Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Rais Samia alishaweka wazi na kujipambanua kimaneno na kimatendo juu ya hasira zake Kali na maamuzi yake magumu kwa yeyote atakaye chezea fedha za umma,Hana Cha Nani Wala Nani katika Hilo,hamuogopi mtu Wala haangalii sura katika hili, Hana uvumilivu Wala Subira katika suala la kumuwajibisha yeyote atakayebainika kwenda kinyume na utaratibu na miongozi ya matumizi ya Fedha za Umma, hapa Ni mwepesi kutumia kalamu yake kutengua na kuagiza uchunguzi wa haraka ufanyike ili wahusika wafikishwe haraka mahakamani kujibu mashitaka Yao.
Hii Ni kutokana na Rais wetu mpendwa Jasiri na shupavu mama Samia kutambua kuwa fedha za umma zinapaswa kutumika vizuri kwa Nidhamu katika kuwapatia huduma watanzania,Anatambua namna watanzania wanavyojinyima ili walipe Kodi,anatambua namna anavyohangaika huku na kule kutafuta fedha kwa ajili ya kupeleka huduma Bora kwa watanzania,Anatambua namna watanzania wanavyo vuja jasho kuchapa kazi na kulipa Kodi serikalini.
Rais wetu mpendwa anatambua watanzania wanyonge aliojitoa na kujitolea kuwatumikia kwa uzalendo Hadi kufikia hatua ya kukosa muda wa kupumzika na familia yake wanavyoumia,kusononeka ,kusikitika na kulia machozi pale wanaposikia Kuna watumishi au viongozi wachache walioapa au kulipwa mishahara mikubwa na minono yenye minofu kwa ajili ya kuwatumikia na kuwahudumia wamefuja na Kuchezea Fedha za Umma bila huruma Wala aibu kwa maslahi yao binafsi,Vijana waliomaliza vyuo vikuu wanaumia na kutokwa machozi wanapoona wanahangaika huku na kule kutafuta mitaji huku nyuma wengine wanakula pesa zao za Kodi bila huruma.
Rais Samia anatambua anaongoza Taifa la aina ipi,Anatambua anaongoza Taifa Ambalo wengi wanahitaji kusaidiwa kukwamuliwa kiuchumi,Anatambua wapo wazee huko vijijini wanahitaji usaidizi wa serikali yao kuwapatia huduma za matibabu pasipo malipo maana wengi wanakuwa hawajiwezi kifedha,Ndio maana Rais Samia hawezi kumvumilia yeyote atakaye chezea fedha za umma.
Rais Samia anatambua namna watanzania wanaolipa Kodi kwa uaminifu wanavyoumia wanaposikia Kuna watu waliopewa dhamana wamegeuka kuwa mchwa wa fedha zao,Rais Samia anatambua Jambo hili linawaumiza Sana walipa Kodi,linawapunguzia molari ya kulipa Kodi au kotoa risti au kudai risti,Rais wetu mpendwa mama Samia anatambua namna mijadala inavyokuwa mingi mitaani miongoni mwa watanzania wanaposikia halmashauli fulani mkurugenzi wake kafuja mamilioni ya Fedha bila huruma ili Hali wao Wana watoto majumbani mwao wanaoamka alfajili kufanya vibarua vya kubeba zege ili wajikimu kimaisha licha ya kuwa Wamesoma Hadi vyuo vikuu.
Hii ndio sababu Rais wetu mpendwa mama Samia amekuwa akichukua hatua za haraka Sana ikiwepo kutengua uteuzi na kuagiza uchunguzi wa haraka kupitia Takukuru, kwa kuwa anauchungu na maisha ya watanzania na anataka juhudi za kutafuta pesa anazozifanya zitoe matokeo chanya kwa watanzania badala ya kuwaneemesha wachache na familia zao huku kundi kubwa likibaki na unyonge.
Hii ndio sababu ya Kuendelea kuaminika na kuungwa mkono na mamillion ya watanzania ambao wanatambua dhamira njema ya Rais wetu katika kulitumikia Taifa letu.
Songa mbele Rais wangu mh mama Samia,Mimi nitaendelea kukutetea na kukusemea kwa nguvu zangu zote katika yale yote unayolifanyia Taifa letu, nitaendelea kuwa mzalendo kwa Taifa langu na nchi yangu, Nitaendelea kutumia jukwaa hili kutoa ushauri wangu Kama mwananchi wa kawaida na mwenye upendo mkubwa Sana na Taifa langu.
usikate Tamaa Wala kukatishwa Tamaa na yeyote maana Tulio upande wako Ni wengi kuliko walio kinyume na wewe,Tumekukabidhi kila kitu Cha nchi hii na kukiweka mikononi mwako na tunaamini vyote vitakuwa salama,Tumia nguvu zako zote za kisheria na kikatiba kulinda Rasilimali za Taifa letu na kupambana na yeyote atakaye kuwa kikwazo katika kuwahudumia watanzania ikiwa ni pamoja na kumuweka pembeni na kumfikisha mahakamani, watanzania tupo bega kwa bega na wewe Rais wetu, Tunaendelea kukuombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia.
Kazi Iendeleee , mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627