GEOPOLITICS KANDA YA MAZIWA MAKUU, EAC NA SADC
16 January 2025
Kigali, Rwanda
KAGAME ALIPUA WANA diplomasia
: '
Tshisekedi Ni Mjinga; Hajawahi Kushinda Uchaguzi Kongo, Na Mnajua Lakini Hamwezi Kusema Hadharani, Leo Nawaambia Live / Mubashara'
View: https://m.youtube.com/watch?v=lxfdT9kYBLA
Rais wa Rwanda amezidisha mvutano kati ya nchi yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuwalipua wanadiplomasia wakati alipokutana nao katika mkutano wa kila mwaka na mabalozi wa nje wanaowakilisha nchi yao mjini Kigali Rwanda jana.
Kagame alimtaja rais mlaghai wa DRC Felix Tshisekedi kama mjinga ambaye hakujua la kufanya kama kiongozi.
Alisema Tshisekedi hajawahi kuchaguliwa kihalali na ndiyo sababu vita mashariki mwa Kongo vinaongezeka.
Kagame anatuhumiwa kuwafadhili waasi wa M23 ambao sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya mashariki mwa DRC.
“Mtu (Tshisekedi) anayesababisha matatizo kati ya Rwanda na DRC hajawahi, mara mbili, kuchaguliwa na nyote mnajua. NA ninajua.
“Mtu huyu Tshisekedi hakuwahi kuchaguliwa, kwanza, hakuchaguliwa kabisa. Na unajua. Ni kwamba tu hatuiongelei hadharani na ninaizungumza hadharani sasa.
“Hiyo ndiyo tofauti. Mnaijua. Mara ya pili, hakuna kilichotokea. Na mnajua.”
Kagame aliongeza kuwa Tshisekedi hakuwa na sifa za uongozi.
“Nawafahamu viongozi ninapowaona. Pia najua wajinga ninapowaona.
"Unaweza kufikiria mchanganyiko wa wote wawili, janga ni.
"Kama wewe ni kiongozi na mjinga, ni balaa kabisa. Ni mbaya zaidi, hata hatari zaidi, ikiwa watu walewale walioshikilia mamlaka mikononi mwao wataamua kuwa watatumiwa na kuchezewa kwa maslahi fulani na wajinga,” alisema Rais Kagame.
Nchini Kongo kuna watu wanaongea Kinyarwanda, pia wilaya kadhaa za nchini Uganda lakini Uganda haisemi wale siyo raia wa Uganda ila Kongo kwa ujinga wao wanaamini raia wa Kongo wanaoongea Kinyarwabda siyo Wakongomani ! Huu ni ujinga na mbaya zaidi sehemu ya Jumuiya ya Kimataifa inakubali mtizamo wa Kongo!
Hili suala la Umoja wa Mataifa kulinda amani kwa miongo 3 yaani miaka 30 bila kufikiwa lengo la kuleta amani nchini Congo.
Hivyo ni jukumu la Rwanda kutafuta njia mbadala kuhakikusha usalama wake kwa kuwa inapakana na nchi iliyoshindwa kulinda usalama wake, huku viongozi wa Kongo wakifumbia macho Intarahamwe waliopo nchi jirani waliohusika na mauaji ya ya kimbari nchini Rwanda..
Inasikitisha jumuiya ya kimataifa chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa kuilaumu Rwanda wakati ni wao jumuiya ya kimataifa imeshindwa kusitisha vita nchini Kongo mbali ya kutumia mamilioni ya dolari, vifaa, na Majeshi ya Kulinda Amani chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa MONUSCO ...