Watano wafariki kwa ajali Bunju B usiku wa Jumamosi 26 Machi, 2022. Walikuwa wakitokea kwenye starehe

Watano wafariki kwa ajali Bunju B usiku wa Jumamosi 26 Machi, 2022. Walikuwa wakitokea kwenye starehe

Kifo bila maumivu..bata mpaka dakika ya mwisho..

Wenyewe wala hawajui kama wamekufa..

Kimbembe ni huko kwa Sir God! Watasemaje sasa wakifika wako tungi ndii na midomo inatoa puyapuya ya tusker baridi na kvant?

Hata hukumu yao itabidi iahirishwe pombe ziwaishe kichwani..
Kifo ni fumbo kali sana. Lakini kuna vingine huja na maonyo na kama wangewasikiliza wale wahudumu kwa ushauri wao wasingekufa.

Mshana Jr umewahi kusikia ushuhuda wa mtu mmoja alipewa maono ya kwenda mbinguni, sasa katika pitapita zake huko anaonyeshwa watu na vitu mbalimbali si akakuta kuna watu 2 wanahesabu pesa, akauliza hawa ni akina nani?

Akaambiwa hawa ni watumishi wa Mungu walikuwa duniani badala ya kuhubiri Injili ya kweli badala yake waliishia kugombania sadaka za waumini.

Kwahiyo utakuta masela huko waliko sasa wanapiga bia bila wasiwasi kila wakimaliza round moja inashuka nyingine.
Mambo ya Mungu yanatisha.
 
Si wangebaki tu mpaka asubuhi ndo waomdoke..

Ila kuna vifo vingine tunajitafutia wenyewe

Mungu atuzidishie hekima na busara
Hakuna kifo Cha kujitafutia,Ukiona mtu kafariki kwenye mazingira yeyote ujue tarehe yake ya ahadi imefika!hata angekuwa kalala chumbani roli lingekosea njia lingemfuata tu
 
Nakumbuka zamani Musoma Tarime road kuna mtu alipita jioni akienda Musoma kwenye ishu zake akiwa huko mvua inanyesha saa tatu usiku anarudi Tarime kufika mahali anapigiwa torch kwa nguvu asimame akaongeza moto akihisi ni majambazi, kumbe anaambiwa asimame mbele daraja limekata akaenda akajibamiza kwenye daraja na ikawa ndo mwisho wake, angeisikiliza torch angepona.
Miscalculated thoughts .. Unadhani ni kwa ubaya kumbe ni kwa wema..!
 
Hizi ni ajali mbaya na ukichunguza ni nguvu kazi za taifa,

tunawaomba polisi wasichoke waendelee kutoa elimu za usalama barabarani na kutoa taarifa ili watu waweze kujifunza kutokana na hizi ajali mbaya!!!

Kama Mimi napita pale kila siku na sijui kabisa taarifa za hiyo ajali, Jana nimesoma taarifa za ajali Kwa wiki mbili Kwa jumla watu 44, hiyo haikutajwa Bado bodaboda, polisi wanaficha ili iweje!?

RIP ndugu waliotutokaQUOTE]

Ni nguvu kazi ndio, baadhi ni vijana wa jeshi letu
 
Watano Wafariki kwa ajali Bunju B Usiku wa Jmosi wakitokea Juliana Pub wakaja kumalizia huku njia ya Moga kuna baa inaitwa Lava Lounge.

Wakanywa tena hadi saa 10 wahudumu Waliwasihi sana walivyolewa hivyo wkalale logde ya huko huko msiendeshe lakini hawakuwasikiliza,

Wakaondoka, ndio wakati wanaingia main Bagamoyo Road pale Lake Oil Lori la mchanga likawagonga walikua 6 mmoja ni majeruhi.

Inamaana na hiyo pisi hapo imeondoka? Kweli dunia ni mapito
 
Hakuna kifo Cha kujitafutia,Ukiona mtu kafariki kwenye mazingira yeyote ujue tarehe yake ya ahadi imefika!hata angekuwa kalala chumbani roli lingekosea njia lingemfuata tu
Sawa.Mimi nkiwa na utimamu wangu najaribu kuweka jiko la mkaa karibu na mtungi wa gesi.huku nikipuuza hisia kwamba litalipuka.naacha naendelea na shughuli nyingine kweli kunalipuka nakufa..nliandikiwa?

Unatoka hapa unaingia baharini kuogelea wakati unajua ni risk na hujui kuogelea.unazama unakufa unasema iliandikwa?

Hakuna yeyote aliyendikiwa chochote.Bali maisha yetu ni matokeo ya maamuzi yetu ama ya wengine.

Dereva wa Lori kwa maamuzi ake kaamua kwenda bar kupiga konyagi huku anajua anaendesha.anarudi kwenye gari anaacha njia anakuja kuvamia nyumba nliyopo kwa overspeeding. Mi nliandikiwa nife mapema kwa uzembe na ujinga wa mwingine?

Sikubaliani na hiyo hoja!
 
Mnavyosemaga kafa kujitakia,au kafa sio tarehe yake nyinyi mnafikiria alitakiwa kufa tarehe ngapi?
Ukiona umeenda kuogelea ukafa eti kisa hujui kuogelea wewe jua ndio siku yako ya kudepart imefika,course Kuna mamilioni ya watu Hawajui kuogelea wanaongia na kutoka humo baharini na hawajafa.
 
Back
Top Bottom