HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Baada ya hiyo comment ulimuacha tu hivyo?
 
Pole sana Yani n hatari
 
Wakuu wa taasisi kama hataki anakataa kwenye vacancy maombi hayaendi mbele
 
Wakuu wa taasisi kama hataki anakataa kwenye vacancy maombi hayaendi mbele
Inawezekana hujaelewa mada, issue sio kutaa au kukubali. Issue ni kwamba amekubali sawa ila comment yake iko vipi..? Unajua comment ni muhimu sana kule Utumishi. Boss anaweza kukupitishia vizuri lakini akawa ameweka comment ya kukusagia kunguni. Kumbuka comment ya Boss wako huwezi kuiona kwenye mfumo, utaona kuwa amepitisha tu
 
Naomba kuuliza, sijathibitishwa kazn bado lkn nataka kuhama, nikienda utumishi Dodoma watanisikiliza hoja zangu? Au najisumbua au nianzie tamisemi? Nipo Arusha nataka kwenda pwani mwalimu mathematics
 
Mkuu wako

Hana Mamlaka ya kukataa yeye anashauri halafu anapitisha
Hii ndio ukwel mkuu wa taasisi hana huwezo wa kukataa maombi yasiende utumishi, yeye kazi yake ni kuandika comment tu. Kwa sababu maombi huwa yaenda kwa katibu mkuu, so katibu mkuu anafanyia kazi kutokana na comment za mwajiri wako... mwaka juzi wakati bado hard copy kuna mtu akiandikiwa bado tunamuhitaji, so katibu mkuu alifanya maamuz kutokana na comment hiyo, kwa hiyo hata ambao mnakataliwa kuba comment unaweza kutwa imeandikwa ingawa wewe huoni, ila utumishi wako fair sana
 
Naomba kuuliza, sijathibitishwa kazn bado lkn nataka kuhama, nikienda utumishi Dodoma watanisikiliza hoja zangu? Au najisumbua au nianzie tamisemi? Nipo Arusha nataka kwenda pwani mwalimu mathematics
Kaka wewe kua na utulivu tu, nje ya hapo tafuta connection ya kueleweka
 
Wakuu wa taasisi kama hataki anakataa kwenye vacancy maombi hayaendi mbele
Umeandika nini na mimi nimeandika nini? Mkuu wa taasisi akikataa kwako inakuja rejected na ujumbe kwamba not recommended! Na ombi halifiki kwake bila kupita kwanza kwa HR!
 
Nafikiri huenda hii ikawa ndio sababu, niliiwaza pia. Japo niliwapigia simu utumishi wakasema kitu kikubwa wanachoangalia wao hasa ni ikama.

Kwa namna hii ndio maana watu wanahama kiharamia au kuacha kazi.
Hapo kwenye ikama ndo uchawi ulipo!! Ikama huangaliwa unapotoka sio unapokwenda!
Boss wako ni lazima athibitishe kuwa pengo lako lina mbadala ili ukiondoka asijeenda omba kibali utumishi kuajiri mtu wa kada yako!!

Ndo yale unaona mtu kaputishiwa anakoenda lkn utumishi wanamliga chini!

Ndo maana mnaona halmashauri za mijini kwenye watumishi wengi hasa walimu wa sanaa kuchomoka ni rahisi sana! Taasisi zenye changamoto kuchomoka ni mbinde maana katibu mkuu akikupa kibali ni lazima ajiridhishe ikama inakaaje!!
 
Hii nakubali Mkuu, Ikama inafuatiliwa sana.. maana unaweza kuta Afisa wa kada X anaomba kuhama kwenda taasisi fulani lakini taasisi hiyohiyo aliyopo ina uhitaji au ina nafasi za kupokea watu wa kada hiyo X.
Sasa kwa mantiki hii UTUMISHI ndio huwa wanashikilia bomba
 
Kabisa! Nimeandika haya kama mzoefu niliyekaa kwenye utumishi! Mwajiri wako ana sauti kubwa sana kwenye maamuzi ya uhamisho wako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…