Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,988
- 30,183
Ubarikiwe sana mkuu wangu aseee naona umemaliza kabisa mpk kwa wale wa Kilimo teh teh teh kama ulivyosema nmeleta hii as a challenge tujipime tunakwama wapi mbn kipindi hiki cha Magufuli ndo kipindi cha uthubutu wajaribu wataweza. Wapo wanaoona kuwa tunawadhalilisha kama Baba Swalehe naomba anisamehe wala sina maana hiyoLOooh, mkuu'Shark' umetoa mada ya kichokozi kweli!
Unakumbuka hadi 'suppl' wakati huu?
Kuna sababu nyingi mkuu zinazowakwamisha hawa maticha wetu, nyingi ya hizo zikiwa nje ya uwezo wao kabisa, na nyingine zikihusiana na mazingira tu wanamofanyia kazi.
Kwa mfano nikupe huu wa siasa zetu zinazolipa kushinda jambo jingine lolote kwa hapa kwetu Tanzania.
Chukulia maprofesa wangapi, bila kuhesabu wenye fani zao zisizokuwa za sayansi, walivutwa kutoka kwenye fani hizo mhimu walizosomea na kujitumbukiza kwenye siasa!
Na wanapotumbukia huko, huku nyuma walipotoka hawapakumbuki tena kupapigania ili pawe na mazingira ya kuwezesha wenzao waliobaki huko.
Sio siasa tu. Profesa anaamua ajishughulishe na ufugaji wa ng'ombe, kuku wa mayai. Jana nzima kuku walikuwa wakifa "kifo cha nusu nusu" (hii niliipata kwa wataalam humu JF), unadhani profesa huyo anahabari tena na kutafiti chochote?
Yapo mengi sana ya kutolea "visingizio" kwa nini maticha wetu wapo wapo tu!
Lakini nirudi nyuma kidogo.
Tukiachia mazingira yao yasiyoruhusu kuonyesha uimara wa uwzo walionao katika nyanja zao, imani yangu kubwa ni kuwa wataalam tunao wengi kabisa wa kutosha hapa nchini, kama wakipewa CHANGAMOTO (kichocheo) na kupata uongozi mzuri wa kusimamia juhudi zao.
Ninayo imani kabisa, tulipofikia kama nchi, Tanzania sasa inao uwezo wa kufanya mambo mengi sana mhimu ya kupunguza changamoto tulizonazo kwa kuwategemea wataalam wetu sisi wenyewe.
India na Pakistan hawakwenda kutafutiza wataalam toka nje kwenda kuwajengea mabomu yao ya nuklia, hata kabla ya kutimiza miaka 30 baada ya uhuru wao.
Nchi zao ziliamua kwamba kwa usalama wao katika eneo lile, walihitaji kuwa na uwezo wa kuwa na silaha hiyo. Wataalam wao wakapewa changamoto (challenge) na wakatimiza.
Leo hii bado sisi tunalialia na changamoto nyiingi tu, tena nyingine ndogondogo kabisa, tukitafuta tuje tusaidiwe, huku wataalam wetu tuliowaandaa sisi wenyewe wakishindia kwenye vijiwe - mfano mzuri kwa hili ni wahitimu wa Sokoine University.
Kila mwaka wanahitimu wangapi, kwenye fani mbali mbali kama za ufugaji - hadi leo hii hata kiasi cha maziwa tunayozalisha sisi haifikii nusu ya yale yanayozalishwa na jirani zetu hapo kaskazini, na inatubidi tuuziwe maziwa!
Jiulize mwenyewe - hawa watu wamesoma, hata msaada wa kutuwezesha kufuga kuku wa kisasa kwa ufanisi, kweli hawana?
Naweza kuandika gazeti hapa na kutoka nje kabisa ya Coronavirus.
Ukimwangalia coronavirus alivyokaa (hata picha hatuwezi kumpiga, kwa sababu darubini hatuna, sasa tutamsoma vipi - lifikirie hilo pia) - nilishaweka challenge humu nikitamani niwe mwalimu mahala, niwaambie vijana wangu, wanavyomwona yule coronavirus,alivyo umbwa, wangeanzia wapi kumshambulia? Ile mikia yake haiwezi kudhurika?
Acha hiyo - kwa nini tusiangalie anapoingilia kumshambulia binaadam, puani au mdomoni, ndio njia kuu - hawa vijana wangu hawawezi wakapendekeza tuweke kinga puani? Mbona kila leo wataalam wa madawa wanaelekeza wagonjwa fulani fulani kuweka matone puani, mara kadhaa kwa siku, ili haya matone yawe na dawa za kumshambulia au kumzuia asikanyage na kujiimarisha kwenye cell ambazo ndizo anapoanzia kushambulia na kuingia na kusambaa sehemu mbalimbali?
Hawa vijana wangu, tena wenye akili zinazochacha kabisa, wakisubilia kuongozwa tu na mwalimu makini, hata wasiweze kubuni njia za kuondoa haraka zile 'aerosols' tunazoambiwa kuwa ndio njia kuu ya kusambazwa kwa coronavirus, mara tu mtu aliyeathirika anapopiga chafya, ili aerosol hizi zisivutwe ndani na watu waliopo karibu naye?
Sitaaandika chochote njia nyingi zinazowezekana kuzuia uharibifu mwilini akishaingia kwenye cell anazozishambulia.
Mkuu 'shark', imani yangu kubwa ni kuwa maticha wetu uwezo wanao kabisa, ila mzingira yanawaangusha. Sio mazingira ya maslahi tu, bali ni kukosekana kwa uongozi unaohitajika kusimamia, kuweka mkazo katika maeneo ambayo taifa letu lingeyatambua kuwa ni maeneo wanayotaka kuyafanyia kazi mahususi.
Eneo moja ni lile la utengenezaji madawa na viwanda vya kutengeneza dawa.
Leo hii Rais Magufuli akisimama na kutamka kwamba anaweka dharura, kwamba Tanzania ni lazima iwe na uwezo wa kujitosheleza katika eneo hilo, nina hakika kabisa kwamba katika miaka mitano hadi kumi hilo linawezekana kabisa.
Anaweza hata akaamuru aweke kama kambi za kijeshi na kuwaweka wataalam husika na kuwapa hiyo changamoto na kuisimamia, kwa nini isiwezekane, na hilo ndilo likawa bomu letu la nuklia, na yeye tukamkumbuka kwa kazi hiyo kwenye historia ya nchi yetu.
LOoo, sijui kama bado nina wewe mkuu wangu 'shark'.
Sikuhariri popote. Kunradhi kama kuna makosa, maanake nilitiririka tu bila breki!
Sent using Jamii Forums mobile app