Watano wafariki kwa ajali Bunju B usiku wa Jumamosi 26 Machi, 2022. Walikuwa wakitokea kwenye starehe

Watano wafariki kwa ajali Bunju B usiku wa Jumamosi 26 Machi, 2022. Walikuwa wakitokea kwenye starehe

Aisee ndo maana nikiamua kwenda kulewa huwa sitoki na gari...
 
Issue ni kuendesha na kombania ndani!! Kama man alone mbona hata likikupata ni bahati mbaya!!?? Ila team!?
 
Ukweli ni kwamba ajali haikutokea Bunju B bali Maeneo ya mianzini ambayo ni Bunju A.

Imewaondoa duniani majirani watano wanaoishi sehemu moja... Ni msiba wa ujirani. Bahati mbaya zaidi dereva wa Lori aliyewagonga naye ni jirani akifahamiana vyema na marehemu wote....Wanne wameshazikwa na wa mwisho anazikwa leo, mida hii...

Majeruhi mmoja aliyesalia tayari kashatoka hospitalini.

Mungu yu mwema daima
Bunju tangu enzi hizo majirani walevi hukutana pamoja na kunywa pamoja hii tabia imekuwa n ibada sasa kunywa pamoja na unywaji wa kuhamahama.

Nakumbuka kipindi hcho tulikuwa tunatoka bunju saa nne usiku hapo tushalewa tunaenda sinza (meeda, ambiance au Hongera pale) alafu tunaanza kuja Mdogo Mdogo Ila tukifika boko pale ISAJE kipindi ndo iko Moto lazima kituo hapo hyo n saa nane au Tisa mwishoni watu wanamalizia mtaani hapo n kumwamsha anaetuuziaga bia hata Kama hatuna hela wazee wa kwa baharia unaingia ndani kidogo minazini enzi hzo mpoooh?

Haya maisha haya MUNGU alete uzima na kuzeeka vyema aisee
 
Watano Wafariki kwa ajali Bunju B Usiku wa Jmosi wakitokea Juliana Pub wakaja kumalizia huku njia ya Moga kuna baa inaitwa Lava Lounge.

Wakanywa tena hadi saa 10 wahudumu Waliwasihi sana walivyolewa hivyo wkalale logde ya huko huko msiendeshe lakini hawakuwasikiliza,

Wakaondoka, ndio wakati wanaingia main Bagamoyo Road pale Lake Oil Lori la mchanga likawagonga walikua 6 mmoja ni majeruhi.

Alipata kusema Albert Chalamila

"Sifa ya pombe ukinywa lazima ulewe..

Ukiona hulewi aidha pombe ina matatizo ya ubora au wewe mlevi una matatizo ya kiafya" 😀
 
Ukweli ni kwamba ajali haikutokea Bunju B bali Maeneo ya mianzini ambayo ni Bunju A.

Imewaondoa duniani majirani watano wanaoishi sehemu moja... Ni msiba wa ujirani. Bahati mbaya zaidi dereva wa Lori aliyewagonga naye ni jirani akifahamiana vyema na marehemu wote....Wanne wameshazikwa na wa mwisho anazikwa leo, mida hii...

Majeruhi mmoja aliyesalia tayari kashatoka hospitalini.

Mungu yu mwema daima
Case ngumu
 
Hatujambo mkuu. Hao wadau waliusimamisha mtaa kwa majonzi. Watu walishindwa waende kwenye msiba wa nani, maana ni majirani. Wakajikuta wanakutana baa ya jirani kuomboleza misiba yote kwa pamoja
Noma Sana
 
Hakuna mungu aliepanga siku ya kufa.

Ufe kwa uzembe wako uaingizie mungu?

Hata wazungu wenyewe waliounda hayo magari wanakwambia don't drink and drive, wewe ujifanye much know halafu useme mungu alipanga.


Kwani ndio Mara ya kwanza kuendesha amelewa?wangapi wanaendesha chakari Hadi wanasahau kwao na hawafi?...Mungu anajua siku yako ya kuzaliwa na ya kufa pia,kusema hajapanga trh ya kufa huu Ni upotoshaji bro.
 
Da. Wewe una akili nzito sana. Kwa nini sasa unapovuka barabara huwa unachukuwa tahadhari? Kwa nini usivuke tu bila kuangalia wala kujali chochote kwani ''kama siku yako haijafika'' hakuna kitakachokugusa? Pia kwenye maisha yako hata ukiugua usitafute tiba kwani kama siku yako haijafika hutakufa!
Sio akili nzito tu, huyo hana akili kabisa
 
Back
Top Bottom