Ni wakati umefika kwa Wanasayansi wa Tanzania kuweza kutatua changamoto za Ugonjwa wa COVID-19.
Nchi nyingi za Africa zinakabiliwa na changamoto za Kuwa na Medical ventilators za kutosha kusaidia Wagonjwa wa CORONA. mashine hizi ni ghali sana!! Ila ni wakati wa Wasomi Wanasayansi wa kizazi cha sasa kuweza kubuni na kutengeneza mashine hizi.
Ni wakati Wasomi- Wanasayansi Wa Tanzania wanaweza kuionesha jamii jinsi gani Wanasayansi wanapaswa kuheshimiwa katika jamii.
Jamii yetu kwa miaka ya hivi karibuni imeanza kudharau wasomi hasa hiki kizazi cha dijitali kusema haina maana ya kusoma kwa kuwa kusoma ni kupoteza muda. Naamini vyuo vya UDSM, DIT, Mbeya University, Nelson Mandela University, Arusha Technical College, NIT, IFM, MUHAS, UDOM, Bugando University of Health Allied Science, VETA, IFAKARA Institute of Health Research, UCLASS, SUA mtasugua vichwa ili kuja suluhu ya kupunguza makali ya Ugonjwa wa COVID-19!! hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
" Ni wakati dunia imesimama ikiwategemea Wanasayansi kuja na Suluhu ya Ugonjwa wa COVID-19, Wanasayansi wa Tanzania mnaweza!!!
View attachment 1416436