Naomba uweke hapa serikali ya Hong na Dubai namna zilivyo na uelezee mamlaka zake zilivyo.
Serikali ya Hong Kong na serikali ya Dubai, zote ni non state governments (per Montevideo Convention definition of a state).
Zinafanana kwa hilo, na hiyo ndiyo point muhimu hapa.
Hong Kong si state. Dubai si state.
Zote ni sehemu za states nyingine.
Hong Kong ni sehemu ya China.
Dubai ni sehemu ya UAE.
Hoja yako ni kwamba, serikali isiyo ya state, kama Dubai na Hong Kong, haziwezi kusaini IGA na state ya kigeni. Kwa sababu hazina nguvu ya state kusaini IGA na state ya kigeni.
Mimi napangua hoja yako kwa mfano.
Nimekupa mfano wa serikali ya Hong Kong, ambayo si serikali ya state, ambayo imesaini IGA na serikali ya USA, ambayo ni serikali ya state/nchi USA.
Hapo tunaona kwamba hoja yako kwamba Dubai si state, hivyo haina nguvu ya kusaini IGA na nchi ya kigeni Tanzania, inakosa nguvu.
Kama vile serikali ya Hong Kong, bila ya kuwa serikali ya state, ilivyoweza kusaini IGA na serikali ya state/ nchi USA, vivyo hivyo, serikali ya Dubai, bila ya kuwa serikali ya state, inaweza kusaini IGA na serikali ya state ya Tanzania.
Kinacjohitajika hapo ni idhini ya UAE kuidhinisha Dubai kuingia IGA na Tanzania.
Hoja yako kwamba serikali ya Dubai haiwezi kusaini IGA na Tanzania haina mashiko.
Hong Kong imepata idhini ya China na kusaini IGA na USA.
Dubai nayo inaweza kusaini IGA na Tanzania kwa mtindo huo huo, kwa idhini ya UAE.
Hoja nzima ya "Dubai si nchi" haina mashiko.
Mataifa kama China na UAE huwa yanafanya devolvement, yanatoa nguvu kwa no nstate governments ndani ya hayo nataifa, kuingia mikataba ya kimagaifa, kwa sababu zao wwnyewe, labda za kibiashara au kisiasa, whatever. Mataifa yote, China, UAE, Tanzania, etc, yana nguvu hizo.
Lete hoja nyingine tuzijadili.
Zipo nyingi tu za msingi, mkataba huu mbovu sana, una hoja nyingi sana za kukosoa.
Wewe huna umasikini wa hoja za msingi za kupinga katika mkataba huu, mpaka uokoteze hii habari ya "Dubai si nchi" ambayo si hoja kabisa.