Watanganyika amkeni tujitafakari haraka ! Tunapigwa na kitu kizito

Watanganyika amkeni tujitafakari haraka ! Tunapigwa na kitu kizito

Nina huzuni na kushangazwa na hali ilivyo sasa. Wale waliouwawa, waliotekwa, na waliopotezwa ni watanganyika.

Wale wanaoandamana ni watanganyika, na polisi wote ni watanganyika pia.

Wale wanaoamuru polisi wa Tanganyika kuwapiga na kuuwa watanganyika ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Rais wote kutoka Zanzibar.

Hivyo, watakaoumia na kufa ni watanganyika! Je, kweli huu muungano unafanya kazi? Je, polisi wa Tanganyika wanaelewa ujumbe wangu?

Ni jambo la kushangaza kuona watu milioni 1.5 kutoka Zanzibar wakitoa amri kwa kutumia jeshi linalotokana na watanganyika milioni 60 kuuwa watu milioni 60.

Hii si sawa! Je, hii ni haki? Tunahitaji kujadili kwa kina masuala haya na kuhakikisha haki inapatikana kwa wote bila kujali asili au eneo.
Kama hauna la kuandika ni bora unyamaze, kwani wakati Mkapa anatoa ruksa jeshi kuvuka maji kwenda kuua watu Zanzibar yeye alikuwa ni Mzanzibari? Tanganyika ni nchi mfu acha kujichekesha
 
Ndio Sababu alikata moto usiku hata ,muda wa kupewa Panadol haukuwepo.
 
Tanganyika ilikufa kwa kuunda Tanzania ila Zanzibar ni sehemu ya muungano yenye special autonomy (soma kwa kuelewa special autonomy). Tanzania siyo ya kwanza kuwa na mfumo kama huo. Iko Taiwan, Hong-Kong, Wales, Scotland, Northern Ireland, Bermuda, Puerto Rico etc
Mbona ya Taiwan na Hong Kong hayafanani na ya Tanzania na Zanzibar!??
Mkuu unaelewa hata unachoeleza!?
 
Mumeo, kwanini hutaki kujibu hoja dada angu? tuambie lini ulienda Moshi ukazuiwa kununua ardhi? acha upumbavu amka, nenda Zanzibar ukagombee au uombe kitambulisho cha mkazi tuone.
Huyo anaonekana amelewa wanzuki achana naye.
Mzanzibari akija Bara anapata haki zote kiwepesi hata akiwa na kitambulisho cha mkazi wa Zanzibar Bara anapata kazi na ananunua ardhi.
Nenda wewe mbara Zanzibar leseni tu kama ya bara hauruhusiwi kuitumia Zanzibar.
Kuhusu kazi wanapewa kipaumbele wenye kadi za mkaazi wa Zanzibar.
Kununua ardhi Zanzibar wewe mbara sahau.
Halafu huyo sijui anaongea utumbo gani.
 
Huyo anaonekana amelewa wanzuki achana naye.
Mzanzibari akija Bara anapata haki zote kiwepesi hata akiwa na kitambulisho cha mkazi wa Zanzibar Bara anapata kazi na ananunua ardhi.
Nenda wewe mbara Zanzibar leseni tu kama ya bara hauruhusiwi kuitumia Zanzibar.
Kuhusu kazi wanapewa kipaumbele wenye kadi za mkaazi wa Zanzibar.
Kununua ardhi Zanzibar wewe mbara sahau.
Halafu huyo sijui anaongea utumbo gani.
Ni mwenda wazimu pekee anaweza kukubaliana na wazanzibar
 
Mara kibao mie nimeenda na nimeitembea sana.
Mbara hupewi kipaumbele kama mzenji.
Ila huku TZ mzenji anapewa access sawia na mbara pasi na upunjo wowote.
Hili tulitizame aisee.
Sisi bara hatuna akili maana tumekuwa koloni la Zanzibar ni aibu kubwa sn
 
Leo ndo leo tupo tayari watuue lakini tunaandamana
20240923_172531.jpg
 

Attachments

  • VID-20240923-WA0037.mp4
    4.5 MB
Tofauti iko wapi? Weka hapa unachojuwa nami nitakujibu
Hong kong toka miaka ya nyuma inaitwa vivyo hivyo na China toka kipindi cha Qing na Ming Dynasty inajulikana ni China.
Ni wapi palibadilika jina kama Tanganyika kuwa Tanzania baada ya muungano!??
 
Back
Top Bottom