Watano wafariki kwa ajali Bunju B usiku wa Jumamosi 26 Machi, 2022. Walikuwa wakitokea kwenye starehe

Watano wafariki kwa ajali Bunju B usiku wa Jumamosi 26 Machi, 2022. Walikuwa wakitokea kwenye starehe

Nilishuhudia hiyo ajali mwanzo mwisho. Aisee lile scania liliwapa kitu inayouma. Ile gari haikujulikana ni harrier, vanguard, fortuner au ni nini. Ila scania pia lilizingua.
 
mwisho wa mwezi baada ya kupokea mshahara tulia nyumbn na familia yako...uskute hao ni ndugu au marafik walisoma pmj wakaona sio mbali kutoka out na kwenda kuinjoi lkn kifo hakina taarifa poleni sana kwa msiba but ol n ol pombe ni haramu ..
 
Ukweli ni kwamba ajali haikutokea Bunju B bali Maeneo ya mianzini ambayo ni Bunju A.

Imewaondoa duniani majirani watano wanaoishi sehemu moja... Ni msiba wa ujirani. Bahati mbaya zaidi dereva wa Lori aliyewagonga naye ni jirani akifahamiana vyema na marehemu wote....Wanne wameshazikwa na wa mwisho anazikwa leo, mida hii...

Majeruhi mmoja aliyesalia tayari kashatoka hospitalini.

Mungu yu mwema daima
Duhh! suka aliamua kujipa kazi ya ziraeli
 
Hatujambo mkuu. Hao wadau waliusimamisha mtaa kwa majonzi. Watu walishindwa waende kwenye msiba wa nani, maana ni majirani. Wakajikuta wanakutana baa ya jirani kuomboleza misiba yote kwa pamoja
Kumbe wewe pia ni jirani yangu
 
Nilishuhudia hiyo ajali mwanzo mwisho. Aisee lile scania liliwapa kitu inayouma. Ile gari haikujulikana ni harrier, vanguard, fortuner au ni nini. Ila scania pia lilizingua.
Hiyo barabara usiku ni hatari sana sana. Malori yote mabovu ya mchanga ndiyo ''yanaamka'' usiku mrefu ukifika ili kukwepa polisi. Yanakwenda mwendo mbaya sana na madereva wake wengi ni watu wa bangi.
 
Hakuna kifo Cha kujitafutia,Ukiona mtu kafariki kwenye mazingira yeyote ujue tarehe yake ya ahadi imefika!hata angekuwa kalala chumbani roli lingekosea njia lingemfuata tu
Siyo kweli hata kidogo. Hata Mungu hakupanga siku ya kufa mtu. Ndiyo maana akakupa akili na utashi wa kujiamulia mambo yako. Mtu unalewa chakari halafu unaingia kuendesha gari unasema siku yako ndiyo imefika?
 
Kwani ndio Mara ya kwanza kuendesha amelewa?wangapi wanaendesha chakari Hadi wanasahau kwao na hawafi?...Mungu anajua siku yako ya kuzaliwa na ya kufa pia,kusema hajapanga trh ya kufa huu Ni upotoshaji bro.
 
Nakumbuka zamani Musoma Tarime road kuna mtu alipita jioni akienda Musoma kwenye ishu zake akiwa huko mvua inanyesha saa tatu usiku anarudi Tarime kufika mahali anapigiwa torch kwa nguvu asimame akaongeza moto akihisi ni majambazi, kumbe anaambiwa asimame mbele daraja limekata akaenda akajibamiza kwenye daraja na ikawa ndo mwisho wake, angeisikiliza torch angepona.
Tochi sio alama ya barabarani.Hata Mimi ningenyosha kwa speed
 
Watano Wafariki kwa ajali Bunju B Usiku wa Jmosi wakitokea Juliana Pub wakaja kumalizia huku njia ya Moga kuna baa inaitwa Lava Lounge.

Wakanywa tena hadi saa 10 wahudumu Waliwasihi sana walivyolewa hivyo wkalale logde ya huko huko msiendeshe lakini hawakuwasikiliza,

Wakaondoka, ndio wakati wanaingia main Bagamoyo Road pale Lake Oil Lori la mchanga likawagonga walikua 6 mmoja ni majeruhi.

Zao zimefikia r i p marehemu wote 5
 
Kwani ndio Mara ya kwanza kuendesha amelewa?wangapi wanaendesha chakari Hadi wanasahau kwao na hawafi?...Mungu anajua siku yako ya kuzaliwa na ya kufa pia,kusema hajapanga trh ya kufa huu Ni upotoshaji bro.
Da. Wewe una akili nzito sana. Kwa nini sasa unapovuka barabara huwa unachukuwa tahadhari? Kwa nini usivuke tu bila kuangalia wala kujali chochote kwani ''kama siku yako haijafika'' hakuna kitakachokugusa? Pia kwenye maisha yako hata ukiugua usitafute tiba kwani kama siku yako haijafika hutakufa!
 
Back
Top Bottom