Watajeni wote waliotekwa au kuuawa Enzi Nyerere akiwa Rais

Watajeni wote waliotekwa au kuuawa Enzi Nyerere akiwa Rais

Mara kadhaa nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakisema kuwa enzi za Mwalimu Nyerere akiwa Rais watu "wengi" Sana waliuawa au kupotezwa.

Sasa kabla ya waliofanya kazi na Nyerere wote kufa, ni Bora watu wanaowafahamu waliouawa zama Julius Nyerere alipokuwa Rais wa nchi yetu, wawataje watu hao walikuwa ni kina nani?

..kuna Wazanzibari walikamatwa na kufungwa na Sheikh Abeid Karume na baadae kuuwawa.

..suala hilo naliweka mikononi mwa Mwalimu Nyerere kwasababu yeye ndiye alikuwa Raisi wa Muungano.

..Pia namlaumu kwa kushindwa kuhakikisha kwamba miili ya Wazanzibari waliouwawa kipindi cha Karume inapatikana.

..Na mwisho kuwachukulia hatua waliohusika na mauaji hayo.

..Wazanzibari waliopotezwa kipindi cha Nyerere na Karume ninaowakumbuka ni Abdullah Khassim Hanga, Mdungi Ussi, Aziz Twala, Othman Majura,na wenzao.
 
Kwa staili hii itabidi kila utawala kuanzia wakoloni waliouawawa watajwe. Alafu mbona huwa kuna siri hutolewa baada ya miaka kama arobaini misheni huwekwa wazi, vitabu viko wapi mbona hatuvioni tusome siri released/rejected?
 
Mnataka kujua kila rais aliua wangapi?, hiyo hesabu ni pamoja na waliouawa kwa adhabu ya kunyongwa?
 
Mnataka kujua kila rais aliua wangapi?, hiyo hesabu ni pamoja na waliouawa kwa adhabu ya kunyongwa?

..Ndio maana ya Ukweli, Haki, Maridhiano, na Upatanishi.

..Wote walioumizwa na serikali ktk awamu zote tangu tupate UHURU wanapaswa kujulikana, na familia zao ziombwe radhi, na kupewa mkono wa pole.
 
Nyerere alikuwa groomed kuongoza watu, alisoma na yeye mwenyewe alipenda kuwa "philosopher king". Kiongozi mwenye busara. How much he achieved that is debatable, lakini ukimsikiliza, ukiangalia vitabu alivyosoma na hata kutafsiri, the latest being Plato's "Republic", unamuona huyu bwana angalau anamsoma Plato.

Sasa Kikwete Magufuli na Samia wamemsoma Plato?

Nyerere alianza kuongoza watu tangu enzi za ukoloni akipita nchi nzima kuwaeleza jambo ambalo wengi hawakufikiri linawezekana, kudai uhuru.

Kwa hivyo Nyerere aliheshimika kama kiongozi aliyesaidia Watanganyika kupata uhuru.

Na wakati anaanza kuongoza nchi, kulikuwa hakuna watu wengi, kama milioni 9-10 tu. Ni kama Greater Dar es salaam tu kwa sasa.

Kwa hivyo alivyoachiwa nchi na wakoloni, nchi haikuwa comolex sana, aliweza kui shape vizuri alivyotaka yeye, na hata alipopata changamoto, ali deal nazo na kujifunza mapema (1964 Tanganyika mutiny, the Citizenship Act, labour strikes , internal dissent, geopolitics, etc).

Long story short Nyerere alichukua nchi tangu mwanzo, nchi ilikuwa simpke, alijua na kiasi fulani kujali hali ya Watanzania. Nchi haikuwa na complexity kama sasa hakukuwa na TV, hakukuwa na mtandao, magazeti karibu yote yalikuwa ya chama na serikali, wasomi walikuwa wachache, Watanzania waliosafiri walikuwa wachache.

Kadiri siku zilivyoenda ndivyo yote hayo yalibadilika.

Mwinyi kaingia kuwa rais tushaanza kumuangalia Michael Jackson na Harrison Ford kwenye TV. By 1989 tushaona Tiananmen Square na Perestroika. Watanzania wametoka kuwa nchi ya watu milioni 9 -10 mpaka sasa milioni 70.

Tumeongeza idadi ya watu mara 7 tangu uhuru.

Huwezi kutegemea nchi iwe vilevike viongozi waweze kui control kirahisi.

Hususana kama weledi wa viongozi unazidi kupungua.

Kadiri tulivyoendelea ndivyo viongozi walivyozidi kukosa grooming, wakati kiukweli ni kwamba walitakiwa kuongwza grooming.

Of course Nywrere ataonekana aliweza kui control nchi zaidi ya Samia.
Umeeleza vyema sana sanaa 😊 kwa kuongezea nyerere alikuwa mjamaa (Utopian socialist)

Ujue socialism Ina type mbili Utopian socialism na scientific socialism ie. China Sasa nyerere yeye ana angukia kwenye Utopian socialism

Ndio maana hakujilimbikizia Mali , alitamani kuona jamii inakuwa na usawa, nyerere angekua na akili za rais wa Gabon mzee BONGO hakika siku moja mtoto wa kumzaa ange mwandaa awe Raisi wa Nchi....

Wazee wengi baba zetuu wa 1950's wanaishia ishia Kuna wazee walikua WAZALENDO sanaa kwa Sasa hiyo cream inaishia ishia..

Kingine mtu kama Samia hakupaswa kuwa raisi maana sidhanii kama hayo ma book ya kina Plato na Wana philosophy hao kawasoma kina AGREI WA GHANA E.T.C

NB. Unaweza UKAWA kiongozi mzurii kama utawaweka karibu wenye maarifa na akili ila izii nchi tegemezi za third world country ni ngumu sana kupata maendeleo ya kweli
 
Kuna kitu sikielewi, sababu ya rais kuamua nani anyongwe na nani asinyongwe baada ya hukumu ya mahakama ni nini hasa!

Hii naiona kama rais kuingilia muhimili wa mahakama.
Yaani ingekuwa mahakama ikisema tu kazi inaendelea.
You have a point.
 
Nyerere aliweka watu wengi detention kuliko aliowaua akitumia Preventive detention act ya 1962.

Adhabu nyingine ilikua ni kunyimwa uhuru japo unaweza kuwa mtaani ila kutoka lazima uwe na ruhusa na wanakuwepo watu wa kukuangalia.

Sheria hiyo ilimpa uwezo wa kumuweka mtu kizuizini bila kumfungulia mashtaka kama ameonekana ni tishio japo wengi waliwekwa kizuizini kwa kutofautiana nae mawazo na hawakuwa tishio kwa namna yoyote.
 
Karume,titi Mohammed, Hassan bin amir, abdallah fundikira(alikimbilia Mombasa)teddy kaselabantu,kasanga tumbo, yule mbaya aliyeandika the dark side of nyerere na nyerere,a saint or untarnished tyranny orodha ni ndefu
Wewe ni mlemavu wa akili. Karume aliuawa na Nyerere!! Lazima uwe mwendawazimu.
Karume aliuawa na mwanajeshi ambaye baba yake aliuawa na Karume. Yale yalikuwa ni mauaji ya kisasi.
Bibi Titi Mohamed, Fundikira, Kasela Bantu, Kasanga Tumbo, watu wote wanafahamu kuwa walikufa vifo vya kawaida, hawakuuawa na yeyote.

Wakati wa Mwalimu Nyerere, hakukuwa na utekaji wala upotezaji watu. Hata waliotaka kumpindua, walikamatwa na kupelekwa mahakamani. Mwalimu Nyerere, kwa nafasi yake kama Rais, waliokuwa karibu naye wanasema alikuwa hapendi kabisa kuweka sahihi kuidhinisha kifo hata kwa mtu aliyehukumiwa na mahakama kuuawa. Katika kipindi chake chote cha utawala alitia saini kuidhinisha hukumu ya kifo kwa watu wawili tu: Mwamindi, muuaji wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Kleruu; na wa pili alikuwa ni mhindi wa Songea aliyemwua mkewe ili alipwe bima ya kifo aliyokuwa amemkatia mkewe. Hakuna mwingine yeyote ambaye mwalimu aliidhinisha hukumu zao za kifo.
 
Mara kadhaa nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakisema kuwa enzi za Mwalimu Nyerere akiwa Rais watu "wengi" Sana waliuawa au kupotezwa.

Sasa kabla ya waliofanya kazi na Nyerere wote kufa, ni Bora watu wanaowafahamu waliouawa zama Julius Nyerere alipokuwa Rais wa nchi yetu, wawataje watu hao walikuwa ni kina nani?
Utekaji wao ulikua digital mtu anapote kimya kinya bila kushtukiwa alienda wapi
 
Kuhusu kunyonga wawili tu si kweli,na hili linathubitishwa na yule mzee aliyekua mnyongaji mstaafu Dodoma aliyefanyiwa mahojiano na mwananchi,huyu mzee alianza kunyonga tangu nyerere akiwa madarakani na alisema kanyonga wengi tu
Siku za mwanzo kunyonga watu walikua wakimtokea ndotoni mpaka alipofanyiwa mambo na wazee wake
Tabora kuna story ya mtu kunyongwa na kutokufa,ikabidi mnyongaji ampopotoe shingo
Mnyongaji akawa mwendawazimu wa kudumu
Hizi story za nyerere kunyonga wawili tu ni za kutaka kum-potray kama mtakatifu
Hujui historia, Mwinyi, Kikwete ndo wamenyonga watu wengi.
 
Karume,titi Mohammed, Hassan bin amir, abdallah fundikira(alikimbilia Mombasa)teddy kaselabantu,kasanga tumbo, yule mbaya aliyeandika the dark side of nyerere na nyerere,a saint or untarnished tyranny orodha ni ndefu
Umeelewa swali au kazi(assignment) uliyo pewa?
Titi Mohamed amekufa mwaka 2000 Afrika Kusini
Nyerere amekufa 1999. Sasa marehemu alimuuwa vipi Titi Mohamed?
Kuna wengine hapo waliokufa vifo vya kawaida vya wazi tu. Sijui Nyerere aliwauwa vipi?
Hii chuki mbaya sana.
Karume kauwawa na wazanzibar wenzie ambao hatima yao inajulikana. Nyerere anahusikaje hapo?
Weka ushahidi hata wa kimazingira.
 
Back
Top Bottom