KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,181
- 17,187
Mkuu 'Mokaze' umejitututmua sana katika uandishi hapa. Pole sana kama umejihisi nimekukwaza, lakini elewa kwamba elimu yangu sio kiduchu hata kidogo, na siwezi kukuficha hili..Hivi wewe ni mshenzi wa wapi usiyeweza kuandika bila expletive language??!!---- you idiot blind fool.
Subject matter ni; jinsi gani wanataaluma wa kiafrika wanavyojihusisha na utafutaji wa dawa na chanjo za magonjwa mbalimbali na hususan yale magonjwa yanayotusibu sisi waafrika mfano Ebola, kazi hiyo tumewaachia Wazungu au Waasia tu, wataalamu wetu hawana uthubutu, hiyo ndiyo ilikuwa mada, wewe ukaleta hoja kwamba Antibodies zimeweza kupatikana, mimi nikakuambia that is not an issue kwasababu Antibodies zinaweza kupatikana kwenye Serum ya mtu yeyote aliyepona Covid -19 na Wachina wanatumia njia hiyo na wanadai imeweza kuokoa maisha ya wagonjwa waliokuwa kwenye acute stage, swali (mada) ni hili; ni wanasayansi gani wa kiafrika wapo involved katika kazi ya Isolation ya hizo antibodies ili zitumike kuwatibu wagonjwa wa Covid -19 huku kwetu Afrika??!!, for the disease is a pandemic,, ni wataalamu gani wa kiafrika wanafanya tafiti ama za kupata Vaccines (innoculation) kwa magonjwa kama Ebola inayolipuka mara kwa mara huku Africa??--- badala ya kujikita kwenye Subject matter wewe unakuja kujionyesha (kujimwambafai) kwamba ni mtaalamu wa mambo ya magonjwa na huku ukinitusi !!!, hiyo ndiyo tabia ya kiafrika ya majivuno na kujiona baada ya kupata " elimu" kiduchu!!!, wewe bado hujaelimika na utakuwa mjinga kujiona umeelimika kwani duniani hayupo aliyeelimika na hatotokea.
Huo mstari wako wa kwanza haunipi shida hata kidogo, kwa hiyo unaweza kuendelea kutumia hiyo lugha bila kuniathiri chochote kama ulivyoathirika mwenyewe.
'Subject matter naielewa na kuiheshimu, ndio maana nikakujibu hayo mengine yaliyofuata.
Kama antibodies zidi ya coronavirus wameweza kuzitambua wachina na kuzitumia, wewe kazi hiyo huitambui kwamba ni juhudi mojawapo zidi ya coronavirus? Ndiyo, antibodies zinaweza kupatikana kwa mtu yeyote aliyewahi kushambuliwa na virus hao, lakini si pia kuna kazi ya kutambua na ku'isolate' ili iweze kutumika, hata kama ni ndani ya hiyo plasma?
Kitu nilichokuona kwamba unaonyesha 'ukilaza' ammbalo ndilo tatizo lililokuvuruga akili ni kutojua kwamba hata hiyo kazi iliyofanywa na wachina ni sehemu ya juhudi, sio lazima iwe tu kutafuta vaccine unayoililia wewe.
Swala la wataalam wa kiafrika, hapa ndipo unapokosa uelewa kabisa na kubaki kulaumu tu kwa nini huoni wakijishughulisha na maswala uya ugunduzi, hasa katika magonjwa yanayoanzia na kushambulia eneo lao.
Kwanza hujui kwamba ni Afrika nzima hakuna juhudi hizo, kwa hiyo kutoa tu msimamo kama huo unakuonyesha kuwa na upungufu wa ufahamu.
Lakini mhimu zaidi, kabla hujalalamikia hawa wataalam wa kiafrika, kwa nini usiangalie mambo yanayowakwamisha, yanayozuia wasiifanye kazi kama hiyo? Kwa nini uwe mwepesi tu wa kutoa lawama bila ya kujiridhisha na mazingira wanamofanyia kazi zao!
Ndio, kuna baadhi kati yao hata uwape kila kitu cha kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi, bado kazi haitafanyika. Lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kutoa 'decleration' tu ya lawama kwa kundi zima.