Watajeni wote waliotekwa au kuuawa Enzi Nyerere akiwa Rais

Watajeni wote waliotekwa au kuuawa Enzi Nyerere akiwa Rais

Nyerere kuna watu wengi kawafunga kwa sheria dhalimu za indefinite detention.

Wengine kawafungia vijiji fulani kutoka mpaka kwa kibali maalum.

Kina Balozi Christopher Kassanga Tumbo, Joseph Kassela Bantu, Chief David Kidaha Makwaia, walikuwa wengi sana hawa.

Kuna jamaa alikwenda likizo Tanzania miaka ya tisini, akaenda Kagera kuna kijiji alikuwapo mzee mmoja kafungiwa hivyo. Sasa jamaa akawa anataka kwenda na yule mzee mjini.

Yule mzee akamwambia hawezi kwenda mjini mpaka apate kibali maalum.

Hapo ni karibu miaaka 20 baada ya Nyerere kutoka urais, huyu mzee alikuwa bado anaogopa kutoka kijijini bila kibali. Ikabidi yule mgeni amwambie Nyerere si rais na hakuna atakayekufanya kitu. Wakaenda mjini.

Kwenye kuua Nyerere hakuua sana kiasi cha cases kuwa nyingi zinazojulikana. Hakuhitaji kuua hivyo kwa sababu watu wengi walimuheshimu na kumuogopa.

In fact Nyerere hata wafungwa waliohukumiwa kunyongwa alitia saini wawili tu wanyongwe, yule mkulima Mwakindi aliyemuua Dr. Kleruu, na mtu mmoja tu mwingine nimemsahau.
Kuhusu kunyonga wawili tu si kweli,na hili linathubitishwa na yule mzee aliyekua mnyongaji mstaafu Dodoma aliyefanyiwa mahojiano na mwananchi,huyu mzee alianza kunyonga tangu nyerere akiwa madarakani na alisema kanyonga wengi tu
Siku za mwanzo kunyonga watu walikua wakimtokea ndotoni mpaka alipofanyiwa mambo na wazee wake
Tabora kuna story ya mtu kunyongwa na kutokufa,ikabidi mnyongaji ampopotoe shingo
Mnyongaji akawa mwendawazimu wa kudumu
Hizi story za nyerere kunyonga wawili tu ni za kutaka kum-potray kama mtakatifu
 
Kuna jamaa alikwenda likizo Tanzania miaka ya tisini, akaenda Kagera kuna kijiji alikuwapo mzee mmoja kafungiwa hivyo.
Inawezekana kulikuwa na hiyo Sheria ya "Indefinite detention". Umetaja watu kadhaa hapo juu, lakini ilipofika kuelezea kwa kina unatoa mfano wa Mzee asiye na jina wa huko Kagera.

Kwa mtazamo wangu huyo Mzee asiye na jina haikufaa kutolea mfano hoja zako.
 
Nyerere alikuwa na njia tatu
Detention
Au kukuondoa nchini
Au kukuteka na kukuua

Mambo haya yamekoma na kuisha wakati wa Mwinyi , JK na SSH
 
Nyerere kuna watu wengi kawafunga kwa sheria dhalimu za indefinite detention.

Wengine kawafungia vijiji fulani kutoka mpaka kwa kibali maalum.

Kina Balozi Christopher Kassanga Tumbo, Joseph Kassela Bantu, Chief David Kidaha Makwaia, walikuwa wengi sana hawa.

Kuna jamaa alikwenda likizo Tanzania miaka ya tisini, akaenda Kagera kuna kijiji alikuwapo mzee mmoja kafungiwa hivyo. Sasa jamaa akawa anataka kwenda na yule mzee mjini.

Yule mzee akamwambia hawezi kwenda mjini mpaka apate kibali maalum.

Hapo ni karibu miaaka 20 baada ya Nyerere kutoka urais, huyu mzee alikuwa bado anaogopa kutoka kijijini bila kibali. Ikabidi yule mgeni amwambie Nyerere si rais na hakuna atakayekufanya kitu. Wakaenda mjini.

Kwenye kuua Nyerere hakuua sana kiasi cha cases kuwa nyingi zinazojulikana. Hakuhitaji kuua hivyo kwa sababu watu wengi walimuheshimu na kumuogopa.

In fact Nyerere hata wafungwa waliohukumiwa kunyongwa alitia saini wawili tu wanyongwe, yule mkulima Mwakindi aliyemuua Dr. Kleruu, na mtu mmoja tu mwingine nimemsahau.
Kwa nini watu wengi walimuheshimu na kumuogopa Nyerere tofauti na wengine waliomfuatia?
 
Inawezekana kulikuwa na hiyo Sheria ya "Indefinite detention". Umetaja watu kadhaa hapo juu, lakini ilipofika kuelezea kwa kina unatoa mfano wa Mzee asiye na jina wa huko Kagera.

Kwa mtazamo wangu huyo Mzee asiye na jina haikufaa kutolea mfano hoja zako.
Kwa nini?
 
Kwa nini?
Nadhani jambo likiwepo/tokea huwa kunakuwa na nadharia njama (Conspiracy theories) kadhaa kulihusu.

Kwa mfano kwetu sisi watu wa Nyanda za juu kusini Kuna kisa cha Tuntemeke Sanga kuwekwa kizuizini.

Kwa ivo mada kama hii kunyumbulishwa kwake majina ya wahusika ni kitu muhimu sana.
 
Mara ya mwisho kuonekana ilikua tanganyika akichambwa na nyerere kwenye mkutano wa hadhara,tuamini vipi aliuawa na karume?
Huo mkutano ulifanyikia wapi na maneno gani Nyerere alisema dhidi ya Hanga.

Wakosoaji wengi wa Mwalimu waliishi maisha yao hata uhai wao ulipotamatika!!
 
Nyerere hakuwa na upuuzi wa kuua, kuteka na kupoteza watu.
Haya mambo yalianza enzi za Mkwere.
Enzi za Nyerere walioenda kinyume naye walikuwa wanapigwa exile tu mf TUNTEMEKE Sanga , Aboud Jumbe , Kambona ,tofauti na sasa ukienda kinyume na mtawala unatekwa na kufungwa juu ,unawekewa sumu,unapotezwa ,unanyimwa ulaji na kuambiwa staafu.
 
Kwa nini watu wengi walimuheshimu na kumuogopa Nyerere tofauti na wengine waliomfuatia?

Nyerere alikuwa groomed kuongoza watu, alisoma na yeye mwenyewe alipenda kuwa "philosopher king". Kiongozi mwenye busara. How much he achieved that is debatable, lakini ukimsikiliza, ukiangalia vitabu alivyosoma na hata kutafsiri, the latest being Plato's "Republic", unamuona huyu bwana angalau anamsoma Plato.

Sasa Kikwete Magufuli na Samia wamemsoma Plato?

Nyerere alianza kuongoza watu tangu enzi za ukoloni akipita nchi nzima kuwaeleza jambo ambalo wengi hawakufikiri linawezekana, kudai uhuru.

Kwa hivyo Nyerere aliheshimika kama kiongozi aliyesaidia Watanganyika kupata uhuru.

Na wakati anaanza kuongoza nchi, kulikuwa hakuna watu wengi, kama milioni 9-10 tu. Ni kama Greater Dar es salaam tu kwa sasa.

Kwa hivyo alivyoachiwa nchi na wakoloni, nchi haikuwa comolex sana, aliweza kui shape vizuri alivyotaka yeye, na hata alipopata changamoto, ali deal nazo na kujifunza mapema (1964 Tanganyika mutiny, the Citizenship Act, labour strikes , internal dissent, geopolitics, etc).

Long story short Nyerere alichukua nchi tangu mwanzo, nchi ilikuwa simpke, alijua na kiasi fulani kujali hali ya Watanzania. Nchi haikuwa na complexity kama sasa hakukuwa na TV, hakukuwa na mtandao, magazeti karibu yote yalikuwa ya chama na serikali, wasomi walikuwa wachache, Watanzania waliosafiri walikuwa wachache.

Kadiri siku zilivyoenda ndivyo yote hayo yalibadilika.

Mwinyi kaingia kuwa rais tushaanza kumuangalia Michael Jackson na Harrison Ford kwenye TV. By 1989 tushaona Tiananmen Square na Perestroika. Watanzania wametoka kuwa nchi ya watu milioni 9 -10 mpaka sasa milioni 70.

Tumeongeza idadi ya watu mara 7 tangu uhuru.

Huwezi kutegemea nchi iwe vilevike viongozi waweze kui control kirahisi.

Hususana kama weledi wa viongozi unazidi kupungua.

Kadiri tulivyoendelea ndivyo viongozi walivyozidi kukosa grooming, wakati kiukweli ni kwamba walitakiwa kuongwza grooming.

Of course Nywrere ataonekana aliweza kui control nchi zaidi ya Samia.
 
Nadhani jambo likiwepo/tokea huwa kunakuwa na nadharia njama (Conspiracy theories) kadhaa kulihusu.

Kwa mfano kwetu sisi watu wa Nyanda za juu kusini Kuna kisa cha Tuntemeke Sanga kuwekwa kizuizini.

Kwa ivo mada kama hii kunyumbulishwa kwake majina ya wahusika ni kitu muhimu sana.
Hiyo sheria nzima ni udhalimu, kwa hivyo jambo hilo kumtokea mtu yeyote ni udhalimu, bila kujali jina wala sababu.

This is one of the forty Draconian laws declared oppressive since the Justice Nyalali report.

The very existence of this law was an affront to freedom in Tanzania.
 
Back
Top Bottom