Watakiona chamoto watakaobainika Kuchezea fedha za Umma katika uongozi wa Rais Samia

Awamu hii ya Rais Samia hakuna atakayesalimika na kuishi kwa amani ikiwa atabainika kugusa pesa za umma,ndio maana unaona Takukuru wapo kazini muda wote kufanya uchunguzi na upelelezi wa kina kufuatilia fedha za watanzania
 
Uteuzi unatafutwa sana
Hapana ndugu yangu Mimi siandiki kusaka uteuzi Bali naandika kutoa mawazo yangu juu ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania mama Samia suluhu Hassani na namna alivyojipanga kuleta matokeo chanya kwenye maisha ya watanzania
 
Endelea tu kumwaga sifaaaaa lakini katika meza ya ulaji huwezi kumuweka nje sababu Ile system pia imemchafua
 
Huku mbali sana! Nenda kaanzie kule kule Mbozi,utapanda vyeo mdomdo! Tatizo umri nao
Huku mbali sana! Nenda kaanzie kule kule Mbozi,utapanda vyeo mdomdo! Tatizo umri nao
Serikali ya Rais wetu mpendwa mchapa kazi na mzalendo wa kweli nyota ya Matumaini hagawi vyeo kwa watu Bali anagawa majukumu kwa watu wa kumsaidia katika kuwahudumia watanzania,Pia Mimi siandiki hapa kwa ajili ya vyeo Bali naandika kwa hiyari yangu na uzalendo wangu kwa Taifa langu na nchi yangu,Mbozi inaendelea kumshukuru mh Rais kwa kuwapatia mbolea za Ruzuku zilizo Leta Tabasamu kwenye mioyo ya wakulima wa kata zote 29 za wilaya ya mbozi
 
Kwenye Avatar hapo weka na picha yako kabisa! Itarahisisha kukumbukwa
 
Mimi nimetoa maoni yangu kuhusu Rais Samia na uthabiti na uimara wake kiuongozi katika kushughulika na wabadhirifu wa fedha za umma na siyo habari za uteuzi
ila weeeee tumghoje unazingua sana aisee...sijui mnyiha wa wp wewe hakyamungu, yaani unatia aibu sana .. sijui nani alikuleta mjini aisee, yaani huyo ndo wa kulaumiwa kbs kbs aisee. .ilitakiwa akuache huko huko nyimbiri na msangamweru uwe mtengeneza bunduki za kienyeji [emoji23][emoji23][emoji23]..huu uongo na nguvu unayoitumia hapa , lait ungeitumia kule kutengeneza magobore muda huu ungekuwa tajiri mkubwa hapo nyimbiri ... Chini ya chama kinachoitwa ccm upigaji hauwezi kuisha , na hata ww unatamani uteuliwe ili ukaibe ndo maana unaweka hiyo namba yko ya simu...weee veepi mnyiha weeee [emoji23][emoji1][emoji23]

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Aliweza magufuri hadi akajenga miundombinu.
 
Kununua magari kwa 500M sio kuchezea fedha za umma?? 🤣🤣🤣
 
Vijana waneona uchawa unalipa...ujinga mtupu.
Jamaa anaandika mashudu matupu hapa
 
Hakuna atakayebakia salama akibainika Kuchezea Fedha za umma
Hawa wote waliopo salama maana yake hawajabainika!!??
Basi hiyo serikali yako ina tatizo kubwa sana zaidi ya tujuavyo.

Tupo nao mitaani wakiwa full na amani wanachezea tuu fedha za umma.
 
CCM na serikali Yake ni imara Sana ndio maana imekuwa ikichukua hatua za haraka na Kali kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma
Huna hoja wewe bado chawa mchanga kisiasa na kiakili.
Hebu choma vitumbua kwanza akili ikomae ndipo uwe chawa mwenye hoja
 
Hawa wote waliopo salama maana yake hawajabainika!!??
Basi hiyo serikali yako ina tatizo kubwa sana zaidi ya tujuavyo.

Tupo nao mitaani wakiwa full na amani wanachezea tuu fedha za umma.
Vita dhidi ya ubadhirifu wa Mali ya umma ,ufisadi,Rushwa,matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa fedha za umma Ni endelevu na haina kikomo ndio maana unaona muda wote serikali ipo kazini na silaha zake kupambana na watu wa aina hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…