Watangazaji waliokuwa wanamuhoji Ruto, Tanzania hatutowapata wa kiwango kile daima

What's so special? Kuhoji Rais maswali kunahitaji kusomea Havard au ni matakwa ya Rais kuhitaji kuhojiwa?
 
Kiongozi tatizo ni wateja, Watanzania Ndio wanataka hizo habari! Ujinga na upumbavu umetamalki Kila Kona ! Ni Hatari sana! Hebu fikiria Wakenya wanauana Kwa ajili ya Bajeti , vyombo vya habari vya Tanzania asilimia kubwa vinajafili Cloutus Chota Chama😠😠😠
 
Sahihi
 
Hahaaa . Umetuunganisha sote
 

Mkiwa kwenye mfumo ambao wenye akili na upeo mdogo wanaongoza nchi, watapenda kila mahali wawepo watu wa namna hiyo.

Watu wenye uelewa mdogo huwa ni very defensive, hawapendi ule upungufu walio nao uonekane. Hivyo wanataka kuuziba kwa ukatili na udikteta.
 
Ndio maana nilisema kwenye uzi humu kuwa watu wanaotumia lugha ya kiingereza wana uelewa mkubwa kuliko waswahili. Kuna baadhi hawakunielewa
 
Akili kubwa zinajadili maendeleo.
Akili za kawaida zinajadili matukio.
Akili mbovu zinajadili watu.

Tangu umekaririshwa hicho ukiwa bado mdogo, umebakia nacho hicho hicho mpaka unakuwa kikongwe. Cha ajabu hata ulichokaririshwa, mpaka umezeeka hujaelewa maana yake.

Nani hapa umemsikia anamjadili mtu? Watu wanajadili uwezo wa wanahabari wa watanzania, hawajadili maumbile au sauti za wanahabari.

Wewe yumkini hata watu wakiomba ajira, waajiri wakianza kupitia profiles za waombaji, utasema wanamjadili mtu wakati kinachoangaliwa ni uwezo wa mtu.
 
Mkuu kwanza una moyo mgumu. Unasikilizaga?
 
Kuna jamaa aliwahi kuandika uzi anakwambia kikubwa ubunifu elimu haina umuhimu, ukicheki mahojiano wanayofanya watangazaji wa bongo ni ushuzi mtupu, utaskia eti wewe kama wewe akaunti yako haikosi kiasi gani? Mara ooh tunaskia zuchu anamimba yani ujinga ujinga tu, yote inatokana na kuweka elimu pembeni kusema eti ooh huyu mtangazaji anakipaji matokeo yake hata content wanashindwa kutengeneza
 
Kuna wakati nikiwa naendesha gari, naamua kusikiliza, kwa kweli utabadilisha mpaka unachoka, maana kila unayoipata, hakuna cha maana, na mambo ya ujinga ujinga mtupu. Unaamua kyzima kabisa redio, na kusubiria muda watakapojiunga na BBC.

Tasnia ya habari, kwa kweli ni uozo mtupu. Ndiyo maana watu kwa sasa wanategemea twitter, JF na makundi ya whatsap kuweza kupata habari.
 
Sisi huyu Pascal Mayalla kama hajapewa Bahasha anaweza kidogo.
Pascal Mayalla yupo vizuri, anajitahidi sana hasa umkute kwenye vile vipindi vyake, huku kwenye siasa ni kama anaogopa kuwavua nguo hivyo akajiweka kwenye wakati mgumu. So amekuwa hapendelei sana zaidi ya kuandika.

Angekuwa hata na youtube chanel yake akawa anakutana nawanasiasa kuanzia wakongwe hadi hawa, piga maswali ya kuchimbua mambo. Aiachie hadhira kumbukumbuku.
 
Usipo kutana na Mada ya Ndoa, utakutana mada ya Yanga na Simba au mada ya Wamama na Wababa wa Kambo, au taarabu au Mada za ma House Girls
 
Jamani, hima hima, njaa haijawahi kumwacha mtu hai, njaa ya tumbo, njaa ya kichwa, njaa ya akili, mwenye njaa huweza kula hata uchafu, huuza hata utu wao. Hapa TZ hatuna kabisa waandishi wa habari, kilichobaki ni usanii tu, usanii hadi vyuo vinavyotoa taaluma hii.
Saa nyingine huwa namkumbuka RIP Magufuli kumwambia Pascal Mayala, kuwa " Mayala" kisukuma ni njaa! Sikuelewa, njaa tumboni, kichwani au kielimu, au ya "UCHAWA". Ene wei, naomba wateuzi wamwonee huruma mzee wa watu, wampe hata la ukuu wa wilaya, hata wasanii mbona wanapewa? Kwani yeye kakosa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…