulia.

Mkuu 'shark', imani yangu kubwa ni kuwa maticha wetu uwezo wanao kabisa, ila mzingira yanawaangusha. Sio mazingira ya maslahi tu, bali ni kukosekana kwa uongozi unaohitajika kusimamia, kuweka mkazo katika maeneo ambayo taifa letu lingeyatambua kuwa ni maeneo wanayotaka kuyafanyia kazi mahususi.

Eneo moja ni lile la utengenezaji madawa na viwanda vya kutengeneza dawa.


Leo hii Rais Magufuli akisimama na kutamka kwamba anaweka dharura, kwamba Tanzania ni lazima iwe na uwezo wa kujitosheleza katika eneo hilo, nina hakika kabisa kwamba katika miaka mitano hadi kumi hilo linawezekana kabisa.

Anaweza hata akaamuru aweke kama kambi za kijeshi na kuwaweka wataalam husika na kuwapa hiyo changamoto na kuisimamia, kwa nini isiwezekane, na hilo ndilo likawa bomu letu la nuklia, na yeye tukamkumbuka kwa kazi hiyo kwenye historia ya nchi yetu.

LOoo, sijui kama bado nina wewe mkuu wangu 'shark'.

Sikuhariri popote. Kunradhi kama kuna makosa, maanake nilitiririka tu bila breki!
 
Mkuu embu taja hayo mashirika yanayotoa funds kwa research 😊😊😊


Chukua mfano wa HIV au Malaria, kama unayo propasal yako ya kutafuta chanjo ya HiV au Malaria,--- tafuta njia yoyote na tangaza hiyo propasal wala hapo huna haja ya kutafuta wafadhili nk, kwani Wao wenyewe watakutafuta ili kukuhoji na wakiridhika na mahojiano basi watakufadhili tu. Shida ni hii kwamba Ma intellectuals wetu wapo in deep slumber, hawana utamaduni wa kufanya researches wao wanasubiri researches zifanywe na Wazungu na wao Wacrame kwa ajili ya kufundishia na kuwa disco Wanafunzi na kugawa degree cha "Chupi."🤣
 
Back
Top Bottom