Watajeni wote waliotekwa au kuuawa Enzi Nyerere akiwa Rais

Aaah kile kipindi cha Nyerere ilikuwa ni Kipindi cha Giza na upumbavu wa kutupwa, ni kama tulikuwa tuko stage ya Kwanza kuwa nyani...baadhi ya watu wangu wa karibu walikumbwa na madhila au tuseme mkono wa Nyerere, ni mambo ya kusikitisha lakini sasa kule tushatoka, tusawazishe mambo ya sasa hivi maana yaliyopita yamepita kwasababu tukianza kutafutiana sababu na kutengeneza mazingira ya Nani alikuwa mzuri itakuwa ni uongo maana hakuna msafi hata mmoja wote waliowahi kushika kijiti ni wachafu vibaya...Inabidi tujinasue sasa hivi.
 
tujikite kutafuta suluhu ya matatizo ya nchi kwasasa, ni kweli historia ni muhimu. TAL anawashinda wengi ktk kutambua ukweli wa historia ya matatizo tunayo jadili.


 
Aliye
Inaaemekana kuwa aliyemuua Karume aliamini kuwa Karume alimuua baba yake. Karume alijua kuwa amejiapiza kumuua lakini hakumtilia maanani. Aliamini utoto ndio unaomsumbua. Nyerere hakuhusika.

Hayo ya Karume kutaka kujitoa kwenye Muungano ni mazungumzo ya vijiweni. Hakuna ushahidi wowote wa nia hiyo. Acheni uongo.

Amandla...
 
Unatengenezewa story,kuna kitu inaitwa kitembelea nyota, yaani watu walipitia humohumo,humud hakua peke yake kwenye kutekeleza mauaji,hao wengine motive ilikua nini?
 
Soma tena topic,usikurupuke kama uharo
 
The Dark side of Nyerere's Legacy by Ludovic S. Mwijage | Open Library The Dark side of Nyerere's Legacy by Ludovic S. Mwijage | Open Library
Humud hakuwa peke yake kwenye kutekeleza mauaji ya karume,aliokua nao motive ilikua nini?
 
Nyerere hakuwa na upuuzi wa kuua, kuteka na kupoteza watu.
Haya mambo yalianza enzi za Mkwere.

Soma kitabu hiki mkuu ndio utafahamu kuwa hii nchi ne jehanam tangu tulipopata uhuru...
Sio lazima ukitafute amazon, hata hapa JF kilishawekwa japo sikumbuki ni uzi gani!
 
Karume,titi Mohammed, Hassan bin amir, abdallah fundikira(alikimbilia Mombasa)teddy kaselabantu,kasanga tumbo, yule mbaya aliyeandika the dark side of nyerere na nyerere,a saint or untarnished tyranny orodha ni ndefu
Hao wengine sijui,ila Kasanga Tumbo ni mzee wangu na tumeishi Tabora miaka yote na Nyerere kafariki kabla ya mzee
 
Wewe unaongea siasa za maandiko,hapa tunajadili fact ukweli ni kuwa Karume aliuwawa na Nyerere na wengine wengi tu.
 
Karume,titi Mohammed, Hassan bin amir, abdallah fundikira(alikimbilia Mombasa)teddy kaselabantu,kasanga tumbo, yule mbaya aliyeandika the dark side of nyerere na nyerere,a saint or untarnished tyranny orodha ni ndefu
Kuna waliokimbia nchi........
Abdurahman Babu, Oscar Kambona nk
 
Nyerere ni muasisi wa chama gani ? Je hicho chama kimeleta maendeleo gani katika miaka 64 ya uhuru ? Nyerere aliisaidia vyama gani kwa kuweka kambi hapa nchini kwa ajili ya mapambano ya uhuru ? Je hivyo vyama vilivyoweka kambi hapa nchini vimesaidiaje nchi zao ? Ukishajibu haya ndio utajua kuwa nyerere alikuaa kilaza au mwerevu. Haiwezekani baada ya kupata uhuru chama chake na vyama alivyovisaidia vyote vikaua uchumi wa nchi zao na kushindwa kupiga hatua hata ndogo. Siku zinavyozidi kwenda ndio anazidi kuonekana mjinga na mpumbavu. Huko mbeleni CCM ikiendelea hivi kuna siku maandamano yatafanyika na watu wataenda kuchoma moto mussoleum kule BUTIAMA.
 
You must be crazy unataka ushahidi kwenye siasa,huo ni zaidi ya uwendawazimu.
Unadhani ni kawaida kwa Raia wa kawaida au mwanajeshi kumchapa Rais risasi pasipo mikono ya wakubwa wenzake.
Toka usingizini brother.
 
kwahyo utekaj uachwe uendelee
Wahi milembe una matatizo ya akil
Huelew kuwa hz tabia soon mtaanza fanyiwa nyiny
 
Unatengenezewa story,kuna kitu inaitwa kitembelea nyota, yaani watu walipitia humohumo,humud hakua peke yake kwenye kutekeleza mauaji,hao wengine motive ilikua nini?
Luteni Humud na wenzake walikuwa sehemu ya mpango ulioongozwa na wakina Babu wa kumuondoa Karume.

Motive ilikuwa ni ukatili na utawala wa mabavu wa Karume. Wazanzibari walikuwa wanapumua pale tu wanapokuja Bara. Ingawa viongozi wa jaribio hilo walitaka liahirishwe lakini wauaji waliamua kuendelea nalo maana walijua kwa vyovyote vile wangeuawa maana tayari walikuwa wanatafutwa.

Karume angehakikisha wanauawa kama angepona jaribio hilo. Kama alivyofanya kwa wakina Mdungi Ussi, Kassim Hanga na wengine.

Amandla...
 
Mshabadili story baada ya kuuliza wengine motive ilikua nini,babu hakuhusika na hayo mauaji,na probably alikua serikali ya muungano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…