Kwa mantiki hivyo basi. Mkataba huu tumeshauza bandari zetu?
Hatujauza Bandari. Tunaweza kuuvunja mkataba kwa namna mbili tu.
1. Kuwaomba DPW tuvunje makataba, wakakubali. Hapa uwezekano wa hili kutokea ni karibu na sifuri.
2. Kwenda kwenye usuluhishi wa kimataifa. Ambapo piga ua galagaza tutapigwa faini, tulipe faini kwa kuvunja mkataba. Tundu Lissu anashauri tufanye hivi, kwa sababu tutapigwa faini, lakini itakuwa ndogo tukiwahi mapema, kadiri tunavyozidi kuchelewa ndivyo faini itakavyozidi.
Pia, tunaweza kuongea na DPW tubadili vipengele vya mkataba, tuurudishe bungeni, upate ratification upya, lakini hapa tutategemea huruma za DPW kama option 1 hapo juu, na most likely watakataa na tutaishia kwenye usuluhishi kama option 2 hapo juu.
Vyovyote vile, hakuna ku nullify mkataba bila faini hapo.
Tumecheza ule mchezo wa chess ambapo viongozi wameona wanakula, wanakula, wanakula kete, mwisho wake wanajikuta wamefungwa kwa checkmate, hawana pa kucheza, mchezo umeisha.
Uroho wao umewaponza.
Mkataba huu uneshabadili sheria za Tanzania kwa namna ambayo maliasili za Tanzania zimepunguziwa ulinzi wa kisheria, kwa hiyo, hata tukivunja mkataba huu, madhara yake ni zaidi ya mkataba wenyewe, kwa sababu umeshabadili mpaka sheria tayari.
Madhara yake yatakuwapo kwenye mikataba yote inayofuata.
Zaidi ya mkataba, tunatakiwa pia tufute mabadiliko ya sheria yaliyoletwa na mkataba huu.
Yani hata tukiuvunja mkataba, tusi deal na DPW tena, madhara yaliyofanywa na mkataba kwenye kubadili sheria bado yapo, mpaka tuondoe mabadiliko ya sheria yaliyotokana na mkataba.