Watajeni wote waliotekwa au kuuawa Enzi Nyerere akiwa Rais

Watajeni wote waliotekwa au kuuawa Enzi Nyerere akiwa Rais

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,982
Reaction score
51,157
Mara kadhaa nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakisema kuwa enzi za Mwalimu Nyerere akiwa Rais watu "wengi" Sana waliuawa au kupotezwa.

Sasa kabla ya waliofanya kazi na Nyerere wote kufa, ni Bora watu wanaowafahamu waliouawa zama Julius Nyerere alipokuwa Rais wa nchi yetu, wawataje watu hao walikuwa ni kina nani?
 
Huyo warioba anayepiga kelele sasa hivi,akiwa waziri mkuu kuna dogo wa udsm alitekwa akapelekwa huko bandarini,akishikikiwa na njemba zimeshiba zimeenda juu na madevu, warioba akaenda huko mafichoni kumtisha dogo
Kama unadhani hayo hawakujifunza kwa mtangulizi wao,pole
 
Ilikuwaje?
Screenshot_20241128-222219~2.jpg
 
Sasa hapo unanipa
Aliyemuua karume aliapa kumuua karume akiwa kozi jeshini ulaya,mara nyingi tu alisikika,huko ulaya mashariki wakamtaarifu nyerere, dingi kama hakusikia
Siku karume anauawa alipanga jioni kuzungumza na wazanzibar so wakae mkao wa kula, ilikua atangaze kuitoa zenji kwenye muungano
 
Karume,titi Mohammed, Hassan bin amir, abdallah fundikira(alikimbilia Mombasa)teddy kaselabantu,kasanga tumbo, yule mbaya aliyeandika the dark side of nyerere na nyerere,a saint or untarnished tyranny orodha ni ndefu
Hao walitekwa au kuuawa... Ni kweli maisha yao yote waliishi nje ya Tanzania kuogopa kuuawa ama kukamatwa?

Kati ya hao uliowaandika ni yupi aliwahi kusema kuwa Nyerere anataka kumuua.
 
Aliyemuua karume aliapa kumuua karume akiwa kozi jeshini ulaya,mara nyingi tu alisikika,huko ulaya mashariki wakamtaarifu nyerere, dingi kama hakusikia
Siku karume anauawa alipanga jioni kuzungumza na wazanzibar so wakae mkao wa kula, ilikua atangaze kuitoa zenji kwenye muungano
Kwani Karume jioni aliyouawa alikuwa wapi. Ili tuweze kuhusisha na hiyo hoja yako ya kuwa karume alikuwa atangaze kuitoa Zanzibar kwenye Muungano.
 
Mara kadhaa nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakisema kuwa enzi za Mwalimu Nyerere akiwa Rais watu "wengi" Sana waliuawa au kupotezwa.

Sasa kabla ya waliofanya kazi na Nyerere wote kufa, ni Bora watu wanaowafahamu waliouawa zama Julius Nyerere alipokuwa Rais wa nchi yetu, wawataje watu hao walikuwa ni kina nani?
Nyerere kuna watu wengi kawafunga kwa sheria dhalimu za indefinite detention.

Wengine kawafungia vijiji fulani kutoka mpaka kwa kibali maalum.

Kina Balozi Christopher Kassanga Tumbo, Joseph Kassela Bantu, Chief David Kidaha Makwaia, walikuwa wengi sana hawa.

Kuna jamaa alikwenda likizo Tanzania miaka ya tisini, akaenda Kagera kuna kijiji alikuwapo mzee mmoja kafungiwa hivyo. Sasa jamaa akawa anataka kwenda na yule mzee mjini.

Yule mzee akamwambia hawezi kwenda mjini mpaka apate kibali maalum.

Hapo ni karibu miaaka 20 baada ya Nyerere kutoka urais, huyu mzee alikuwa bado anaogopa kutoka kijijini bila kibali. Ikabidi yule mgeni amwambie Nyerere si rais na hakuna atakayekufanya kitu. Wakaenda mjini.

Kwenye kuua Nyerere hakuua sana kiasi cha cases kuwa nyingi zinazojulikana. Hakuhitaji kuua hivyo kwa sababu watu wengi walimuheshimu na kumuogopa.

In fact Nyerere hata wafungwa waliohukumiwa kunyongwa alitia saini wawili tu wanyongwe, yule mkulima Mwakindi aliyemuua Dr. Kleruu, na mtu mmoja tu mwingine nimemsahau.
 
Back
Top Bottom