Watanganyika msihofu bandari zenu zitarudishwa mikononi mwenu na mahakama mkataba uloridhiwa na Bunge ni Void ab initio

Uamuzi kama Taifa tufanye nini?
 
Kwa kuwa emir wa dubai ndio waziri mkuu wa uae na ndio mtendaji mkuu wa serikali ya uae yaani federal govt hivyo basi maamuzi ya dubai ni maamuzi ya uae amri ya dubai ni amri ya uae. Ni sawa na mheshimiwa Raisi Mwinyi wa Zanzibar ni makamu wenyekiti ccm maamuzi yake ni halali kama makamu mwenyekiti na ni maamuzi ya ccm na viongozi wa chini wanatii.
 
Kwa kutokuupata mkataba wote rasmi, mengine yanayobaki ni speculations tu. Ikishakuwa issue ya kisheria, ni bora tu kujihakikishia hata kama uwezekano wa hilo kutokea ni mdogo mno.
Hizo ni hoja ulizotakiwa kuzitoa kabla ya mkataba kusainiwa.

Mkataba wenyewe una kipengele cha wewe kutoupata mkataba wote rasmi, hivyo, wewe kuuona mkataba wote rasmi ingekuwa ni kuvunja mkataba. Huu uliouona umeuona kwa kuvuja tu.

Tatizo lako si mkataba, tatizo lako ni viongozi walioingia huo mkataba.

Huelewi wapi?
 
Acha kuongea ujinga. Zanzibar lili ilishasaini mikataba kwa niaba ya Muungano? Wapi Zanzibar ina ubalozozi wa kudumu?
Kwani wapi nimesema Zanzibar imesaini mkataba kwa niaba ya Muungano?

Unaelewa kusoma na kufuatilia hoja kimantiki au unajibu kishabiki tu?

Nakwambia hivi, serikali ya Zanzibar inaweza kusaini mkataba wa kimataifa kati ya serikali ya Zanzibar na nchi ya kigeni, kama mkataba huo umepata idhini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Hapo si kusaini mkataba kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Unaelewa hilo mpaka hapo?
 
Dubai sio state na haina capacity ya kuingia mkataba wa aina yoyote.

Mahakama itatenda haki
Mafisadi wa CCM chini ya mwenyekiti wao wataaibika

Huyu Wasira na pumba zake za kumtusi Lissu ataona aibu
 
Uamuzi kama Taifa tufanye nini?
Ondoeni CCM, wekeni utamaduni wa kusimamia viongozi, maana mkiondoa CM bila kusimamia viongozi yatajirudia hayahaya kwa yeyote, wekeni uwazi wa hii mikataba ili iwe inajadiliwa kwa kina kabla ya kupitishwa, pitisheni katiba mpya inayoondoa mamlaka makubwa sana ya viongozi, hususan rais, ukiweka uhuru wa rais kushitakiwa unapunguza impunity.

Zaidi ya yote, futeni ujinga wa watu wengi, ujinga huu ndio mtaji wa viongozi kufanya wanavyotaka, bila kuuondoa ujinga huu mnaweza kupata katiba mpya na sheria za kuruhusu uwazi, halafu mkashindwa kuzitumia kwa sababu wajinga wengi.
 
Dubai sio state na haina capacity ya kuingia mkataba wa aina yoyote.

Mahakama itatenda haki
Mafisadi wa CCM chini ya mwenyekiti wao wataaibika

Huyu Wasira na pumba zake za kumtusi Lissu ataona aibu
Wewe huelewi unchokiongea, hata wewe unaweza kuingia makubaliano na serikali MoU.

 
Hapana,

Inategemea anafanya maamuzi kwa capacity gani.

Ujue hata Rais wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kuna vikao anaingia kama Mwenyekiti wa CCM, anafanya maamuzi kama Mwenyekiti wa CCM, na kuna vikao anaingia kama Rais, anafanya maamuzi kama rais.

Hatusemi kwamba kwa kuwa mtu mmoja huyu ni Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, basi maamuzi yake yote ni ya Rais na ya Mwenyekiti wa CCM pia.

Kwa mfano, Rais ana uwezo wa kulivunja Bunge, Mwenyekiti wa CCM hana.

Samia akitaka kulivunja Bunge, atalivunja kama Rais, hawezi kulivunja kama Mwenyekiti wa CCM.

Full Instruments of Power kwenye mkataba uliovuja zimetoka serikali ya Dubai.
 
Wavunje huo mkataba, uwe Void au laa, watamke kwamba umevunjwa..

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Simple tu kwa kuwa emir wa dubai ndio waziri mkuu wa uae na mtendaji mkuu wa serikali yaani federal govt ya uae basi maamuzi ya emir wa dubai ni maamuzi ya uae kwa kuwa always since creation ya uae dubai wao ni vice president na waziri mkuu na utendaji wa serikali uko chini yao maamuzi yao ni maamuzi ya uae .
 
Hilo si kweli.

Lakini, hata lingekuwa kweli, issue ya "Dubai si nchi" ndiyo ingezidi kukosa nguvu.
 
Dubai sio state na haina capacity ya kuingia mkataba wa aina yoyote.

Mahakama itatenda haki
Mafisadi wa CCM chini ya mwenyekiti wao wataaibika

Huyu Wasira na pumba zake za kumtusi Lissu ataona aibu
Binafsi nauona usaliti, usaliti uliofanywa na waliofungua kesi na mawakili wanaojidai kuwatetea walalamikaji. Naita usaliti saba kesi hii haikutakiwa kufunguliwa, ilatakiwa nginja nginja hii waachiwe wanahatakati na wanasiasa. Naita wasaliti sababu ikitojea maamuzi ya mahakama ikawapa ushindi Selikari maana yake hoja hii ya kupinga mkataba itakuwa imekufa na kuua uanaharakati. Ndio maana wengine tukiwa tunapambana na mdai hatuendi mahakamani tuna ng'ang'ana na mdai wetu mpaka mwenyewe anyoshe mikono, sababu ukimpeleka mahakamani akashinda ndio mwisho wa madai yetu.😭😭
 
What is a state?
 
Hapana
 
Mbona unajichanganya braza, unatetea usichokijua mara imevujishwa sasa kitu kilichovujishwa uwa haina uhalisia mbona unaitetea?

Tanganyika hamko serious nyie ujinga umewatawala aise
 
Vichwa maji CCM wameleta balaaa kubwa kabisa
 
Why is the question of "what is a state" important here?

Umesoma na kuelewa nilichoandika ukakinukuu?

Au unauliza maswali kwa kukariri tu?
Nenda kasome mkataba wa Montevideo. Sio unadandia mada wakati kichwani ni bumunda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…