Watangazaji waliokuwa wanamuhoji Ruto, Tanzania hatutowapata wa kiwango kile daima

Unataka awe chanzo cha mabadiliko ili mumpoteze??? Mifano ya mliowapoteza hamuioni kama inatosha???
 
Hatuna watangazaji. TUNA WASANII AKA MACHAWA AU WACHUMIA TUMBO!
 
Lipi zaidi lilikufanya uandike hivyo, au Kingetreza kinakupiga chenga?
 
Ukiweka Siasa Pembeni hatuna Watangazaji levo za kuwakaribia Wakenya,na tuna kwama sana kama nchi, kama umefuatilia mahojiano ya leo jioni ya Ruto na Watangazaji wa habari utagundua kwamba tuna kosa sana Watangazaji aina ile.
Samahani sana mkuu 'BLACK MOVEMENT', naomba usinielewe vibaya; lakini nikuulize swali kwanza: Hivi hawa watangazaji wetu unawatofautishaje na sisi wengine wote, ambao sasa inatulazimu tuitwe "MAITI"?
Ni jambo lisilotegemewa kabisa, kukuta watu hai (watangazaji) wakiwa katikati ya maiti, watafanya kazi gani hiyo?

Ukinijibu hili swali langu vizuri, najua tutaelewana vyema.

Ndiyo, huko kwenye nchi hiyo uliyotaja kuna waandishi, wanaosomeka na watu walio hai na siyo maiti.

Hapa kwetu Nappy, na yule 'Comic' Abbas waliwateka vyombo vyote vya habari. Kiufupi, hatuna waandishi, wala vyombo vya habari vinavyoweza kuwahudumia watu walio hai.
 
Wapo,unamjia vizuri Tido Mhando na Zuhra Yunusi na bila kumsahau Kikeke,shida ni njaa hapa bongo
 
Lipi zaidi lilikufanya uandike hivyo, au Kingetreza kinakupiga chenga?
I lofu you so much FaizaFoxy come to bed

Ntaweka wana Habari wawili tu ambao wakipewa kiongozi wanampasukia bila kujali chochote au yeye ni nani yaan anapasuliwa na maswali mpaka ananuna

Kuna yule mmoja aliwahi kumuhoji Pole Pole hadi akawa anasema "Wewee Mimi nani wa kuniloga, Shetani mwenyewe ameshindwa" Jina simjui yule Ila alikua anafanya vizuri

Anyway wawili ni Hawa hapa :

1. Mtozi Aloyce Nyanda wa kipindi cha The Big Agenda -star TV

2. Chief Edwin Odemba wa kipindi cha Medani za Siasa -star TV

Hivyo vipindi viwili hata aitwe nani anapasuliwa maswali hata yale asiyoyapenda kuyasikia na kuyatolea ufafanuzi wengine huishia kusema no comment mfano Mrisho Gambo alipohojiwa alipigwa maswali mpaka akapanik

Mwambieni Salama J km anataka kua na vipindi vya namna hio kwenye mahojiano ya
Salama Na basi ahakikishe wale anaowaita hususani Wanasiasa maswali chokozi anawapasukia sio kuwauliza maswali shela lako la harusi ulinunua wapi mumeo mlikutana wapi?

ITV Dakika 45 ni kizuri Ila tatizo ni moja hawaulizi maswali Chokozi labda akiwa Farhia Middle kidoogo anauliza maswali Chokozi mpaka unaona mtu anakunja ndita kuna maswali mengine sio ya kuulizwa au kujibu kwenye hadhara
 
Shallow.
 
Nadhani ni viongozi hawataki changamoto
Nakumbuka kipindi flani cha uchaguzi wkt huo Mkurugenzi wa TBC ni Tido

Alianzisha challenge akaiita mchakato majimboni
Ile ilikua nzuri Sana kwasababu walikutana wagombea wa vyama vyote kwenye Jimbo husika na wananchi wapo na waandishi wa habari wapo na ilikua live ni mwendo wa maswali na majibu

Baada ya matukio yale ilionekana Ccm walikua weupe Sana
Kilichofuata Tido akaliwa kichwa
 
Mabale Matinyi hivi alikuaga nani huyu akaliwa Kichwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…